Dk. Mkumbo hukujua muda wa kudai demokrasia?

Dk. Mkumbo hukujua muda wa kudai demokrasia?

Dr Mkumbo alijifungia kabatini akawa anaandika bila kufikiria baada ya kulishwa sumu kwamba viongozi wake ni watu hatari! Nimependa sana hii tafakuri. Inatueleza mengi. Hukumtaja Mzee wa TLP ambaye alipoondoka CCM kwenda NCCR na kisha TLP tuliona walivyomfuata. Hatuwezi kuanza kufikiria kubadilisha majemadari tukiwa vitani. Ukifanya hivyo mosi unaweza kumpata jemadari asiye na uzoefu, pili utapunguza kasi ya mapigano, tatu, utaweza ukasababisha msuguano, nne, unampa adui nafasi ya kukupenyezea watu wake kwa manufaa yake na tano, unapoteza muda kwa mambo yasiyo wakati wake. Asante sana kwa andiko lililotulia
 
Dkt. ni mtu muhimu sana Jimboni kwa gaidi Nchemba,jitihada zake sisi wanajimbo tunazitambua,mbali na uamuzi wa kimasilahi wa CDM.
 
Hata kama wewe sio mtaalam wa sayansi ya siasa,basi umewazidi hata hao wanaojiita wanasayansi wa siasa.Big up sana....pia mimi nilijaribu kulitazama suala hili kwa huu mtizamo lakini wengi sana walinipinga
 
Kapotea mchana huyo,abadilishe shart nje ndani ili asiendelee kupotea.
 
Binafsi nimeikubali chambuzi hii, mleta mada yuko makini sana..., ndg. Mkumbo anajua kuwa walicho kifanya yeye na mamluki wenzake sio jambo jema na halikubaliki hivo anatafuta kichaka cha kujificha na kupata huruma ya wananchi, lkn ajue kuwa wa Tanzania wa leo ni tofauti na wale wa miaka 47 iliopita...! Tunaweza kuchambua mpunga na mchele, ameidhalilisha sana ( u-Dr.) Mpaka naichukia kiwango hicho cha elimu, poor Dr.
 
Mh ! kweli mtoa hoja nami nikupe big up kwani upembuzi wako umetulia.Ni elimu ya kutosha kwa dr wetu wa vitabuni na wengine wenye mawazo na fikra kama zake.Si wakati muafaka kuibua hoja na kuweka mikakati ya kudai demokrasia ndani ya cdm.wanahitaji kujiimarisha,ili kasi na nguvu waliyonayo isidhofike.hakuna jingine hapo zaidi ya usaliti ili kudhoofisha chama pia tamaa ya madaraka basi.wanadhani kuwa dr.au kuwa na shahada ni kigezo pekee cha kuwa kiongozi bora au shupavu? Asidhalilishe taaluma yake.mwisho ,nimuunge mkono mwanajf aliyesema mtoa hoja ni prof.katika sayansi ya siasa na jamii pia.
 
Back
Top Bottom