Dk Slaa afunguka

Molemo

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
14,620
Reaction score
13,361
Katibu Mkuu wa Chadema Dr Wilbroad Slaa amefichua mkakati kabambe uliopangwa na chama hicho wa kujiimarisha ndani ya miezi 6

Dr Slaa amesema kuanzia Aprili mpaka Septemba mwaka huu kutakuwa na operesheni kubwa ya M4C nchi nzima ambayo anaamini itatikisa nchi.

Dr Slaa amesema operesheni hiyo itafanyika kwa wakati mmoja nchi nzima na zitaongozwa na makamanda mbalimbali wa chama

Kiongozi huyo anayeogopwa na Mafisadi amesema kwa kipindi hicho cha miezi 6 chama kimejiwekea malengo ya kuvifikia vijiji 18000 na kuzindua matawi ya chama 18000 na pia yatazinduliwa mashina ya msingi 50000.

Kiongozi huyo ameendelea kusema M4C itaimarisha misingi ya chama vijijini.Katika kila kaya 30 za Familia Chadema itakuwa na kiongozi atakayeitwa Balozi na katika kila kaya 10 kutakuwa na shina ambalo litaitwa ngazi ya msingi ya uongozi.

Baada ya kukamilisha mpango huo kutakuwa na waratibu wa M4C ngazi ya Kijiji,Kata,Jimbo,Wilaya,Mkoa na mwisho ngazi ya Kanda.

Dr Slaa amesema Chadema itaishangaza CCM katika uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka 2014 na utakuwa ndio mwanzo wa mwisho wa utawala wa CCM.

Source:Raia Mwema.
----------------------
HABARI KAMILI
---------------------

 
:majani7::majani7:Hureee Dr sio muda wa kulala sasa hivi hadi kieleweke,hadi wachanganyikiwe,mnavyozidi kukaa huko maofisini mnapoteza muda,mguu kwa mguu,wakitoa mnabandika hadi wapige kelele,mnavyotulia wanazidi kuwadanganya wananchi msiruhusu hali hiyo tokeni ofisini sio muda huu wa kukaa ofisini,ofisini ni baada ya 2015
 

Cha msingi hapa ni kuomba uzima toka kwa Mungu"tulianza na Mungu tutamaliza na Mungu"
 
Ni vitisho au kweli????

Dk. SLAA alikuwepo hivi punde kwenye Uzi huu akisoma comments mbona kapotea bila kujibu chochote?
 
hadi kieleweke, mchakamchaka huu magamba hauuwezi, futa nyayo za msomali mnafiki ambaye anahubiri asiyotenda
 
Mkuu hii M4C ya kuanzia mwezi wa nne ni lazima nishiriki, ikishindikana kabisa basi nitato mchango wangu wa hali na mali hata kama utakuwa mdogo, CCM walisha tufanya Mazuzu, mpaka wamefikia kuzuia Bunge lisirushwe live ili wawe wanalaa bungeni na nina uhakika kama halitaonyweshwa mahudhurio yatakuwa hakuna wabunge wengi wa Magamba watakuwa kwenye dill zao
 
mwendo mdundo kwa speed hii break ikulu 2015 hakuna kuwapa pumzi jamaa ya kujipanga. Aluta continua....
 
Kijijini kwetu kuna watu 876 na wote ni wa ukoo mmoja. Mkijaribu kusogelea yatakayowapata msilalamike.
 

Mkuu chasa hili swala la Makinda kuzuia bunge kurushwa tayari ni Agenda maalum na ni kati ya kete zitakazotumiwa na Chadema kwenye operesheni hii.

Chadema itawaeleza waziwazi haya ni maamuzi yaliyofikiwa na Kamati kuu ya CCM ili wananchi wasigundue uovu unaoendelea bungeni.

Wananchi wataombwa kuiunga mkono Chadema ili ipate wabunge wengi wakawarudishie wananchi haki yao ya kuona bunge lao kupitia TV.
 
Last edited by a moderator:

Safi sana, Hii iwe ni Moja ya Agenda, Maknazania CCM wamezamilia kijichimbia makabuli yao wao wenyewe, Hii ishu ya Bunge itawaghalimu sana Magamba, na kama wanazani watawakomoa Wapinzani wameumia, Na mimi kuanzia keshi kila nitakaye kutana naye ni Elimu ya Uraia ikiwemo hili la kuzuia Bunge, kitaeleweka tu
 
Mbio za sakafuni...

Hayawi hayawi mwishowe....... na dua la kuku halimpati........Hakuchi, hakuchi mwishowe.....

misemo ya kiswahili inapingana kutegemea mhusika analenga nini.

mfano: haraka haraka haina baraka pia ngojangoja yaumiza matumbo au polepole ndio mwendo na chelewa chelewa

utakuta mwana si wako - tufuate kipi


Nakutakia usiku mwema shekhe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…