Elias Msuya
Platinum Member
- Dec 23, 2011
- 260
- 998
Dk Melikisedeki Kaijage, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) aliyekuwa akishikiliwa na Jeshi la polisi mkoani Dodoma kwa madai ya kuhamasisha maandamano ya Julai 7, 2026, sasa amebadilishiwa shitaka na kuwa la ugaidi na hivyo kunyimwa dhamana.
Awali, Jumanne Julai 21, Dk Kaijage alipewa dhamana na Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma, baada ya kushikiliwa katika kituo cha Polisi Chang’ombe jijini humo tangu Julai 8, 2026, lakini kabla hajaachiliwa, akapewa shitaka hilo.
Soma pia: Mhadhiri UDOM akamatwa kisa Maandamano ya Sabasaba
Akizungumzia suala hilo, Mwenyekiti wa Chama cha Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOMASA), Dk Gerald Shija amesema walibaini mabadiliko hayo wakati wanashughulikia dhamana.
“Mahakama ilitoa uamuzi kwamba atoke ndani, lakini wakati tunashughulikia dhamana, tukaambiwa amehamishiwa Gereza la Isanga,” amesema Dk Shija.
Amesema Dk Kaijage anatarajiwa kuletwa Mahakamani Agosti 5, 2026.
“Sijajua watampeleka mahakama gani, kwa sababu wamefungua kesi Mahakama ya Mwanzo ambayo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za ugaidi,” amesema.