Ngandema Bwila
JF-Expert Member
- Sep 8, 2010
- 1,017
- 258
Sijasikia strategy ya CCM
Strategy yao ni ZUIA/ Fungia. Zuia mandamano, fungia magazeti, Fungia TV live! Upoozi?
Sijasikia strategy ya CCM
Zero, hujambo?
Katibu Mkuu wa Chadema Dr Wilbroad Slaa amefichua mkakati kabambe uliopangwa na chama hicho wa kujiimarisha ndani ya miezi 6
Dr Slaa amesema kuanzia Aprili mpaka Septemba mwaka huu kutakuwa na operesheni kubwa ya M4C nchi nzima ambayo anaamini itatikisa nchi.
Dr Slaa amesema operesheni hiyo itafanyika kwa wakati mmoja nchi nzima na zitaongozwa na makamanda mbalimbali wa chama
Kiongozi huyo anayeogopwa na Mafisadi amesema kwa kipindi hicho cha miezi 6 chama kimejiwekea malengo ya kuvifikia vijiji 18000 na kuzindua matawi ya chama 18000 na pia yatazinduliwa mashina ya msingi 50000.
Kiongozi huyo ameendelea kusema M4C itaimarisha misingi ya chama vijijini.Katika kila kaya 30 za Familia Chadema itakuwa na kiongozi atakayeitwa Balozi na katika kila kaya 10 kutakuwa na shina ambalo litaitwa ngazi ya msingi ya uongozi.
Baada ya kukamilisha mpango huo kutakuwa na waratibu wa M4C ngazi ya Kijiji,Kata,Jimbo,Wilaya,Mkoa na mwisho ngazi ya Kanda.
Dr Slaa amesema Chadema itaishangaza CCM katika uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka 2014 na utakuwa ndio mwanzo wa mwisho wa utawala wa CCM.
Source:Raia Mwema.
----------------------
HABARI KAMILI
---------------------