Dk Shein azikumbusha nchi za Maziwa Mkuu

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
NCHI za Maziwa Makuu zimetakiwa kuandaa mkakati wa kutoa michango ya fedha za kuendeleza mapambano dhidi ya ukimwi ili kuendeleza mradi unaofadhiliwa na Benki ya Dunia.
Zimetakiwa kutambua wazi kwamba Benki ya dunia itamaliza ufadhili wake mwishoni mwa mwaka huu na kwamba ni jukumu la nchi husika kuanza kuchangia mradi ili kuendeleza mapambano dhidi ya ukimwi.
Akifungua mkutano wa Baraza la mawaziri wa nchi hizo jijini Dar es Salaama jana, Makamu wa Rais Dk Ali Mohamed Shein alisema ili kuhakikisha mkakati huo unaendelea, wanachama wanapaswa kuheshimu makubaliano ikiwa ni pamoja na kulipa michango yao kwa wakati.
“Naamini utimizwaji wa majukumu kwa wakati kwa serikali zetu katika kuchangia, kama ilivyoelezwa katika mkataba wetu ni changamoto inayopaswa kufanyiwa kazi ili kuhakikisha maendeleo katika mapambano dhindi ya ukimwi yanaendelezwa” alisema.
Aliwashauri washirki wa mkutano huo kubuni uwekezaji mpya wa maendeleo utakaowezesha mkakati huo kufanikisha rasilimali watu na fedha.
“Mkakati wa nchi za maziwa makuu dhidi ya ukimwi, unapaswa pia kuanzisha miradi ya maendeleo kupitia sera za maendeleo na mipango inayolenga kufanya tafiti zenye mwelekeo wa kikanda. Taarifa za tafiti hizo zisaidie mkakati wa nchi za maziwa makuu katika kupambana na ukimwi, kama mkakati wa umoja, ili kusadia rasilimali watu na fedha” alisema.
Mkakati wa maziwa makuu katika mapambano ya ukimwi (GLIA), ulianzishwa mwaka 1998 na umekuwa ukitumika kueleza matokeo ya ugonjwa wa ukimwi na masuala mengine ya kiafya ukilenga hasa wakimbizi, jamii zinazozunguka kambi za wakimbizi na watu wanaorudi kwenye makazi yao ya awali. Inatoa pia huduma za afya kwa madereva wa magari makubwa wanaovuka mipaka ya nchi zao mara kwa mara.
Makamu wa Rais aliupongeza makakti huo kwa mafanikio iliyopata tangu ulipoanzishwa na kutoa wito kwa jitihada zaidi katika kupambana dhidi ya janga hilo.
Awali, Mwenyekiti mtendaji wa tume ya kudhibiti ukimwi (Tacaids), Fatma Mrisho, alisema mkutano huo wa siku tatu, ulianza siku moja kabla ya ufunguzi kwa kufanya kikao cha kamati kuu kilichoandaa ajenda za mkutano.
 
Back
Top Bottom