Dk Shein apangua baraza la mawaziri Zanzibar

Kakke

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,883
1,482


Kwa mamlaka aliyopewa Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohammed Shein amefanya mabadiliko katika baraza lake la mawaziri ambapo Ramadhan Abdallah Shaaban amekuwa Waziri Ardhi, Maakazi, Maji na Nishati, Ali Juma Shamhuna amehamishiwa wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, Suleman Othman Nyanga amepeleka Wiraza ya Kilimo na Maliasili na Mansoor Yussuf Himid amekuwa Waziri asiye na wizara maalumu, na Abdillahi Jihad Hassan amehamishiwa wizara ya Mifugo na Uvuvi na Said Ali Mbarouk amehamishiwa wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii Michezo na pia Rais amemteuwa Sheha Mohammed Sheha kuwa mshauri wake Kisiwani Pemba
 
Hatimaye Shamuhuna Abigwa Panga kwakupewa wizara ngumu na kuekwa Dipasha kwa kuondolewa
 
Samahanini wana JF, mie kwa kweli mambo ya hawa jamaa huwa sioni uzito wake. Mwaziri wa ZnZ ndio nini?? Hiyo serikali ipo kwa gharama za nani?? Ni mzigo kwetu wadanganyika....
 
Hahahahaaa...
Andika rais wa Zanzibar bana!
Akiletwa huku bara hadh yake inabaki kuwa kama diwani wa kigamboni(tukizingatia ukubwa,idadi ya watu,miundombinu nk)
 
Jamani huyu mpemba mmwenzetu kutupangulia baraza la mawaziri je itakuwa chachu ya utendaji ndani ya wizara
 
lete habari iliyokamalika siyo umbea umbea tu


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein amefanya mabadiliko ya kuwabadilisha wizara baadhi ya Mawaziri.
Katika mabadiliko hayo, Dk. Shein amemteua Ramadhan Abdalla Shaaban kuwa Waziri wa Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati, kuchukua nafasi Ali Juma Shamuhuna.
Kabla ya mabadiliko hayo, Waziri Shaaban alikuwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali.
Waziri Shamuhuna ameteuliwa kuwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, wizara ambayo ilikuwa ikishikiliwa na Waziri Shaaban.
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyosainiwa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Dk. Abdulhamid Yahya Mzee, Dk. Shein amemteua Suleiman Othman Nyanga kuwa Waziri wa Kilimo na Maliasili kuchukua nafasi ya Mansoor Yussuf Himid ambae sasa anakuwa mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na Waziri asiyekuwa na wizara maalum.
Kabla ya mabadiliko hayo, Nyanga alikuwa mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na Waziri asiyekuwa na Wizara maalum.
Aidha Dk. Shein amembadili wizara aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo, Abdilah Jihad Hassan ambae sasa anakuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi.
Aliyekuwa Waziri wa wizara hiyo, Said Ali Mbarouk sasa anakuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo.
Katika uteuzi mwengine, Dk. Shein amemteua Sheha Mohammed Sheha kuwa mshauri wa Rais Pemba.
Uteuzi huo umeanza tarehe 2 Aprili
 
Haya mabadiliko naona yana harufu ya kero za Muungano ...

Waziri Shamuhuna alikana kushirikishwa kwenye sakata la serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuomba kuongeza mpaka wa bahari, ingawa wizara hiyo ilituma mwakilishi. Sina hakika kama mwakilishi anaweza kwenda mpaka New York kuwakilisha Wizara na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar bila Waziri kujua.

Hiyo Wizara ya Ardhi iko very sensitive kwa kuwa ndiko kuna hoja ya gesi na mafuta na sasa swala la mpaka wa huko baharini.

Mh. Mansoor amekuwa na msimamo mkali sana kwenye swala la gesi na mafuta, sasa sijui kinachoendelea huko.

Lakini bottom line ni kwamba Dr. Shein ana kazi ngumu sana na pia Maalim Seif nae ana wakati mugumu ... time will tell.
 
Our "President" with mediocre re-shuffles aka recycling! What for? Really!
 
wakati huku bara jk anaendelea kubebelea gunia la misumari kichwani, wao wazenj wanachapa kazi. I think shein ana nia thabiti ya kuleta maendeleo kwake.
Jk kalala usingizi baraza la mawaziri masela wake tu
 
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein amefanya mabadiliko ya kuwabadilisha wizara baadhi ya Mawaziri.
Katika mabadiliko hayo, Dk. Shein amemteua Ramadhan Abdalla Shaaban kuwa Waziri wa Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati, kuchukua nafasi Ali Juma Shamuhuna.
Kabla ya mabadiliko hayo, Waziri Shaaban alikuwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali.
Waziri Shamuhuna ameteuliwa kuwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, wizara ambayo ilikuwa ikishikiliwa na Waziri Shaaban.

Huyu JUMA SHAMUHUNA tuliambiwa kwamba aliridhia SMT kuongeza eneo tengefu la bahari (EEC) bila kuishirikisha SMZ. Baraza la wawakilishi likaazimia kwamba Shemuhuna AJIUZULU na kama atashindwa kufanya hivyo basi Rais Dr. Mohammed Shein amuwajibishe.

Sasa imekuwaje Shein badala ya kumuwajibisha amemuhamisha wizara ili kuu soo.

Watu wengi tulijua kwamba eti SMZ haikuhusishwa lilikuwa Changa la Macho tu kwa Wazanzibari na Shein amedhihirisha hilo. Upo hapo Mh. Jussa Ladha?!
 
Nawauliza hivi hatuwezi kuposti kitu chochote bila ya kumsema JK?Tusiguze ukumbi huu kuwa ni uwanja wa kumshambualia JK,kwa wale ambao wanaona hawaridhiki na kitu chochote ila kumshambulia JK waanzishe shambulia JK forum
 
Dr. Shein is doing fine so far atawashika adabu wanafiki wanaoweza kuuza uhuru wa wazenj kwa ajili ya madaraka
 
Kweli Pemba ni noma hadi rais ana mshauri maalum wa hadhi ya uwaziri anahusika na mambo ya kumshauri kuhusu Pemba tu....kweli Zanzibar kuna mambo.....je wajuzi wa Zanzibar hebu tufahamisheni rais ana mshauri wa hadhi ya uwaziri wa kumshauri kuhusu Unguja?
 
unajua mie nashindwa kuwaleewa baadhi yetu humu jamvini, linapokuja swala la muungano jk anapewa heshima zaidi ya obama na sifa kedekede lkn ukitoka apo tu anapewa matusi kuliko ya lusinde, hivi mnazani wazenji wapumbavu kiasi gani?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom