Dk. Slaa abeba makombora 20 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk. Slaa abeba makombora 20

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Selous, Aug 4, 2010.

 1. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #1
  Aug 4, 2010
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Dk. Slaa abeba makombora 20

  • CCM nao waandaa mamluki kummaliza

  na Waandishi wetu

  MGOMBEA urais kupitia Chama cha Maendeleo na Demokrasia (CHADEMA), Dk. Wilbrod Slaa, ameandaa makombora yapatayo 20 yatakayotumika kukimaliza Chama Cha Mapinduzi (CCM) na mgombea wake, Rais Jakaya Kikwete, kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.

  Tayari Rais Kikwete na chama chake wameanza kushtuka kuhusu makombora hayo, kwani yamefanyiwa utafiti wa kina na yatatumika kuanika uozo uliokithiri uliofanywa na Serikali ya Awamu ya Nne; na yatatumika kama silaha ya Dk. Slaa katika kuusaka urais.

  Vyanzo vya habari kutoka ndani ya chama hicho kikubwa cha upinzani nchini, vimeliambia Tanzania Daima Jumatano kuwa hata hivyo Dk. Slaa hatalipua mabomu hayo hadi kampeni zitakapoanza rasmi mwishoni mwa mwezi huu.

  Chanzo cha habari kilisema: “Anachokifanya Dk. Slaa hivi sasa ni kujitambulisha kama mgombea, pia kuomba kudhaminiwa, hajaanza kampeni. Atakapoanza mtaona mambo mazito yenye ushahidi wa nyaraka zinazoonyesha ufisadi uliofanywa na viongozi wa serikali katika kipindi hiki cha miaka mitano.”

  Katika baadhi ya mikutano yake ya hadhara ya kuomba kura, Dk. Slaa mwenyewe amekuwa akiwaambia wananchi kuwa ana mambo mazito yanayohusu ufisadi wa serikali. Baadhi ya mambo hayo amekuwa akiyahoji bungeni kila alipopata nafasi, lakini hayajawahi kupatiwa majibu.

  Dk. Slaa ambaye amejipatia umaarufu kutokana na kufanyia utafiti kila jambo analolizungumza, amekuwa akiwaahidi wananchi kuwa kwa vile yuko kwenye mikutano ya kuomba udhamini, ataanza kufyatua makombora hayo wakati wa kampeni.

  Itakumbukwa kuwa Dk. Slaa ndiye aliyelipua bungeni bomu la ufisadi mkubwa kupitia Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA); na ndiye alitaja orodha ya mafisadi 11 wakiwamo Rais Kikwete, aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu, Daudi Ballali, Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz, Mwanasheria Mkuu wa Serikali wa zamani, Andrew Chenge, waziri wa fedha wa zamani, Basil Mramba na makatibu wakuu, Patrick Rutabanzibwa na Gray Mgonja. Baadhi yao wako mahakamani; wengine tuhuma zao zinaendelea kuchunguzwa.

  Walitajwa pia Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono, Rais mstaafu, Benjamin Mkapa na aliyekuwa waziri wa nishati na madini, Nazir Karamagi.

  Na ingawa viongozi wakuu walianza kwa kumbeza na kuwateta ‘mafisadi,’ hivi sasa nao wanajitapa kuwa wameshughulikia ufisadi.

  Tangu alipotangaza kuwania urais, Dk. Slaa amewashtua viongozi wakuu na wanachama wa CCM, kiasi kwamba kwa nyakati tofauti Mwenyekiti wake, Rais Kikwete na Katibu Mkuu, Yusuph Makamba, wametoa kauli zinazoonyesha kiwewe walichonacho.

  Dk. Slaa, ambaye alifanya kazi kubwa katika Bunge la Tisa, hakuwa akitajwa sana kugombea urais, lakini baada ya CHADEMA kufanikiwa kumshawishi aingie kwenye mbio za Ikulu, ameonekana kuongeza nguvu na umaarufu wa CHADEMA, chama ambacho sasa ndicho kinaonekana tishio kwa CCM.

  Hata juzi Rais Kikwete aliporejea kwenye ofisi ndogo za makao makuu ya CCM baada ya kuchukua fomu ya kugombea tena urais, aliwaonya wana CCM wasidharau upinzani, bali wajiandae kufanya kampeni kali ili waweze kushinda.

  Aliwaasa waachane na kauli kwamba CCM itatawala milele.

  Tanzania Daima limezungumza na vigogo kadhaa wa CCM ambao wamekiri, bila kutaka majina yao yatajwe, kuwa wasipokaa vizuri Dk. Slaa anaweza kujenga wimbi la harakati zinazoweza kuifanya CCM ijikute nje ya serikali au ishinde kwa taabu.

  Tayari zipo taarifa zisizothibitishwa kwamba CCM imeshaanza kujipanga kumkabili Dk. Slaa, kwa kuandaa majeshi ya kukodi na kufadhili ili yakisaidie kumshambulia kampeni zitakapoanza, kama njia ya kumpunguza makali.

  Baadhi ya viongozi wa vyama vidogo vya siasa na vyombo vya habari vyenye uhusiano na CCM wametajwa kuhusika na njama hizo kwa kupewa ujira mdogo na CCM.

  Miongoni mwa hoja wanazoandaa kutumia kama silaha zao ni imani ya Dk. Slaa, ili kumpambanisha na wananchi wasiofuata imani yake; na masuala binafsi kuhusu familia yake.

  Hata hivyo, baadhi ya wachambuzi wameonya kuwa iwapo CCM na vyama hivyo watafanya kosa la kuingiza udini katika siasa za nchi, watakuwa wanajichimbia kaburi refu, maana matokeo ya kampeni chafu za viwango hivyo ni mabaya kwa wote, na yanaweza kugeuka silaha kwa wasio madarakani.

  Wameonya pia kuwa iwapo masuala ya kifamilia yatageuzwa silaha ya kisiasa kwa wagombea, yanaweza kujitokeza masuala mazito dhidi ya walio madarakani, ambao watakuwa wamempatia Dk. Slaa kombora la nyongeza la 21.

  Tayari, baadhi ya makada wa CCM na watumishi wa Ikulu wameshaanza kutumia vyombo vya habari kusambaza uvumi na propaganda dhidi ya Dk. Slaa ili kumchonganisha na wanachama na viongozi wenzake.

  Katika hatua nyingine, mwasisi wa mageuzi nchini na mwanasheria maarufu, aliyejiunga na CHADEMA hivi karibuni, Mabere Marando, amesema ana mafaili ya viongozi wa kitaifa yenye sahihi zao, yakionyesha jinsi walivyohusika na kashfa mbalimbali za ufisadi serikalini.

  Akihutubia mamia ya wananchi kwenye Uwanja wa Mwembetogwa, mkoani Iringa na Mbeya jana, kwa nyakati tofauti kwa ajili ya kuwaomba ridhaa ya kumdhamini mgombea urais wa chama hicho, Dk. Slaa, Marando alisema ana mafaili ambayo akiyaanika hadharani yatagusa wengi, akiwamo kiongozi mkuu ambaye hakumtaja jina.

  “Kuna watu wameanza chokochoko eti kwamba uamuzi wangu wa kuingia CHADEMA ni kutaka kudhoofisha vita dhidi ya ufisadi ambayo imekuwa ukiendeshwa na chama hiki, leo (jana) napenda kuwaambia bila woga wowote kwamba pale ofisini kwangu kuna mafaili ya viongozi wa serikali, tena yakiwa na sahihi ya kiongozi mkuu (hakumtaja jina), nikiyaanika haya, hawatajaribu hata kidogo kuchokoza tena, eti mtu ukianza kupata umaarufu wanasema nimeanza… jamani nasema mimi sidanganyiki,” alisema Marando.

  Alisema kwa kipindi kirefu, amekuwa akihusishwa na taarifa kuwa yeye ni ofisa usalama, hivyo amekwenda kufanya uchunguzi CHADEMA, Marando alisema: “Kweli mimi ni afisa usalama niliyesomea maeneo mengi, yakiwamo nchini Cuba, nilifaulu vizuri na kuwa tegemeo kwa taifa, hata wakati najiandaa kuondoka kwenye kazi hii, walitaka kunizuia eti kwa kisingizio kwamba maadili hayaniruhusu.

  “Nikiwa kule sikula kiapo cha kunizuia kuingia kwenye siasa ndiyo maana nikaamua kuingia kwenye upinzani, nimeingia CHADEMA nikiwa nimedhamiria kuandika historia nyingine kwa ajili ya kuwakomboa Watanzania,” alisema Marando.

  Alisema kama chokochoko hizo zitaendelea atafumua mabomu mazito ya kesi mbalimbali ambazo ziko mezani mwake, hali ambayo itasababisha kampeni za uchaguzi wa rais, wabunge na madiwani kuchimbika.

  Akihutubia mkutano huo, Dk. Slaa aliwasihi wakazi wa Mkoa wa Iringa kuacha tabia ya kila uchaguzi kuipigia kura CCM, kwa kuwa imewageuza kuwa mtaji wao kila kukicha.

  “Nawaambia kama tulivyofanya ukombozi kwenye halmashauri nyingine, tumepeleka ukombozi mkubwa, lakini wananchi wa mkoa huu mnapaswa kubadilika kwa vile tangu mfumo wa vyama vingi umeingia nchini, hamjawahi kutoa mbunge wa upinzani,” alisema Dk. Slaa.

  Alisema amekamata barua zilizotumwa na CCM makao makuu kwenda kwa wakuu wa wilaya kote nchini, zikiwaagiza kukusanya wafanyabiashara wote kila mkoa kuhakikisha wanaichangia CCM fedha kwa ajili ya kampeni za Uchaguzi Mkuu.

  Dk. Slaa alipowasili mkoani hapa, alipokewa kwa maandamano makubwa yaliyotikisa mji wa Iringa kutokana na kupita mitaa mbalimbali kabla ya kuingia kwenye uwanja wa mkutano.

  Mara baada ya mkutano huo, Dk. Slaa akitumia ndege ya kukodi aliwasili majira ya saa 11:3 jioni kwenye Uwanja wa Ndege wa Mbeya ambako alipokewa na mamia ya wananchi, waliosababisha shughuli mbalimbali kusimama.

  Mamia ya wananchi wakiwemo watu wazima, vijana na watoto, huku wakikimbia mchakamchaka kwa umbali wa zaidi ya kilomita mbili na nusu wakiimba nyimbo za “mpisheni rais apite, kiboko ya mafisadi ametua Mbeya.” Kadiri msafara huo ulivyosonga mbele, vijana wakiwa na mabango yaliyosomeka “Dk. Slaa ulizaliwa uikomboe Tanzania, mafisadi chali, Dk. Slaa mtetezi wa wanyonge, chaguo la Watanzania, mdogo mdogo baba mpaka Ikulu.” Dk. Slaa na msafara wake leo wanatarajiwa kuwasili katika mikoa ya Ruvuma, Lindi na Mtwara kwa ajili ya kuendelea kuomba ridhaa ya udhamini wa wananchi kwa ajili ya kugombea urais.

  CCM,

  Ole wenu mcheze na hisia za watu at this point. Mnachukua kodi zetu kwa ajili ya kutununua just for your primaries. tunajua jinsi mlizofanya na video za haya masibusi zipo na akili inayotumika inajulikana.

  Kuna watu wanauchungu na hii nchi na next move kwa taarifa yenu labda mkataze mobile ofisini kwenu.

  Hatutaki machafuko ila ujangili wenu tena ukiongozwa na wale wanaojifanya wanajua kuchangia while wamevaa ngozi ya kondoo wamekwisha. Haiwezekani wao kuwa na vipande viwili eti kwa kuwa mnataka kuhalalisha vitumike ndo mtuharibu.

  Nasema tena tumechoka, na hatuna pa kukimbilia zaidi ya hapa hapa. Bora mkaanza nyie kuondoka kuliko tuwalazimishe, Ole wenu nyie vibaraka, maana mngefikiria hata vizazi nyenu msingefanya hivyo. idios.
   
 2. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #2
  Aug 4, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,604
  Likes Received: 4,730
  Trophy Points: 280
  Nyumba ndogo umeshaamka, JK akipiga chafya unaitika.
   
 3. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #3
  Aug 4, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,422
  Likes Received: 393
  Trophy Points: 180
  Duh! Hii kali...nyumba ndogo ya mkulu?
   
 4. kmp

  kmp Member

  #4
  Aug 4, 2010
  Joined: Jun 18, 2009
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi hii inayojiita luninga ya Taifa TBC mbona haituonyeshi raisi wetu ajaye Mh. Dkt. W.P. Slaa anavyoendelea na ziara ya kutafuta wadhamini wakati wanatoa mpaka dakika 15 au nusu ya habari za ndani ya nchi kuzungumzia mambo ya Chama Cha Mafisadi ( CCM ) tu!!!

  Kwa kweli mimi wananiudhi sana and it is not fair at all.

  Mkurugenzi wa TBC Bw. Tido Mhando je, bado unadiriki kusema hicho ni chombo cha Taifa wakati mnatoa habari za upande mmoja wa CCM??

  Go to the hell TBC, tumewachoka na upendeleo mnaoufanya hamuoni hata aibu! LOL!!!!!!!!

  Tido Mhando hebu rekebisha hili bwana , this is shame. Tukichukua nchi hii, walahi huna kazi tena!!!!!!
   
 5. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #5
  Aug 4, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Goo to hell TBC1 ningekuwa na babomu ningekilipua
   
 6. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #6
  Aug 4, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,163
  Likes Received: 1,251
  Trophy Points: 280
  Mafisadi waliopo ndani ya CCM wamenunua hata magazeti,maana zaidi ya TZ daima, Majira, M/Halisi na Raia Mwema, mengine yote kimya kuhusiana na suala la Slaa na mikutano yake.
   
 7. Mtu66

  Mtu66 Senior Member

  #7
  Aug 4, 2010
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 166
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kizuri kunauzika tu bila hata hayo ma TVs yao ... kwani wanaompokea airport huwa wametangaziwa na hizo TV...waandikieni ndugu zenu ....wapigieani simu ndugu zenu......SMSssss ndugu zenu.....na waambieni habari za ujuo wake ...... Dr. Slaa
   
 8. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #8
  Aug 4, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Katika kurusha makombora, tunaomba Dr. Slaa asipuuzie wala asisahau hata kidogo kutueleza atatufanyia nini Watanzania wanyonge katika kutusaidia kuboresha maisha kama tutampa ridhaa yetu kuingia Ikulu. JK alikuja na slogan yake ya 'maisha bora kwa kila Mtanzania', miaka 5 imepita hatuoni maisha yoyote bora kwa wanyonge zaidi ya kuzidi kuumia kutokana na mfumko wa bei n.k.. Twataka 'makombora' ya Dr. Slaa viende sambamba na data sera za maisha bora kwa kila Mtanzania kutoka kwake Dr. Slaa against kushindwa kwa JK kutimiza ahadi yake. Nasema hivyo kwa sababu Makamba keshaanza kudai kwamba Dr. Slaa ana agenda moja tu ya ufisadi. Twataka Dr. Slaa awe na agenda kuu mbili ya ufisadi pamoja na nyingine kuu ya Maendeleo ya kila mtu Tanzania, ili sote tugawane na tufaidi keki ya Taifa kwa uwiano unaokubalika.
   
 9. SILENT WHISPER

  SILENT WHISPER JF-Expert Member

  #9
  Aug 4, 2010
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 2,231
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  kama unatoka jimbo ambalo halijawahi kutoa mpinzani ...u r part of the problem..! wake up and say not to chama cha mafisadi.
  nani kakwambia ati chama kimekulea ..? huko ni kuwatukana wazazi wako waliokulea kwa shida...!

  mungu ametupa musa wa pili baada ya nyerere..!
   
 10. e

  ejchao7 Member

  #10
  Aug 4, 2010
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 19
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 5

  Wanatumia pesa za walipakodi na watoa jasho wa nchii hii kuendeleza uozo wao waliouzoea

  I say not at this time,

  I say not at this hour

  I say not at this moment,

  Hii television ya taifa watueleze kama nayo ni ya ccm au ??

  Wasituchanganye sasa

  Inaonekana mkuu amewapa order,

  But they won't succeed at this time

  We need change,

  We want change,

  We are tired of more than 40 years of festivals,

  We are down for business now

  And that time is now.
   
Loading...