Dk Shein apewe nafasi Zanzibar

kalulukalunde

JF-Expert Member
May 27, 2016
1,056
1,083
Ni hali ya kusikitisha paleinapoonekana viongozi wa kisiasa wakishiriki kuhamasisha wananchi wafanye migomo baridi visiwani kwa vile tu hawakubaliani na matokeo ya chaguzi. Namna yeyote ile ya kufanya hujuma za kiuchumi zinasababisha hali ngumu zaidi kwa wananchi wa kawaida na hususan wasio na kipato kikubwa. Haiwezekani ikawa ni busara na hekima ya mwanasiasa kutumia njia hizo ili kutimiza malengo yake.

Kwa uhalisia uliopo sasa, Dk. Mohammed Ali Shein ndiye Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. Ni uhalisia ambao, kuubadilisha kwake ni lazima uendane na njia za kisiasa zisizo za kudidimiza hali za wananchi na hata kuchochea vurugu.

Siasa inahusu mijadala endelevu na isiyokoma, na ndio maana ya siasa. Ni wakati sasa, kwa hata wenye kuwa na ndoto za kuongoza visiwa vya Zanzibar na Pemba kwa miaka ijayo, kuwa ni wenye subira na kuruhusu uwepo wa mazungumzo kuliko kuandaa mazingira ya wao wenyewe kuja kuongoza vyenye wakazi waliogawanyika na hata kubaguana kwa misingi ya kiitikadi.

Makala haya yanayapa MAZUNGUMZO nafasi ya kwanza kwa pande zenye kutofautiana ili wafikie kwenye muafaka. Itakumbukwa, kuwa baada ya matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2005 Maalim Seif Shariff Hamad alikaririwa akitamka kuwa; 'Hakuna tena mufaka wa tatu". Rais Karume naye akakaririwa akitamka; "Sitaki kusikia habari ya serikali ya mseto".

Tulipofika hapa, na kwa njia ya mazungumzo, CUF na CCM Zanzibar walifikia muafaka, na Serikali ya Mseto ikapatikana. Na mara hii tena tunaamini muafaka utafikiwa na Serikali ya Mseto itaendelea kuwepo, hakuna namna nyingine ya kuviongoza visiwa vya Zanzibar bila mseto.
Kuna umuhimu pia wa viongozi wa CCM na CUF kufahamu kuwa dunia imebadilika. Leo dunia inafuatilia kwa karibu yanayotokea kwetu kwa vile yana mahusiano na athari hata nje ya mipaka yetu.

Sura ya dunia imekuwa ikibadilika katika vipindi tofauti. Marekani, kwa sababu za kimaslahi imekuwa na historia ya kuingilia mambo ya ndani ya sio tu nchi za kiafrika, hata nchi za Marekani ya Kusini, Asia na hata Ulaya.

Katika karne hii, tukubaliane, kuwa hakuna tena masuala ya ndani ya Tanzania , Zimbabwe, Uganda au Ushelisheli. Dunia imebadilika. Yanayotokea Mji Mkongwe Unguja na Micheweni Pemba yanaihusu Idara ya Ulinzi ya Marekani, Pentagon, Shirika lake la ujasusi CIA na hata FBI. Tuiangalie dunia ya sasa kwa miwani hiyo.

Itakumbukwa baada ya Vita Kuu ya Pili, dunia ilipitia kipindi cha vita baridi . Miaka ile ya 60 dunia iligawanyika katika kambi mbili kubwa kiitikadi; zilijulikana kama Warsaw Pact na Nato Pact. Kambi ya Warsaw iliongozwa na Urusi ya zamani na ile ya NATO iliongozwa na Marekani. Kulikuwepo pia na kundi la nchi zisizofungamana na upande wowote. Tanzania ilikuwa mwanachama wa kundi hili. Hata hivyo, nyingi ya nchi hizi kimsingi zilikuwa na upande zilizoegemea kati ya makundi mawili niliyoyataja.

Tunasoma kuwa Marekani na hususan kupitia Shirika lake la ujasusi la CIA ilijiingiza kwa mara ya kwanza katika siasa za Zanzibar mara baada ya mapinduzi ya 1964 kwa lengo la kupunguza kasi ya kuenea kwa Ukomunisti. Marekani iliingiwa na hofu ya Zanzibar kama kisiwa kutumiwa na Wakomunisti. Katika Zanzibar bado kuna kumbukumbu ya historia hii kwa kuyaangalia majina kama Uwanja wa Mao Tse Tung, hospital ya V.I Lenin, shule za Fidel Castro, Patrick Lumumba na mengineyo. Yote haya yalikuwa na mwelekeo wa kambi ya Warsaw; Ukomunisti.

Mvutano wa kiitikadi kati ya Warsaw na NATO uliendelea kuwepo hadi pale ukuta wa Berlin uliopoangushwa Agosti 23, 1989. Huo ndio ulikuwa mwisho wa vita baridi ya dunia. Marekani ikabaki bila mpinzani wa kiitikadi. Kuanzia hapo upepo wa kisiasa uligeuka ghafla, wimbi la demokrasia ya vyama vingi likaanzia Ulaya Mashariki na kuikumba Afrika.

Kati ya mwaka 1990 hadi 1998 tulishuhudia kuwepo kwa ombwe la kiitikadi. Uchaguzi wa Zanzibar wa mwaka 1995 ulifanyika kukiwa na ombwe hilo la kiitikadi duniani. Miaka mitatu baadae, Agosti 7, 1998, sura ya dunia ilianza kubadilika. Ni mara ile balozi za Marekani Nairobi na Dar Es Salaam zilipolipuliwa. Septemba 11, 2001 sura ya dunia ilibadilika ghafla, pale kikundi cha kigaidi cha Alqaida kilipofanya maangamizi makubwa katika miji ya Washington na New York.

Kwa Marekani adui Ukomonisti alishafutika machoni, aliyejitokeza sasa ni adui mpya mwenye nguvu za kutisha, ugaidi wa kimataifa ukiongozwa na Al-Qaida ya Osama Bin Laden. Marekani na washirika wake wameweka bayana, kuwa wamo katika vita dhidi ya ugaidi katika kila kona ya dunia.

Hakika yanayotokea Zanzibar yanatutaka tutangulize busara na hekima nyingi. Ndani ya nyumba kunaweza kuwa na hali ya kutoelewana kati ya wanafamilia. Ni mambo ya kawaida. Lakini inapofika mahala njia za mazungumzo ya kawaida za kutatua tatizo zikashindana. Badala yake ugomvi na zogo likatokea, basi, hata majirani na wapita njia nao husogea kuangalia, jambo hilo ni la aibu.

Na tunaamini katika diplomasia kama njia ya kutatua migogoro. Profesa wa Sayansi ya Siasa, Robert Dahl alipata kuandika; "Ni wajibu wa dola kuendesha juhudi za kutafuta suluhu za migogoro ya kijamii. Siasa ni hatua za majadiliano endelevu yenye kuhakikisha migogoro inapatiwa ufumbuzi kwa njia za amani". (Theory and Methods of Political Science Uk. 211)

Tofauti za kifikra na kimitazamo ni mambo ya kawaida katika siasa. Kunahitajika majadiliano endelevu katika kupata ufumbuzi wa migogoro. Si lazima papatikane mshindi katika kila mgogoro, wakati mwingine hutengenezwa mazingira ya pande zote mbili kushinda, kila mmoja kujisikia ameshinda. Wazungu wanaita; win- win situation.

Mazungumzo baina ya CUF na CCM yaendelee kwa kushirikishwa mpatanishi kutoka nje. Katika mazingira ya sasa ya CUF na CCM kutoaminiana busara lingefanyika hilo. Dunia inatuangalia.
Mazungumzo ni vema yakatunguliwa na nia ya dhati ya kumpa nafasi Rais wa sasa, Dr. Mohammed Shein, afanye kazi yake ya kuwaongoza wa Zanzibar bila kuhujumiwa kwa makusudi. Hivyo, CCM na CUF lazima wazungumze, wapatinishwe, utafutwe muafaka wa tano, kwa maslahi ya taifa.

Kamanda makini anaelewa , kuwa kwa hali ilivyo sasa kwenye uwanja wa mapambano, kujichimbia handakini ni mkakati wa makosa. Hakuna aliyeshinda kwenye vita ya jana, hakuna atakayeshinda kwenye vita ya leo wala kesho. Bila muafaka, sote tutashindwa.

Chanzo: Raia Mwema
 
Zungumzia haki na sio unajikremua mambo ya kipuuzi .eleza chanzo cha mfarakano ni nini ? Kama hakuna haki mifarakano ndio jibu sahihi.usituzingue tushachoka kudhulumiwa .
 
Ni Alfu leila ulela,sala za tarawehe au riwaya za Bi kidude? tusubiri mwezi wa kula mchana kama inatuhusu wazanzibari. Mwezi huu wa toba!
 
Mleta Uzi Kumbuka Kwamba →→→ "WHEN INJUSTICE BECOMES LAW, REBELLION BECOMES DUTY"

Sasa Utakuwa Mtu Wa Ajabu Sana Kuzungumzia Mrejesho bila ya Source of Problem.

Jinamizi la October 25, 2015 ndio linalofanya Kazi! Kwanini Maamuzi Ya Wananchi Waliowengi yasiheshimiwe???

Wazanzibari Walifanya Maamuzi yao, CCM wakakataa Maamuzi ya Wazanzibar!
Na CCM wanaamini kuwa wao ni wengi hawawezi kuzidiwa na watu wachache (CUF),
Sasa Kama wao ni wengi! inakuaje wanashuhulishwa na Mgomo wa Watu Wachache??
Hapo ni wazi kuwa Nguvu ya Umma iliyo kubwa na Watu Wengi ndiyo iliyoingia katika kueka mgomo baridi, na ndomana Uhaba wa CCM Zanzibar ukaanza kujikuta dilemma na kulalamika.

Sasa si Dola na Mazombi Mnayo, si fanyeni tu Ubabe wenu.
 
Back
Top Bottom