Elections 2010 Dk Slaa amtaka Jk ataje waliopewa Sh1.7 trilion

Kaa la Moto

JF-Expert Member
Apr 24, 2008
7,903
1,053
Dk Slaa amtaka Jk ataje waliopewa Sh1.7 trilioni http://www.mwananchi.co.tz/componen...0YWplLXdhbGlvcGV3YS1zaDE3LXRyaWxpb25pLmh0bWw=Monday, 04 October 2010 07:34 digg

_dk%20wilbord%20slaa.jpg
Beatus Kagashe, Iringa MGOMBEA wa urais wa Muungano kwa tiketi ya Chadema , Dk Willibrod Slaa alimtaka mgombea wa CCM, Jakaya Kikwete kuwaeleza Watanzania ni kampuni zipi zilipata Sh 1.3 trilioni ambazo alisema amezitenga kwa ajili ya kukabiliana na mtikisiko wa kiuchumi duniani.
Katika mkutano mwingine uliofanyika Chimala wilayani Mbarali, Dk Slaa alimwomba mnadhimu mkuu wa Jeshi la Wananchi, Abdulrahman Shimbo kutoa ufafanuzi wa kashfa ambayo haijawahi kutolewa ufafanuzi hadi leo ya migodi ya Meremeta na Buhemba ambazo zinadaiwa kuchota kiasi cha Sh155 bilioni.
Rais Kikwete alitangaza mpango wa kunusuru uchumi kwa kutenga kiasi hicho cha fedha kukabiliana na mtikisiko wa kiuchumi uliozikumba taasisi za kifedha barani Amerika na Ulaya, mtikisiko ambao ulitarajiwa kutetesha uchumi wa nchi nyingine duniani. Kikwete alitangaza mkakati huo kwenye ukumbi wa Kilimani mjini Dodoma Juni 10 mwaka jana, ambao ulihusisha kutumia Sh21.9 bilioni kufidia wanunuzi wa mazao baada ya bei kushuka bila ya kutarajia, kutoa mitaji ya uendeshaji ya riba nafuu kwa mabenki, kutoa mikopo ya thamani ya Sh20 bilioni kwa benki ya TIB, kutoa Sh20 bilioni kwa ajili ya mikopo ydenye riba nafuu kwa ajili ya ununuzi wa zana za kilimo.

Mkakati mwingine ni kuongeza idadi ya wakulima watakaopata mbolea ya ruzuku na kiasi cha Sh90 bilioni kwa ajili ya mbolea hiyo na pia kuboresha Reli ya Kati kwa kutumia dola 43 milioni za Kimarekani.

Dk Slaa, ambaye pia ni katibu mkuu wa Chadema, anataka maelezo ya uchanganuzi wa matumizi hayo baada ya mwaka mzima wa utekelezaji wa mkakati huo uliowekwa kwenye bajetinya mwaka 2009/2010. Akizungumza kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika mjini Iringa, Dk Slaa alisema kuwa matumizi ya fedha hizo yanatia shaka kutokana na kutojulikana kwenye Bunge badala yake kutangazwa kwenye kikao cha CCM kilichoofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam.

"Nataka Kikwete atueleza ni makampuni gani yalipewa fedha hizo na yamezitumiaje," alisema Dk Slaa. “Hizi fedha ni za umma, lakini hakuna anayejua nani kanufaika nazo. Nitazishughulikia na kuhakikisha zinarudishwa kwenye matumizi ya umma.

” Alisema alifikia hatua ya kutaka maelezo hayo kwa kuwa dalili zinaonyesha kuwa matumizi ya fedha hizo ni ya shaka mno na kwamba hayana tofautiani na yale ya ukwapuaji wa Sh 133 bilioni uliofanywa kwenye Akaunti ya Malipo ya Nje (Epa) kati ya mwaka 2005/2006. Alidai kuwa pesa hizo zimewanufaisha baadhi ya mawaziri, wanafamilia na maswahiba wa Kikwete ambao wanaogopa kuwataja hadharani.

“Hizo fedha hazikupita bungeni, zilisomwa mbele ya mkutano wa wanachama wa CCM pale Mlimani City, mbona kampuni hazijulikani hadi leo. Tunataka tuzijue ni zipi na fedha zimegawiwaje kwa kuwa ni kiini macho; ni kama Epa nyingine,” alisema Dk Slaa. “Kama ni uongo, akanushe kama mwanawe na maswahiba zake hawachezi na raslimali zetu. Na kwanini atangazie Mlimani City kwenye kikao cha CCM,” alihoji. Aliahidi pia akiingia madarakani mwaka ujao atakagua fedha za serikali ya Kikwete kwa kuwa fedha hizo ni za umma na zimewanufaisha watu wachache tu.

Kuhusu kashfa ya Meremeta na Buhemba, Dk Slaa alisema badala ya Shimbo kujitokeza hadharani kuzungumzia uchaguzi mkuu, ni vizuri angejitokeza mapema kuzungumzia kashfa ya wizi wa fedha hizo unaodaiwa kufanywa na mgodi huo wa jeshi.

“Bilioni 155 zilipotea baada ya kuibwa katika mgodi wa dhahabu wa Buhemba. Sasa kama Shimbo ni muadilifu, ajitokeze hadharani kuwaeleza Watanzania fedha hizo ziko wapi... wizi ni wizi tu hata kama umetokea jeshini,” alisema Dk Slaa. Dk Slaa, ambaye amekuwa akiulizia suala hilo mara kwa mara bungeni ambako alikuwa akiwakilisha Jimbo la Karatu, alisema Waziri Mkuu ameshindwa kuto jibu la maswali kuhusu mgodi huo, kitu ambacho kinaacha dukuduku kwa Watanzania.

Dk Slaa pia aliongeza kuwa maduka ya jeshi nchini kote yameondolewa kodi, lakini bidhaa zinauzwa sawa na mitaani, kitu alichokielezea kuwa ni wizi mkubwa ndani ya jeshi hilo. Alisema pia atatumia siku 100 kushughulikia mgogoro wa bonde la Ihefu na Mbarali ikiwa atapewa ridhaa ya kuongoza nchi kwa kuwa hata baada ya maelekezo ya Kamati ya Bunge bado CCM imekuwa na kigugumizi kutekeleza.

“Hakuna mkataba ambao hauvunjwi hasa pale ambapo haukushirikisha wanajamii wa pale, mabonde yetu ila wamepewa wawekezaji na sisi tunalia hatuna cha kufanya, siku 100 nikiwa madarakani nalimaliza hili,” alisema Dk Slaa akizungumzia kitendo cha serikali kuwahamisha wafugaji kwenye bonde la Ihefu, Mbarali Machi 2006 bila ya utaratibu wala mipango. Alisema serikali ya CCM imekosa ubunifu wa kuendesha nchi ndio maana watu wanaobuni vitu wanakamatwa na kukatishwa tamaa.

Alitolea mfano wa kijana aliyebuni na kutengeneza gobore na wengine wanaorusha matangazo ndani ya kata zao kuwa wanakatishwa tamaa badala ya kupewa kipaumbele na kusaidiwa. “Huu ndio mwisho wa CCM, haina jipya la kuwaambia watu zaidi ya kukimbizana na wapika gongo, ubunifu Tanzania umekuwa ujambazi, huu ni mfumo mbovu na elimu duni,” alisema Dk Slaa.

Lakini pia, Dk Slaa alisema Chadema ni chama kinachomtegemea Mungu na nguvu za umma katika kuliongoza taifa hili kwa amani na mshikamano. Alisema kwa nguvu ya umma, Chadema imekubali kubadilika na kwamba sasa hakuna atakayeogopa vitisho katika mabadiliko kwa kuipa Chadema ushindi wa kishindo na kuitosa CCM. Alisema Rais Kikwete aliwahi kuulizwa na Rais wa Marekani sababu za Tanzania kuwa maskini wakati ina raslimali nyingi akajibu kuwa hajui.

“Kama hajui kwa nini nchi yake ni maskini, kwanini anaomba kura?” Mgombea ubunge wa Jimbo la Iringa Mjini kwa tiketi ya Chadema, Peter Msigwa alisema kwenye mkutano huo kuwa nyumba nyingi jimboni humo hazina hati na akaahidi kuwa iwapo atachaguliwa atapigana kufa na kupona kuhakikisha wananchi wake wanapata hati hizo.
 
Back
Top Bottom