Dk. Slaa aliipatia CHADEMA wabunge zaidi ya 30, Lowassa ameipatia CHADEMA wabunge 22

Wewe unajua nini kuhusu chadema:what: au povu linakutoka bure kama ngiri aliekoswa na chui, inamaana wabunge 70 kwa 48 wengi wepi:what: au nyie ndio wale mliopunguziwa maksi ili mfaulu:what:

Hicho ni kiwango cha mwisho kabisa cha mtu kufikiri. Wewe unachoshindwa kuelewa hapa ni hiki; Dk. Slaa aliongeza wabunge zaidi ya 30 kutoka idadi iliyokuwepo kabla ya yeye kugombea wakati Lowassa kaongeza wabunge 22 kutoka idadi iliyokuwepo kabla ya yeye kugombea.
 
Umevurugwa, Kila uchaguzi ni kuanza upya hakuna anaye endelea na ubunge bila kuchaguliwa upya.
Hang over ya uchaguzi ukitaka ikitoke haraka, kazimue kwa kufanya kazi kwa bidii.
 
Mimi ni mwanachama wa cdm, kiukweli ndn ya siasa zinazoendelea kukomaa ndn ya tz dr cassava asineweza kuongeza wabunge wng hivi mwaka huu.
 
Wengine tunaangalia Ukawa imefaulu vipi wewe unaongelea chadema na Slaa....

Wakati umetazama ubunge peke yake hujaona halimashauri za wilaya na majiji ambayo Ukawa imechukua...

Pole sana kwa kuzimikia majina ya watu
 
Jiji la Dar mikononi mwa UKAWA chini ya amsha amsha za EL. Endeleeni kukamata Kongwa, UKAWA ni majiji matatu kati ya manne!
 
Jiji la Dar mikononi mwa UKAWA chini ya amsha amsha za EL. Endeleeni kukamata Kongwa, UKAWA ni majiji matatu kati ya manne!

Dar es Salaam
Tanga
Arusha
Moshi
Mbeya

Kwa Dar makosa tu ya kiufundi lakini ccm asingepata hata jimbo moja
 
Ukitaka ku kokotoa asilimia ya kumlinganisha lowassa na slaa, kwa slaa utakokotoa hiyo 48-10/10 x 100, then wa lowassa chukua 71-48/48 x 100(CDM ) + 23-2/2 x 100 (CUF) + 4- 1/ 4 x 100 (NCCR) Then linganisha majibu kuwa nani amekuwa na impact
 
hivi kutoka kura ml 2 mpaka kura ml 6 kama kichwani ni mzima utajua kati ya dr slaa na lowassa nani kakiletea chama faida? kutoka 48 wabunge mpaka 70 kama uoni tofauti kamwone dr wa Akili Ndugu.

Huyo muanzisha thread ni mpotoshaji mkubwa 2010 CDM ilikuwa na viti vya kuchaguliwa 22 na sio 30 na jumla ya wabunge 48',sasa hivi wabunge wa majimbo 35 na jumla ya wabunge 72. Kwa maoni yangu ni mpuuzi tu anayeweza kudharau impact ya Lowassa kwa UKAWA na siasa za nchi kwa ujumla.
 
Vipi Halmashauri za miji na majiji?? vipi madiwani? vipi sehemu amba CDM wamepoteza majimbo? angekuwepo Slaa kwa case yako ya wabunge pekee unadhani CDM ingepoteza majimbo mangapi na kupata mangapi??

nasubiri jibu lako
 
Wakati aliyekuwa katibu mkuu wa CHADEMA, Dk. Wilbrod Slaa anagombea Uraisi mwaka 2010, CHADEMA ilikuwa na wabunge wa kuchaguliwa na viti maalumu wasiozidi 10 ( Ndesamburo, Zitto Kabwe, Dk. Slaa, Halima Mdee na wengineo) baada ya uchaguzi CHADEMA ilivuna viti vya ubunge zaidi ya 30 na kuifanya iwe na wabunge wa kuchaguliwa na viti maalumu wapatao 48 na hivyo kuunda kambi ya rasmi ya upinzani bungeni. Lakini hali ya mambo imekuwa tofauti kabisa mwaka huu wa 2015 ambapo CHADEMA ilimsimamisha ndugu Edward Lowassa kama mgombea wa Urais huku akiungwa mkono na vyama vya CUF, NCCR na NLD kwani CHADEMA imepata wabunge wa kuchaguliwa na viti maalum wapatao 70 ambalo ni ongezeko la wabunge 22 tu kutoka wabunge 48 waliowapata mwaka 2010. Hivyo basi CHADEMA kwa kumsimamisha Lowassa mwaka 2015 kama mgombea wake kimepata wabunge wachache ukilinganisha na wabunge waliowapata mwaka 2010 kwa kumsimamisha Dk. Slaa kama mgombea wake bila ya kuungwa mkono na chama chochote.

Si bure warogwa wewe...
 
Watu wengine huwa sijui wanaenda shule zipi?

Ina Maana wakati Dr. Slaa anajiunga CHADEMA chama hakikuwa na wabunge? Je hao wabunge tokea atoke wamepungua au kuongezeka?

Ni Halmashauri ngapi za Wilaya, Msnispaa na Majiji CDM iliziongoza na Mwaka huu ni Kiasi gani?

Je ni madiwani Wangapi CDM ilipata mwaka 2010 ukilinganisha na 2015?

Je unafahamu kuwa CCM imeathirika sana Kiruzuku mwaka huu kuliko 2010 na CDM kuongeza maradufu ruzuku yake?

Hata hivyo mwaka 2010 CDM ilikuwa na Wabunge 24 na siyo hizo Stastics zako za uongo!!!
 
Back
Top Bottom