Dk Shein amefanya Uteuzi wa nafasi mbali mbali za Uongozi Zanzibar

LUKAZA

Senior Member
Nov 30, 2010
140
70
Dk Shein amefanya Uteuzi wa nafasi mbali mbali za Uwongozi zanzibar ili kuweza kuimarisha utendaji kazi bora zaidi

Hii ni kuzidi kufuta zana ya Malim Seifu kuwadanganya wana CUF kuwa Ban Qimun anakuja nchini tarehe 8 mwezi 11 mwaka 2016 anakuja kukabidhiwa nchi

==========

Dk. Shein amefanya uteuzi wa uongozi katikaTaasisi mbali mbli za Serikali

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dk. Ali Mohamed Shein amefanya uteuzi wa uongozi katikaTaasisi mbali mbli za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kamaifuatavyo:

1. UTEUZI WA NAIBU MAWAZIRI
Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu 47 cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt Ali Mohamed Shein amefanya uteuzi wa Naibu Mawaziri kamaifu atavyo:
i. Naibu Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais –Mheshimiwa Mihayo Juma Nhunga.
ii. Naibu Waziri wa Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto – Mheshimiwa Shadia Mohamed Suleiman.
iii. Naibu Waziriwa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Idara Maalumza SMZ – Mheshimiwa Shamata Shaame Khamis.
2. UTEUZI WA MJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI

Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu 66 cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein amemteua Dr. Sira Ubwa Mamboya kuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi.

3. UTEUZI WA WAKURUGENZI

Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu 53 cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein amefanya uteuzi wa wakurugenzi kama ifuatavyo:
i. Mkurugenzi wa Idara ya Uendeshaji na Utumishi katika Wizara ya Afya - Bwana Ramadhan Khamis Juma.
ii. Mkurugenzi wa Idara ya Mipango, Sera na Utafiti katika Wizara ya Afya - Bibi Attiye Juma Shaame.
iii. Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Uvuvi katika Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi - Bwana Zahor Kassim Mohamed El-Kharousy.
Uteuz ihuo umeanza tarehe 4 Novemba 2016.
 
Back
Top Bottom