Dk. Mkumbo hukujua muda wa kudai demokrasia?

sulphadoxine

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Posts
2,257
Reaction score
649
ASICHOKIJUA Dk. Kitila Mkumbo kuhusu vyama vya siasa ni kwamba; chama tawala mara nyingi hubebwa na ukubwa wa jina na rasilimali zake, lakini vyama vya upinzani (ambavyo ni vya kiharakati), hutegemea sana ukubwa au umaarufu wa majina ya viongozi wake waasisi na wenye mvuto mkubwa kwa wananchi!

Hivi ndivyo navyoweza kuanza kujibu Makala ya Dk Kitila Mkumbo aliyoiandika kwenye gazeti moja linalomilikiwa na serikali, yenye kichwa cha habari kilichosomeka; “Sumu ya Chadema ni ulevi wa umaarufu” ambapo pamoja na mambo mengine, amevishutumu vyama vyote vya kisiasa nchini kwa kukosa demokrasia.

Aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Taifa ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Chadema Dk. Kitila Mkumbo, kwenye Makala yake hiyo amesema kuwa anatoa changamoto kwa watafiti wa sayansi ya siasa, kulifanyia utafiti jambo hilo na kuliweka bayana kwa faida ya vizazi vyote.

Mimi siyo mtaalamu wa sayansi ya siasa, lakini napenda tu kumjibu Kitila kuwa alichokuwa amejaribu kukifanya yeye na kundi lake ndani ya Chadema hata kusababisha kufukuzwa kwake, ni matokeo ya kutokujua ni wapi na wakati gani hasa demokrasia hupaswa kutumika ndani ya chama chochote cha kisiasa.

Nasema hivyo kwa sababu siyo wakati wote demokrasia hutumika ndani ya chama cha siasa, bali hilo huja tu pale chama kinapokuwa kimeshika dola na kujiimarisha kwa rasilimali watu na pesa; hapo ndipo demokrasia hutumika baada ya chama kuwa maarufu kuliko umaarufu wa waasisi ama viongozi wake wa juu.

Mara nyingi vyama vya siasa vya upinzani kabla havijapata ridhaa ya umma kuongoza nchi, huesabiwa kama vipo kwenye harakati za kusaka uhuru, hivyo basi katika mpito huo demokrasia siyo muhimu sana, bali kinachotazamwa ni umahiri na umaarufu wa viongozi wake wa juu, katika kutetea maslahi ya wanyonge.

Vyama vingi vya kiharakati, kwa maana ya vyama vinavyopambana kushika dola, uimara na umaarufu wake mara nyingi hujengwa kupitia Imani waliyonayo watu kwa umahiri na umashuhuri wa kiongozi au muasisi wa chama hicho, wala kamwe siyo kwa sababu ya kudumisha demokrasia wala mapenzi na Imani ya wananchi kwa chama hicho!

Chama ni watu; hivyo basi watu pia humfuata mtu ndani ya chama chochote cha kisiasa anayeonekana kuwa mahiri na shupavu katika kutetea haki zao wanazoona zinabinywa na chama tawala, kwani kwao mtu kama huyo huonekana kuwa na thamani kubwa sana kuliko ukubwa wala umaarufu wa jina la chama chake!

Kinachotazamwa hapo siyo umaarufu wa jina la chama bali ni umaarufu wa jina ama majina ya viongozi wa juu wa chama, ambao wamekuwa watetezi wa haki za wanyonge kiasi cha watu kujenga Imani kubwa kwao, kuliko Imani waliyonayo kwa chama kama chama!

Mfano; wabunge kama vile John Shibuda, Maswa Magharibi (Chadema), John Cheyo, Bariadi Mashariki (UDP), Edward Lowassa, Monduli (CCM), aliyekuwa mbunge wa Karatu (Chadema), Dk. Wilbroad Slaa n.k, hao panga pangua katika majimbo yao wana majina makubwa kuliko vyama vyao!

Leo hii watu wenye majina maarufu kama hayo, jamii inatambua mchango wao mkubwa katika kutetea haki za wanyonge hasa kwenye majimbo yao, kiasi kwamba hata wakiamua kubadili vyama, bado majina yao huendelea kubeba umaarufu mkubwa na mvuto zaidi kuliko majina ya vyama vyao!

Kumbuka hata Nelson Mandela, wananchi wa Afrika ya Kusini hawakutaka kamwe kusikia habari za demokrasia ndani ya chama cha African National Congless (ANC), walidiriki hata kumpa nafasi hiyo mkewe wakati Mandela akiwa kifungoni, bila kujali majina mengine ndani ya chama hicho.

Vivyo hivyo kwa Nyerere na TANU yake, Kaunda na UNIP, Jomo Kenyatta na KANU, Samora na FRELIMO, Mugabe na ZANU-PF n.k, wote hao wamekuwa waasisi na viongozi wa vyama vyao kwa muda mrefu, kabla na hata baada ya uhuru, kwa sababu majina yao yalikuwa maarufu kuliko yale ya vyama vyao.

Hii ndiyo kusema kuwa; vyama hivyo havikuiona nafasi ya demokrasia ndani ya uongozi wao kwa sababu siyo kwamba viongozi hao walikuwa maimla (madikteta), la, bali wananchi walikuwa na Imani kubwa ya kupata ukombozi kupitia umaarufu wa majina ya viongozi wao.

Kingine ni misimamo yao thabiti dhidi ya serikali kandamizi na sababu nyingine kuu na ya msingi ya kutokuruhusu demokrasia wakati vyama vya upinzani vikiwa kwenye harakati za kusaka ukombozi, ni kuhofia kupandikiziwa viongozi mamluki, dhahifu na wasio na uchungu na malengo ya chama ya kuwaletea wananchi ukombozi kamili!

Lakini utaratibu huo unaweza kubadilika pale tu chama kinapokuwa kimeshika dola na kujiimarisha kwa wingi wa rasilimali watu na fedha; ambapo katika mazingira kama hayo umaarufu wa chama unakuwa hautegemei tena kubebwa na umaarufu wowote wa jina la mwanachama.

Hapo ndipo demokrasia huanza kuchukua nafasi yake, ndani ya chama kwa mwanachama yoyote yule mwenye sifa na vigezo, kuweza kuruhusiwa kugombea nafasi za juu za uongozi wa chama, kwa sababu kimeshika dola na kina wingi wa rasilimali watu na pesa, kuanzia ngazi ya shina hadi taifa.

Ndiyo maana nasema kuwa Dk. Mkumbo na wenzake hawakujua ni majira na wakati gani hasa demokrasia inapaswa kutumika ndani ya chama; vyama vya upinzani havijashika dola yeye anataka viwe na demokrasia! Ana ajenda gani ya siri? Demokrasia hiyo ni kwa faida ya nani? Wananchi ama chama tawala!

Dk. Mkumbo anapaswa kusubiri kwanza vyama hivyo vikamate dola ndipo adai demokrasi; lakini kwa sasa asishangae kuitwa muhaini kama akina Kambona na wenzake walivyoitwa enzi hizo, kabla TANU ya Nyerere ilipokuwa bado haijakamilisha vizuri malengo yake kamili ya ukombozi wa Mtanzania.

Ndiyo maana binafsi sishangai kumuona Prof. Ibrahimu Lipumba na Maalim Seif Sharrif wakiishikilia CUF kwa muda mrefu, Slaa na Mbowe wakiikamata Chadema, Cheyo na Mbatia wakiwa na vyama vyao vya UDP na NCCR-Mageuzi, kwa sababu natambua bado wapo kwenye harakati za kusaka ukombozi.

Sikatai; viongozi wa vyama vya upinzani wanaweza kubadilishwa, lakini siyo lazima iwe kwa kutegemea mfumo wa demokrasia bali hata kwa kutegemea busara, Imani, malengo na umaarufu wa majina ya hao wanaotaka kuwa warithi, yanavyokubalika kwa wanachama na wananchi wengi bila kuathiri mwenendo wa chama.

Hivyo basi hatuwezi kudai demokrasia ndani ya vyama vya upinzani kama Kitila na wenzake wanavyodai; bali sisi tunaidai na kuihimiza zaidi demokrasia hiyo ndani ya chama tawala; huku pia tukisubiri vyama vya upinzani navyo vikamate dola ndipo tuanze kuvidai demokrasia ndani ya uongozi wao! (Ni mtazamo tu, siyo lazima uamini hivyo!)
 
Dr Kitila anajua ukweli tatizo anataka kuonekana yuko sahihi na pengine anadhani hatumuelewi vizuri hivyo anajaribu kutuelewesha kwa namna inayozidi kutuongezea maswali sisi wengine maana anazidi kuja kwenye rangi ambayo si ile tuliyokuwa tunaitegemea kutoka kwake.

Bora angekaa kimya abaki na benefit of doubt kuliko hizi kauli zake za sasa.Kutaka kufananisha tuhuma za Zitto na Lowasa kuwa hazina ushahidi bali udhaifu tu wa vyama vyao ni aibu kwakweli kwa mwanamapinduzi kama yeye.
 
ASICHOKIJUA Dk. Kitila Mkumbo kuhusu vyama vya siasa ni kwamba; chama tawala mara nyingi hubebwa na ukubwa wa jina na rasilimali zake, lakini vyama vya upinzani (ambavyo ni vya kiharakati), hutegemea sana ukubwa au umaarufu wa majina ya viongozi wake waasisi na wenye mvuto mkubwa kwa wananchi!

Hivi ndivyo navyoweza kuanza kujibu Makala ya Dk Kitila Mkumbo aliyoiandika kwenye gazeti moja linalomilikiwa na serikali, yenye kichwa cha habari kilichosomeka; "Sumu ya Chadema ni ulevi wa umaarufu" ambapo pamoja na mambo mengine, amevishutumu vyama vyote vya kisiasa nchini kwa kukosa demokrasia.

Aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Taifa ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Chadema Dk. Kitila Mkumbo, kwenye Makala yake hiyo amesema kuwa anatoa changamoto kwa watafiti wa sayansi ya siasa, kulifanyia utafiti jambo hilo na kuliweka bayana kwa faida ya vizazi vyote.

Mimi siyo mtaalamu wa sayansi ya siasa, lakini napenda tu kumjibu Kitila kuwa alichokuwa amejaribu kukifanya yeye na kundi lake ndani ya Chadema hata kusababisha kufukuzwa kwake, ni matokeo ya kutokujua ni wapi na wakati gani hasa demokrasia hupaswa kutumika ndani ya chama chochote cha kisiasa.

Nasema hivyo kwa sababu siyo wakati wote demokrasia hutumika ndani ya chama cha siasa, bali hilo huja tu pale chama kinapokuwa kimeshika dola na kujiimarisha kwa rasilimali watu na pesa; hapo ndipo demokrasia hutumika baada ya chama kuwa maarufu kuliko umaarufu wa waasisi ama viongozi wake wa juu.

Mara nyingi vyama vya siasa vya upinzani kabla havijapata ridhaa ya umma kuongoza nchi, huesabiwa kama vipo kwenye harakati za kusaka uhuru, hivyo basi katika mpito huo demokrasia siyo muhimu sana, bali kinachotazamwa ni umahiri na umaarufu wa viongozi wake wa juu, katika kutetea maslahi ya wanyonge.

Vyama vingi vya kiharakati, kwa maana ya vyama vinavyopambana kushika dola, uimara na umaarufu wake mara nyingi hujengwa kupitia Imani waliyonayo watu kwa umahiri na umashuhuri wa kiongozi au muasisi wa chama hicho, wala kamwe siyo kwa sababu ya kudumisha demokrasia wala mapenzi na Imani ya wananchi kwa chama hicho!

Chama ni watu; hivyo basi watu pia humfuata mtu ndani ya chama chochote cha kisiasa anayeonekana kuwa mahiri na shupavu katika kutetea haki zao wanazoona zinabinywa na chama tawala, kwani kwao mtu kama huyo huonekana kuwa na thamani kubwa sana kuliko ukubwa wala umaarufu wa jina la chama chake!

Kinachotazamwa hapo siyo umaarufu wa jina la chama bali ni umaarufu wa jina ama majina ya viongozi wa juu wa chama, ambao wamekuwa watetezi wa haki za wanyonge kiasi cha watu kujenga Imani kubwa kwao, kuliko Imani waliyonayo kwa chama kama chama!

Mfano; wabunge kama vile John Shibuda, Maswa Magharibi (Chadema), John Cheyo, Bariadi Mashariki (UDP), Edward Lowassa, Monduli (CCM), aliyekuwa mbunge wa Karatu (Chadema), Dk. Wilbroad Slaa n.k, hao panga pangua katika majimbo yao wana majina makubwa kuliko vyama vyao!

Leo hii watu wenye majina maarufu kama hayo, jamii inatambua mchango wao mkubwa katika kutetea haki za wanyonge hasa kwenye majimbo yao, kiasi kwamba hata wakiamua kubadili vyama, bado majina yao huendelea kubeba umaarufu mkubwa na mvuto zaidi kuliko majina ya vyama vyao!

Kumbuka hata Nelson Mandela, wananchi wa Afrika ya Kusini hawakutaka kamwe kusikia habari za demokrasia ndani ya chama cha African National Congless (ANC), walidiriki hata kumpa nafasi hiyo mkewe wakati Mandela akiwa kifungoni, bila kujali majina mengine ndani ya chama hicho.

Vivyo hivyo kwa Nyerere na TANU yake, Kaunda na UNIP, Jomo Kenyatta na KANU, Samora na FRELIMO, Mugabe na ZANU-PF n.k, wote hao wamekuwa waasisi na viongozi wa vyama vyao kwa muda mrefu, kabla na hata baada ya uhuru, kwa sababu majina yao yalikuwa maarufu kuliko yale ya vyama vyao.

Hii ndiyo kusema kuwa; vyama hivyo havikuiona nafasi ya demokrasia ndani ya uongozi wao kwa sababu siyo kwamba viongozi hao walikuwa maimla (madikteta), la, bali wananchi walikuwa na Imani kubwa ya kupata ukombozi kupitia umaarufu wa majina ya viongozi wao.

Kingine ni misimamo yao thabiti dhidi ya serikali kandamizi na sababu nyingine kuu na ya msingi ya kutokuruhusu demokrasia wakati vyama vya upinzani vikiwa kwenye harakati za kusaka ukombozi, ni kuhofia kupandikiziwa viongozi mamluki, dhahifu na wasio na uchungu na malengo ya chama ya kuwaletea wananchi ukombozi kamili!

Lakini utaratibu huo unaweza kubadilika pale tu chama kinapokuwa kimeshika dola na kujiimarisha kwa wingi wa rasilimali watu na fedha; ambapo katika mazingira kama hayo umaarufu wa chama unakuwa hautegemei tena kubebwa na umaarufu wowote wa jina la mwanachama.

Hapo ndipo demokrasia huanza kuchukua nafasi yake, ndani ya chama kwa mwanachama yoyote yule mwenye sifa na vigezo, kuweza kuruhusiwa kugombea nafasi za juu za uongozi wa chama, kwa sababu kimeshika dola na kina wingi wa rasilimali watu na pesa, kuanzia ngazi ya shina hadi taifa.

Ndiyo maana nasema kuwa Dk. Mkumbo na wenzake hawakujua ni majira na wakati gani hasa demokrasia inapaswa kutumika ndani ya chama; vyama vya upinzani havijashika dola yeye anataka viwe na demokrasia! Ana ajenda gani ya siri? Demokrasia hiyo ni kwa faida ya nani? Wananchi ama chama tawala!

Dk. Mkumbo anapaswa kusubiri kwanza vyama hivyo vikamate dola ndipo adai demokrasi; lakini kwa sasa asishangae kuitwa muhaini kama akina Kambona na wenzake walivyoitwa enzi hizo, kabla TANU ya Nyerere ilipokuwa bado haijakamilisha vizuri malengo yake kamili ya ukombozi wa Mtanzania.

Ndiyo maana binafsi sishangai kumuona Prof. Ibrahimu Lipumba na Maalim Seif Sharrif wakiishikilia CUF kwa muda mrefu, Slaa na Mbowe wakiikamata Chadema, Cheyo na Mbatia wakiwa na vyama vyao vya UDP na NCCR-Mageuzi, kwa sababu natambua bado wapo kwenye harakati za kusaka ukombozi.

Sikatai; viongozi wa vyama vya upinzani wanaweza kubadilishwa, lakini siyo lazima iwe kwa kutegemea mfumo wa demokrasia bali hata kwa kutegemea busara, Imani, malengo na umaarufu wa majina ya hao wanaotaka kuwa warithi, yanavyokubalika kwa wanachama na wananchi wengi bila kuathiri mwenendo wa chama.

Hivyo basi hatuwezi kudai demokrasia ndani ya vyama vya upinzani kama Kitila na wenzake wanavyodai; bali sisi tunaidai na kuihimiza zaidi demokrasia hiyo ndani ya chama tawala; huku pia tukisubiri vyama vya upinzani navyo vikamate dola ndipo tuanze kuvidai demokrasia ndani ya uongozi wao! (Ni mtazamo tu, siyo lazima uamini hivyo!)

Mkuu ni uchambuzi mzuri na ninaomba kawatumie hata hao wakina Dr Kitila na ZZK ili wasome! Tunashukuru sana
 
naongezea mkuu... Dr. Slaa alipogombea urais kupitia cdm nayo umaarufu wa chama iliongezeka. na cdm wakileta mtu mwingine nahisi hawatafanya vizuri vile wakimwancha Dr.
 
Dk. Mkumbo anapaswa kusubiri kwanza vyama hivyo vikamate dola ndipo adai demokrasi; lakini kwa sasa asishangae kuitwa muhaini kama akina Kambona na wenzake walivyoitwa enzi hizo, kabla TANU ya Nyerere ilipokuwa bado haijakamilisha vizuri malengo yake kamili ya ukombozi wa Mtanzania.!)

Ni kweli Huwezi kubadilisha rubani wakati ndege ndiyo ipo kwenye run-way tayari kwa kuruka.

Enzi hizo wale wote waliopinga TANU au kutofautiana na fikra sahihi za mwenyekiti wa chama cha TANU mnajua kilichowakuta.

Na walienda mbali zaidi kwa kuweka salam za chama cha TANU zikisema "Zidumu fikra sahihi za mwenyekiti wa TANU --- wananchi - Zidumuuuuu!!! hapa ina maana yeyote atakayebainika anakwenda tofauti ya fikra hizi aliitwa MHAINI na si msaliti.

Demokrasia ina muda muafaka wake na mipaka yake!! iwe ndani ya ndoa au hata kwenye vyama vya siasa.

Mchambuzi upo makini.
 
hivi huyo mfata mkumbo bado anabwata tu,nilishamsahau.
 
Mleta uzi ni mmoja wa wasomi hakika.Wewe umekuwa tofauti na wengi wanaojiita wasomi ingawa naamini Kitila na wenzie walikuwa wanalijua hili vizuri ila kutokana na nia ovu waliyokuwa nayo,wakachagua silaha ya kisomi ili kuwarubuni waliowarubuni waamini vita yao ilikuwa ya haki na kumbe lengo lao lilikuwa tofauti sana na wanachokisema mchana.Kosa kubwa pia la akina Kitila,ni kudhani wanachadema wengi ni vilaza na hivyo ni rahisi kuwapumbaza kwa mikakati yao ya hila ili hatimaye wawaunge mkono.Nakupa like kwa uchambuzi makini wa kisomi mkuu

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
DR MKUMBO tatizo lake ni kufikiri ana akili sana na anajua mambo kuliko hata wale waliomfikisha hapo alipo leo, angekuwa ameyaandika haya wakati akiwa bado ni mkuu wa DUCE au bado ana madaraka ndani ya chama ningemuelewa kwamba yupo makini zaidi lakini anachokifanya sasa ni yale mambo yetu ya SIZITAKI MBICHI HIZI, pole sana dr wangu
 
Mzee wewe mbaya tanatakiwa mfuta mkumbo anyang'anywe huo uDr. tukupe wewe amepewa lift anataka na kupiga honi inaonyesha jinsi gani Elimu tanzania hakuna mtu, kama Dr. anatakakuendelea kutetea ujinga wao wa kutaka kuvuruga chama ambacho watanzania wanakitegemea
Naomba amtaje huo MM1 ndio tutajua kuwa mpango wake ulikuwa ni wa ukweli na manufaa kwa chama, kama anamikakati mizuri angeanza kwa kuchukua jimbo harafu aje na hiyo mikakati
Mara kwenye hoja zake anasema CHADEMA kitakufa kama NCCR kilivyokufa kwa kuwa kimewaondoa watu makini ,Toleo lililofuata anawahimiza watanzania kukiacha chama na kujiunga na kingine inaonyesha jinsi gani alikuwa kazi ambayo hajaimaliza ya kukiua chama unapoteza muda bure watanzania wako makini sana
Kajiunge na Mafisadi huwezi kudanganya
 
Kitila mkumbo ameshapotezwa na mwiguru kwa ushirika wa zitto atulie duce afundishe arambe chaki kama kawaida yake jimbo la mwiguru tutampa mwengine

Yupo dada mmoja jembe sana hata gaidi mwegulu anamtambua,tutampa jimbo asubuhi na mapema huyu masalia Kitila Mkumbo aendelelee na yuda wake...
 
Last edited by a moderator:
Hoja kama hizi ndizo ambazio zinapaswa ziwekwe humu JF. Hongera sana kwa uchambuzi makini ambao nadhani hata MM2 atausoma pamoja na MM1 na MM3 wajue CDM ni watu wa kufanya maamuzi magumu hata kama wao wanayaita eti maamuzi magumu lakini ya hovyo. Kwa taarifa yenu nyie MM's kwisha habari yenu ndio mmepotea jumla kwenye siasa. Tunasubiri tuone MM1 akifanya ziara na chopa nchi nzima eti kujisafisha.

Back
Top Bottom