Dk. Slaa aibuka na Nyaraka za SIRI

sir.JAPHET

JF-Expert Member
May 18, 2012
699
133
Jumatano, Agosti 15, 2012 06:11 Na Mwandishi Wetu, Mikumi

dk.%20slaa.jpg
Dk. Wilbrod Slaa

KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willbrod Slaa, ameibuka na kusema anazo nyaraka za siri, kuhusu mauaji ya faru yaliyofanyika hivi karibuni katika Hifadhi ya Serengeti, mkoani Mara.

Dk. Slaa, alisema nyaraka alizonazo zinaonyesha kuna mtandao mkubwa wa ujangili, unaohusisha vigogo wakubwa serikalini, watumishi wa vyombo vya dola, askari polisi na watumishi wa Idara ya Usalama wa Taifa.

Dk. Slaa alitoa kauli hiyo juzi, wakati akiwahutubia mamia ya wananchi wa vijiji vya Kata ya Malinyi, Mikumi na Ruaha.

Alisema nyaraka hizo, zinaelezea kiundani suala zima la mtandao wa ujangili.

Alisema mauaji ya wanyama adhimu faru, yaliyofanyika katika Mbuga ya Serengeti, ni dalili ya hujuma kubwa katika sekta ya maliasili ambazo zinafanywa na mtandao huo.

Alisema kumekuwapo na tabia ya kuwanyamazisha wabunge wanaotaka kupanua mjadala wa ufisadi mkubwa unaoendelea kuteketeza maliasili za nchi, wakiwamo twiga na faru.

"Naliomba Bunge kuacha kuminya mijadala, inayolenga kuibua matatizo ambayo tunaweza kuyatafutia tiba katika sekta mbalimbali za uchumi na maendeleo ya nchi… ninashangazwa kuona Serikali inaendelea kufumbia macho mtandao huo.

"Watanzania wenzagu wa Ulanga, hii ndiyo hali halisi namna ambavyo Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), imetufikisha hapa tulipo leo, ufisadi umetamalaki kila mahali, leo hapa ninazo mkononi kwangu nyaraka za siri zinazoelezea namna ambavyo faru wetu, wale wanyama adimu walivyouawa hivi karibuni huko Serengeti.

"Kwa mwananchi wa kawaida, inaweza kuwa vigumu kuelewa haraka umuhimu wa faru katika masuala ya uchumi.

"Kwa wale wanaofuatilia Bunge, watakuwa wameona juzi Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa (Chadema), alivyoambiwa bungeni baada ya kuibua suala hili la kuuawa kwa faru…mimi sitaki kuingia huko kwenye kamati yao na kile wanachofanya.

"Lakini nyaraka nilizonazo hapa zinaeleza bayana namna ambavyo faru hao waliuawa, huku wahusika, wakiwemo askari polisi majina wametajwa hapa, maliasili zetu wakiwemo wanyama, ziko hatarini kumalizwa kutokana na uzembe wa serikali kulea ufisadi.

"Kama Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki anaona kuna mahali angeweza kuchukua hatua, lakini anashindwa kwa sababu kuna watu wengine wanapaswa kuchukua hatua zaidi," alisema.

Pamoja na mambo mengi, ameiomba Serikali kuwachukulia hatua kali wale wanaothibitika kufanya vitendo vya ubadhirifu wa mali za umma
 
hivi ulanga ndo alibwagwa yule mtangazaji wa ITV kwenye kura ya maoni ya magamba?
 
tatizo hapa ni kua serikali na viongozi hawajali pigeni makelele ongeeni kwenye majukwaani...mwisho wa siku wao ndio wanaenda benki kuingizia dola million 20 kwenye account yake wakati nyie mnapigwa na jua kulalamika
 
Dr. Kaibuka upya! Angekua mto tungesema kwa kizungu ( river rejuvination)

Hahaha River rejuvination ni topic niliyoipenda sana A-Level lakini haikutoka kwenye mtihani wa taifa sasa DR anataka kuitoa bila hata supervision, safi sana go on huko maliasili ni uozo mtupu
 
Hivi thamani ya pembe (sijui meno) ya Fru ni shilingi ngapi? Na huwa kwa Faru mkubwa hiyo pembe huwa inakuwa na uzito gani? Msaada kujua tafadhali.
 
Dr. Kaamua kujiundia CIA na KGB binafsi ambayo inachunguza, inathibitisha, na kujiridhisha kiushahidi alafu ina report directly kwa wananchi! Ni nomaaaaaa! Ole wako uwe muovu alafu juzi hukuchangia kwenye harambee ya CDM jina lako la kwanza kutajwa. Bora Filikunjombe kajiwahi mapema!
 
Wakati fulani alipata kusema kuwa yeye si mtu wa kukurupuka. Akitoa 'bomu' ujue lina ukweli 100%.
 
Dr Slaa ebu wataje hao vigogo tuwajue sio tu kusema unazo nyaraka za siri Dr Slaa, ulishawai kutuambia kuwa kuna umekamata kontena mbili umezikamata Tunduma zimejaa karatasi za kupigia kura kutoka China zilipolikuja kufunguliwa na polisi mbele ya viongozi wa Chadema wakakuta vipodozi Dr Slaa akawakimbia waandishi wa habari...tumeishakuzoea.
 
Yule sharobaro wa Singida alieteuliwa kuwa waziri wa wizara hiyohiyo sidhani kama atasalimika...tusubiri tuone.... jiwe ndo lisharushwa gizani....mfuka povu wa kwanza anahusika..
 
Dr Slaa ebu wataje hao vigogo tuwajue sio tu kusema unazo nyaraka za siri Dr Slaa, ulishawai kutuambia kuwa kuna umekamata kontena mbili umezikamata Tunduma zimejaa karatasi za kupigia kura kutoka China zilipolikuja kufunguliwa na polisi mbele ya viongozi wa Chadema wakakuta vipodozi Dr Slaa akawakimbia waandishi wa habari...tumeishakuzoea.
haha sasa gamba linawasha au linachoma? subiri kaa mkao wa kula safari hii mtachekea bafuni! Doctor huwa hana papara kwani alipotaja ile list of shame ya mafisadi pale mwembe yanga nani alikanusha??Msigwa kasema Kagasheki alitia aibu kwenda kupokea faru toka uingereza wakati faru wapo hapa kagasheki kasema hajawahi kupokea faru Msigwa kamwaga picha kagasheki anashikana mkono na balozi mzungu kushukuru CDM we acha tuuu!!
 
Aiseee! baba yangu Dr.Slaa na Dr Kikwete mbona majina yao ya mwanzo yanafanana (Dr) lakini maamuzi wanayofanya ni tofauti.Dr ipi ndio inadhamani ya jei kei au ya slaa?

Naombeni majibu kabla sijamaliza mbege.
 
[/QUOTE]Wewe kweli osokoni Mbowe anavyompa JK mkono au siku ile Chadema walivyokwenda Ikulu wote walikuwa wanampa mkono JK walikuwa wanashukuru nini? Vipi zile kontena zipo wapi?
 
Back
Top Bottom