Dk Slaa amshukia mama Anna Mkapa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk Slaa amshukia mama Anna Mkapa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by rosemarie, Jun 2, 2012.

 1. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #1
  Jun 2, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,768
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  Aidha, Dk Slaa alisema serikali kwa kujua iliamua kwa makusudi kumuuziauza kiwanda pekee cha korosho kilichopo mkoani Mtwara kwa sh. milioni 50 na kuwaacha wakazi wa mtwara wakihangaika na korosho zao pasipo kujua ni wapi watazipeleka.
  Alisema kama kiwanda hicho kingeachwa wakazi wa Mtwara wasingekuwa na taabu ya kujua ni wapi pa kupeleka korosho zao.
  “Taarifa nilizonazo kiwanda hicho alichouziwa mama Mkapa kimeondolewa mitambo yote na sasa kimebaki tupu na hakuna kinachoendelea juu ya hilo huku ninyi mkibaki na umasikini wenu”alisema Dk Slaa
  ATAKA MAAFISA USALAMA WA TAIFA WARIPOTI KWAKE
  Akizungumzia hali ya usalama Dk Slaa alisema kuanzia sasa ni lazima maafisa hao wakaripti kwake kila atakapokuwa akifanya mikutano kwa kuwa huo ndiyo wajibu wao.
  Alisema kazi ya polisi ni kufanya kazi ya kulinda wananchi na usalama wa taifa wanawajibu wa kuangalia usalama kwa ujumla na katika taratibu hizo ni lazima wawasiliane naye kabla ya mikutano hiyo kuanza.
  Aliongeza maagizo hayo ni kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 2005 inayoelekeza wajibu wa maafisa wa usalama wa Taifa.
  MNYIKA ASHANGAA MAJIMBO YA WENZAKE
  Akizungumza katika mkutano huo Mbunge wa ubungo John Mnyika alisema kilichomvuta kufika katika majimbo ya wenzake ni kuona wamefanya maendeleo kiasi gani hata kuamua kuwa mabubu wanapokuwa bungeni.
  Alisema ukimya wa wabunge hao ulimfanya kila siku awe anpiga kelele kwa ajili ya mahitaji muhimu ya wananchi kwa kile alichoamini kuwa wenzake wako mbali kimaendeleo.
  “Nilijua kuna maendeleo zaidi ya majimbo yetu ya Dar lakini katika haya niliyoyaona nimekosa hata hamu ya kuwa pamoja na hao mliowachagua kuwa wawakilishi wenu”alisema Mnyika
  HECHE AZUNGUMZIA UDINI
  Mwenyekiti wa Taifa wa Bavicha John Heche akihutubia katika kata ya Namikupa Tandahimba alisema propaganda za udini zinazoelekezwa kwa chama chake ni mawazo ya watu waliofilisika kisiasa.
  Alibainisha kuwa hata mtu akiwa ni kiongozi kutoka katika dini inayowahusu na hafuati maagizo ya dini kuwakomboa wananchi basi dini yake haitakuwa na maana kwa jamii inayomzunguka.
  WANANCH WAMKATAA MBUNGE TANDAHIMBA
  Katika hali isiyo ya kawaida maeneo mbali mbali kulipofanyika mikutano ya hadhara wananchi walipiga kura ya kumkataa mbunge wao Juma Njuwayo huku wengine wakisema hawamjui wala hawataki kumuona.
  Wakazi wa Namipuka walisema mara ya mwisho kuonekana kwa mbunge huyo ni pale alipofika kuwaomba kura na baada ya hapo hajawahi kuonekana tena huku wakiomba uchaguzi mwingine ufanyike katika jimbo lao kwa ajili ya kupata mtu wa kuwasemea.
  Katika uwanja wa Tandahimba kila mara lilipotajwa jina la mbunge huyo wananchi walisema hatumtaki ameiba kura hatumtaki hatuna mbunge huyo ni mbunge wa ccm na siyo wetu sisi


   
 2. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #2
  Jun 2, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,544
  Likes Received: 10,481
  Trophy Points: 280
  hongera chadema kwa kuwaamusha watanzania.!
   
 3. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #3
  Jun 2, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Naona giza limeondoka kwa wanamtwara na wanataka nuru. Viva CDM
   
 4. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #4
  Jun 2, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,320
  Likes Received: 5,611
  Trophy Points: 280
  Kiwanda kingine cha Kubangua Korosho alinunua aliewahi kuwa naibu waziri wa fedha awamu mkapa..Abdisalom Issa Hatibu!!(Mzanzibari) sijajua kama kiwanda kinafanya kazi au amegeuza ghala kuhifadhia korosho na mazao mengine!!!!hawa watu wa kusini wanahitaji mkakati maalumu kuwakomboa kwa kweli!!!wamezaliana sana hakuna cha maana kule ndio maana wanazunguka na vitu mikononi mijini......hatari sana
   
 5. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #5
  Jun 2, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,527
  Likes Received: 19,949
  Trophy Points: 280
  amshukia tena ..tumieni kiswahili vizuri mm nimefungua fasta fasta
   
 6. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #6
  Jun 2, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  Fungukeni makamanda! Naona wale wenye chuki na Heche roho zinawauma.....! Heche piga kazi kaka utuwakilishe vijana wenzako na achana na vijana wenye majungu hasa wale uliowatoa majasho kwenye uchaguzi wa BAVICHA.

  PEOPLE'S.. POWER"
   
 7. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #7
  Jun 2, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,202
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Afadhali tumekubalika huko kusini tofauti na matarajio ya Ribosome, Ritz na Rejao Chezea CDM na Mtwara Nyinyi!!!!!!!!! Mtwara itakuwa kama Beghazi
   
 8. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #8
  Jun 2, 2012
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 271
  Trophy Points: 180
  skills4ever uko sawa kiongozi, wakionja tamu ya M4C watajuta kuifahamu ccm. Miaka yote wanalima korosho lkn bd haiwakomboi. Wafanye uamuzi sasa wa kumfurusha mkoloni mweusi CCM watafaidije Uhuru kamili km magamba hawatoki
   
 9. Arvin sloane

  Arvin sloane JF-Expert Member

  #9
  Jun 2, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 963
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Hivi kumshukia maana yake nini?? kuuliza sio ujinga coz sielewi maana ya hili neno.
   
 10. MANI

  MANI Platinum Member

  #10
  Jun 2, 2012
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,413
  Likes Received: 1,873
  Trophy Points: 280
  Mkuu vipi ulidhani nini?
   
 11. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #11
  Jun 2, 2012
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,501
  Likes Received: 1,082
  Trophy Points: 280
  Kingine kilichoko mkoa wa pwani alikinunua Ali Hassan Mwinyi rais mstaafu alie mmilikisha binti yake.
  Watu wa ajabu sana hawa mwalimu alivijenga viwasaidie watz wao wanauziana!
   
 12. DCONSCIOUS

  DCONSCIOUS JF-Expert Member

  #12
  Jun 2, 2012
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 1,272
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Wapi ritz?
   
 13. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #13
  Jun 2, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  Mtabadilisha mada sasa hivi. mbona kilichomchanganya Saint Ivuga kiko obvious kabisa,tujadili alichokikuta sasa.
   
 14. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #14
  Jun 3, 2012
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  Hata Uzini mlisema mmepokelewa kwa mikono miwili na umati mkuubwa wa watu. Mlichoambuli kwenye kura zilizopigwa, kukitaja hapa ni kuendelea kuwafedhehesha!
   
 15. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #15
  Jun 3, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,812
  Likes Received: 3,893
  Trophy Points: 280
  mbona uchangiaji wako hapa JF huwa ni dhaifu sana? kwa nini usizungumzie mada husika hasa kuuzwa kwa kiwanda cha kubangua korosho na kung'olewa mitambo? wakazi wa tandahimba kumkataa mbunge wao na hali halisi ya umaskini kusini mwa nchi unarukia uzini ambayo wakazi wake ni wachache kuliko kata ya usariver kule Arusha??
   
 16. monongo

  monongo JF-Expert Member

  #16
  Jun 3, 2012
  Joined: Oct 25, 2011
  Messages: 370
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  asiye na hili ana lile,ukiona mtu asieona wakati yeye anasema anaona, ujue kuwa huyo ni Pambafuuuu mkubwa.viwanda karibu vyote alivyoacha JK.Nyerere,havipo,ila majengo yamebaki ndio magodown ya wahindi na waarabu,kwa ajili ya kutunzia mizigo yao.Mungu tusaidie janga hili la magamba liondoke na ikiwezekana life kabisa!!
   
 17. magosha

  magosha JF-Expert Member

  #17
  Jun 3, 2012
  Joined: Apr 25, 2012
  Messages: 641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  m4c lamba nchi nzima.
   
 18. sinafungu

  sinafungu JF-Expert Member

  #18
  Jun 4, 2012
  Joined: Feb 13, 2010
  Messages: 1,406
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  huyu mama muda ukifika nitafurahi saaaana akifikishwa kwa vyombo vya sheria amfuate aliyekuwa rais wa Misri. wametumalizia TTCL YETU, wakaunda kampuni tanzu kusimamia ununuzi wa mali za TTCL, mwenyekiti wa kampuni hiyo akawa mwanaye aliyemzaa na Mr Mramba. akamuuzia jengo la makazi ya wafanyakazi ya wafanyakazi , kwa bei ya kutupa. lile jeno liko pale ilala baada ya ofisi ya mkuu wa mkoa. njia ya kwenda kigogo, huyu mama kwa hakika sina raha naye yeye na mume wake hadi mwisho wa maisha yangu.
   
 19. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #19
  Jun 4, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,527
  Likes Received: 19,949
  Trophy Points: 280
  asante kiongozi ...tujadili kilichopo
   
 20. I

  ISIMAN Member

  #20
  Jun 4, 2012
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 72
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  eyes on hands on too man to man
   
Loading...