Dk. Mwakyembe amchana live DCI Manumba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk. Mwakyembe amchana live DCI Manumba

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KIM KARDASH, Feb 24, 2012.

 1. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #1
  Feb 24, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Kama vile mtu ambaye amekerwa na namna Jeshi la Polisi, kupitia kwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba, Dk. Mwakyembe Februari 18, wiki iliyopita, alitoa taarifa kwa vyombo vya habari kujibu kile kilichoelezwa na Manumba kuhusu afya yake.

  Taarifa hiyo ya Mwakyembe ilieleza : "Napenda nisisitize mapema kabisa kuwa msimamo huo wa Jeshi la Polisi umenikera sana katika hali niliyonayo ya ugonjwa, kwanza kwa kuingilia mchakato wa matibabu yangu na uchunguzi wa kina kuhusu kiini chake unaoendelea hospitali ya Apollo nchini India ambako bado sijahitimisha matibabu yangu; pili kwa ufinyu wa uelewa unaojitokeza bayana kwenye tamko la Jeshi la Polisi unaosisitiza kuwa "sikunyweshwa sumu" wakati sumu si lazima unyweshwe ili ikudhuru, inaweza kudhuru hata kwa kugusishwa tu; na tatu kwa Jeshi la Polisi kujiingiza kwenye suala ambalo kwa takriban mwaka mzima halijawahi kuwa na dhamira ya dhati ya kulielewa au kulichunguza mbali na kulifanyia mzaha kupitia magazetini.


  "Itakumbukwa kuwa tarehe 9 Februari, 2011 nilimwandikia barua IGP Said Mwema kumtaarifu kuhusu njama za kuondoa maisha yangu na ya viongozi wengine. Kwa kutambua kuwa Jeshi la Polisi la Tanzania daima husisitiza kuletewa ushahidi kwanza ndipo lifanyekazi, nilihakikisha nimeainisha katika barua hiyo kila ushahidi nilioupata au kupewa. (Utaratibu huu wa Jeshi la Polisi kusubiri kuletewa ushahidi mezani, kama ambavyo mahakimu wanavyosubiri ushahidi mahakamani, haupo popote pale duniani (ila Tanzania tu) kwani kazi ya msingi ya Polisi si kuletewa, ni kutafuta ushahidi. Polisi wanachohitaji duniani kote ni kupata clue au tetesi tu. Hiyo inatosha kufukua ushahidi wote unaohitajika). Pamoja na kujitahidi kuanika kila aina ya ushahidi niliokuwa nao, mambo manne yalijitokeza ambayo yalionyesha wazi kuwa Polisi hawakuwa na dhamira ya dhati ya kupeleleza suala hilo:  1. Siku chache baada ya kumkabidhi IGP barua hiyo, nilitumiwa timu ya "wapelelezi" ofisini kwangu kuja kuchukua maelezo yangu ya ziada. Timu hiyo ilikuwa inaongozwa na ACP Mkumbo, afisa wa polisi ambaye wiki chache zilizokuwa zimepita alikuwa miongoni mwa askari waliotuhumiwa kupokea rushwa kwa lengo la kumbambikizia madawa ya kulevya mtoto wa Mwenyekiti wa IPP, Reginald Mengi, suala ambalo mpaka leo hii uongozi wa Polisi umeshindwa kulitolea maelezo ya kuridhisha. Kwa msingi huo, nilikuwa nimeletewa mtuhumiwa wa rushwa/ ujambazi kuendesha uchunguzi wa watuhumiwa wengine wa ujambazi! Nikatambua mara moja kuwa zoezi zima lilikuwa la mzaha, tena mzaha mkubwa!
  2. Wiki chache baada ya barua yangu kuwasilishwa kwa IGP na timu ya ACP Mkumbo "kuanza kazi", Jeshi la Polisi likachukua hatua ya kuwapongeza na kuwazawadia askari niliowatuhumu kushirikiana na majambazi! Huhitaji kuwa profesa wa falsafa kuelewa kuwa huo ulikuwa ujumbe tosha wa kunipuuza.
  3. Hivi karibuni tuhuma za askari polisi kujihusisha na vitendo vya ujambazi mkoani Morogoro zilipopamba moto na kuwagusa askari "wale wale" niliowatuhumu kwenye barua yangu, IGP alichukua hatua ya kuwahamishia mikoa mingine!
  4. Ili kunikatisha tamaa kabisa, barua yangu ya "siri" kwa IGP ikavujishwa kwa makusudi kwenye vyombo vya habari na kuchapishwa kama habari ambayo ilikebehi na kukanusha taarifa nzima niliyotoa, sijui kwa faida ya nani! Lakini huu ni mchezo wa kawaida kwa polisi kwani hivi karibuni Mhe. Waziri Samuel Sitta alipohojiwa na ofisa mwandamizi wa Jeshi la Polisi ofisini kwake, wakiwa wawili tu, taarifa ya kikao hicho ikawa kwenye moja ya magazeti ya mafisadi ikikebehi ushahidi aliotoa Sitta! The integrity of the police force leadership is on the line.

  Nimeelezea vizuri katika barua yangu kwa IGP kuwa kundi hilo la mauaji lilikuwa limeelekezwa kuniua kwa kutumia sumu, taarifa ambayo kwa karibu mwaka mzima Polisi hawakutaka kuifuatilia kwa sababu wanazozijua wenyewe. Sasa huu msukumo mpya wa Jeshi la Polisi kutaka kujua kama nilipewa sumu au la na kukurupuka kutoa tamko hata kabla ya kunichunguza nilivyo, kunihoji mimi na wasaidizi wangu ofisini na hata kuongea na mabingwa wa Kihindi wanaonifanyia uchunguzi, umetokea wapi? Si ni polisi hawahawa ambao, badala ya kushukuru, wamekuwa wakikerwa na tahadhari ambazo Waziri Sitta amekuwa akitoa ili suala hili lichunguzwe kwa kina?

  Aidha napata taabu kuamini kama DCI Manumba na wenzake waliisoma taarifa halisi ya matibabu yangu au walisoma taarifa "nyingine", na kama waliisoma taarifa hiyo wenyewe au "walisomewa"! Nasema hivyo kwa kuwa alichokisema DCI Manumba kwa wandishi wa habari hakifanani kabisa na picha iliyo kwenye taarifa halisi ya Apollo ambayo inatamka wazi kuwa kuna kitu kwenye bone marrow kinachochochea hali niliyonayo, kitu ambacho mabingwa wanahangaikia kukijua, kukidhibiti/kukiondoa huku vyombo vyetu vya dola vikipelekeshwa na mafisadi kusema bila msingi wa kisayansi wala aibu: "hakulishwa sumu", "hakulishwa sumu"!

  Nimesoma darasa moja Kitivo cha Sheria Mlimani na DCI Manumba. Baadaye IGP Mwema alikuwa mwanafunzi wangu wa sheria Mlimani. Vigogo hawa wawili wa usalama wa raia nchini hawajanitendea haki, nao wanajua. Wanajua vilevile kuwa sitakaa kimya au kumung'unya maneno come what may pale ambapo haki inakanyagwa.

  Tuendelee kuombeana afya na uhai ili tutendeane haki na vilevile tuitendee nchi yetu haki kwa kuvimalizia viporo vinavyokera vya Dowans, EPA, Kagoda n.k. kwa maslahi mapana ya Taifa letu.
   
 2. M

  Massenberg JF-Expert Member

  #2
  Feb 24, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 1,173
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Wewe nawe unaishi dunia gani? Hii habari imezagaa humu karibu wiki nzima wewe ndiyo unaileta leo?
   
 3. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #3
  Feb 24, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Muwe manasoma topic nyingine kwanza kabla hamjapost.
   
 4. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #4
  Feb 24, 2012
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Mkuu hata mimi nilifikiri kuna jipya!
   
 5. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #5
  Feb 24, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,386
  Likes Received: 22,266
  Trophy Points: 280
  Hii mbona ni mpya kabisa? Hamuoni?
   
 6. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #6
  Feb 24, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  mimi nilidhani Dr. Mwakyembe ameamua kuchana live akiwa India, kumbe mkuu Kim una recycle!
   
 7. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #7
  Feb 24, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  wanajifanyisha tu makusudi achana nao....
   
 8. Job K

  Job K JF-Expert Member

  #8
  Feb 24, 2012
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 6,876
  Likes Received: 2,823
  Trophy Points: 280
  Hakuna upya wowote hapo, hii ilishaletwa hapa siku nyingi. Tafuteni post inayosema Mwakyembe amjibu DCI.......!
   
 9. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #9
  Feb 24, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145

  There are currently 28 users browsing this thread. (8 members and 20 guests)....
   
 10. f

  fungamesa Senior Member

  #10
  Feb 24, 2012
  Joined: Feb 20, 2009
  Messages: 128
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Huyu kaamka na viroba kwa sababu habari hii imeshachuja. alikuwa wapi?
   
 11. Job K

  Job K JF-Expert Member

  #11
  Feb 24, 2012
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 6,876
  Likes Received: 2,823
  Trophy Points: 280
  Nashangaa anavyotaka kutulazimisha tuamini kuwa habari hii ni mpya! kwa kweli bangi siyo mchezo inawaharibu sana vijana!
   
 12. taffu69

  taffu69 JF-Expert Member

  #12
  Feb 24, 2012
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Nafikiri ingekuwa ni jambo la busara zaidi kama tungempa mgonjwa wetu Dr. Harrison muda mwingi wa kupumzika badala ya kuendelea kumjadili kila siku kwenye vyombo vya habari, vijiwe vyetu vya kila siku na kwingineko. Kwa kumpa muda wa kupumzika na kwa wale wenye nia njema na yeye kuendelea kumwombea ili apate kupona mapema tungekuwa tumemtendea jambo jema na la faraja zaidi kwake na familia yake kwa ujumla.
   
 13. Wambandwa

  Wambandwa JF-Expert Member

  #13
  Feb 24, 2012
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 2,240
  Likes Received: 337
  Trophy Points: 180
  KIM KARDASH, the continous abuse of 'gubeli' is dangerous to your mental health.
   
 14. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #14
  Feb 24, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145

  There are currently 51 users browsing this thread. (14 members and 37 guests)
   
 15. bucho

  bucho JF-Expert Member

  #15
  Feb 24, 2012
  Joined: Jul 13, 2010
  Messages: 4,547
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 180
  Lakini najiuliza sana ni kweli dci hajui kinachomsumbua mwakyembe ? Anaweza kweli anaweza kukurupuka tu kuongea bila kuchunguza au kuwasiliana na vyombo vingine vya usalama ikiwemo tiss ? Kuna kitu hapo katikati . Najiuliza sana.
   
 16. L

  LAT JF-Expert Member

  #16
  Feb 24, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  stereotype
   
 17. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #17
  Feb 24, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145


  There are currently 61 users browsing this thread. (14 members and 47 guests)
   
 18. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #18
  Feb 24, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Kim, kwani madaktari wako wa Mirembe wamegoma?
   
 19. M

  Makamuzi JF-Expert Member

  #19
  Feb 24, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 1,157
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  Bangi +viroba=Kim kardash
   
 20. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #20
  Feb 24, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,406
  Trophy Points: 280
  Kim kardashian usijidanganye na users wengi wanajua ni kitu kipya lkn ukiangalia hii habari haina upya,kubali tu mtu mzima taulo imedondoka chutama tu!!!
   
Loading...