Dk. Magufuli msituadhibu

Dk. Magufuli msituadhibu

Magufuli hana shida tatizo mfumo aliopo

nayeye anayo yakwake ambayo ni matokeo ya mfumo huo unao usema. ..ndani ya ccm ndugu usitegemee kupata msafi, ona sasa mzee warioba kesha tekwa. ..
 
Duuu sasa mjomba Magu atashughulikia mchwa siinamana yeye mwenyewe pia atajishughulikia! na swahiba ?hmmmm hapa ndio anazidi kuharibu bora angeendelea kunadi hayo marudio ya sera kuliko porojo hizi
 
*Asema kitanda chenye kunguni hakichomwi moto *Ataka wananchi waichague CCM, aahidi kushughulikia ‘mchwa’

Bakari Kimwanga na Raphael Okello, Bunda
MGOMBEA urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli amewaangukia wananchi na kuwaomba wasikiadhibu chama chake katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi ujao.
Mgombea huyo amewaomba wananchi kuichagua CCM na kuahidi kuwashughulikia watu ambao amewaita kuwa ni mchwa, endapo watampa ridhaa.
Akihutubia mamia ya wananchi wa mji wa Bunda mkoani Mara jana, Dk. Magufuli alisema amejipanga vizuri kuwateketeza mchwa hao mara tu baada ya kuingia madarakani.
“Nawaoamba wananchi msiiadhibu CCM, kwa kuwa nimejipanga kuwashughulikia mchwa serikalini.
“Nawaomba wana Bunda msiipe CCM adhabu…kama ambavyo huwezi kuchoma kitanda kinachoingiliwa na kunguni, badala yake utachoma kunguni, acheni tuwachome kunguni walioko serikalini,” alisema Magufuli.
Kuhusu suala la kuwapatia wananchi wa Bunda maji, Dk. Magufuli alisema.
“Niwaahidi wanabunda, mtapata maji ndani ya miezi mitatu tangu kuunda baraza langu la mawaziri… kama waziri wa maji atashindwa kutekeleza ahadi hii, waziri huyo atageuka kuwa maji,” alisema huku akishangiliwa na mamia ya wananchi.
Alisema kila sehemu ambayo amekuwa akipita, amekuwa na kazi ya kuwaombea msamaha wagombea ubunge na udiwani na kuwasihi wananchi wawachague ili kama akiingia madarakani wasaidie kuleta maendeleo.
AMANI
Katika hatua nyingine Dk. Magufuli amepuuza hoja za baadhi ya watu wanaodai ametoa kauli za vitisho kwa wananchi kwa kuhusisha uchaguzi na vurugu za nchi ya Libya.
Akiwa katika Wilaya za Butiama, Bunda na Serengeti, kwa nyakati tofauti, Dk. Magufuli, alisema kamwe hataacha kuzungumzia amani japo kuna watu wanachukizwa na kauli yake.
Alisema ataendelea kuhubiri amani ya nchi, kwani asipofanya hivyo ni bora asichaguliwe kuwa rais wa awamu ya tano.
“Nimeanzia Butiama kutokana na historia ya amani ya nchi hii. Najua wapo watu eti wanasema nisihubiri amani ya nchi…nasema nitaendelea kuisemea wakati wote.
“Iwe usiku, mchana na hata wakati wote nitazungumzia amani, nisipohubiri amani basi sisitahili kuwa rais.
“…leo Mama Maria Nyerere yupo nchini Namibia anapokea tuzo ya amani kwa sababu ya amani ya nchi yetu kutokana na misingi imara iliyowekwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere,” alisema.
Kauli hiyo imekuja siku moja baada ya Kituo cha Haki za Binadamu na Msaada wa Kisheria (LHRC) pamoja na wasomi mbalimbali, kumtaka mgombea huyo kuacha kutumia mifano ya nchi za Libya na Misri katika kampeni zake.
Itakumbukwa katika nchi hizo, machafuko yalisababisha Kiongozi wa Libya, Kanali Muamar Gaddafi kung’olewa madarakani, huku nguvu ya umma nayo ikimuondoa madarakani Rais wa Misri, Hosni Mubarak.
Dk. Magufuli alisema amedhamiria kuwatumikia Watanzania kwa vitendo na atahakikisha anaunda baraza la mawaziri dogo, lakini lenye uadilifu.

JAJI WARIOBA

Naye Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Warioba, jana aliibuka kwenye kampeni za Dk. Magufuli na kuwashangaza watu wanaobeza maendeleo yaliyopatikana katika miaka 54 ya uhuru.
Jaji Warioba, alitoa kauli hiyo kwenye uwanja wa Mwenge kijijini Butiama alipopewa nafasi ya kusalimia.
Alisema umefika wakati watu wanaomtumia kama dira Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere katika kampeni zao wajitafakari zaidi.
Bila kutaja jina la mtu, Jaji Warioba alisema wakati wa mchakato wa urais ndani ya CCM kila mgombea alikwenda katika kaburi la Mwalimu Nyerere aliyezikwa eneo la Mwitongo na kuanza mikakati yake.
“Wengine katika kampeni zao wanatumia maneno ya Mwalimu kama wamechanganyikiwa. Huwezi kumtumia Mwalimu Nyerere kama dira halafu unasema CCM haijafanya kitu, aliijenga Tanzania kwenye misingi na wote waliomfuata wanapita kwenye misingi yake,” alisema Jaji Warioba.
Alisema hatua ya nchi kupoteza maadili ilitokana na uamuzi wa baadhi ya viongozi kuwa na uhusiano na matajiri.

Magufuli nadhani anaiogopa na kuiota gharika ya Lowasa maana alianza kulipata joto lake tangu Juni 2015.

image.jpg
 
Kitendo cha Jaji Mheshimika ambaye alipigwa na magamba kwa ajili ya katiba mpya na kitendo cha kupigia debe wachakachuaji wa katiba kurejea madarakani kweli nimeamini kuwa Mkuu wa wilaya alikuwa sahihi kuongoza vijana kumpiga na kuanzisha fujo.Sasa tunakuomba warioba utwambie vizuri kuhusu meremeta ambayo na wewe ulihusishwa,vilevile utwambie vizuri kuhusu hisa unazomiliki ndani ya airtel!!!!.
Ni aibu kwa mheshimiwa kiongozi wetu wewe na polepole kuwageuka ukawa ati kisa magufuli.Je magufuli amekuahidi kurudisha vipengele vya katiba vilivyonyofolewa!!! Mfano kuhusu watu kutorosha pesa na kuweka mabenki ya nje!!
 
Mbona analia lia? Kwani amejipangaje (In Mangi's voice)

Adhabu iko pale pale


Ndugu zangu wa kusini wanasema "Ukichimama nchale,ukikimbia nchale"
 
Kwa nini aombe msamaha kwani Waziri Mkuu ndiye Mwenyekiti wa baraza la mawaziri? Ameishawaambia kuwa mamlaka ya juu ilitoa maagizo kuwa mkataba wa Richmond usainiwe kama kawaida, acheni unafiki kwa nini hamtaki kumuwajibisha Kikwete kwa hili?

mkuu unajua nafasi ya waziri mkuu kwa mujibu wa katiba? pia kwa nini hataki kusema hiyo mamlaka ya juu ni nani? makamu wa Rais au Rais? kwa nini asimtaje hadharani kama kweli ana nia ya kweli?
 
MAGUFULI anakiri serikali ya CCM ni ya wala RUSHWA, serikali imejaa wezi...mafisi wala rushwa... mchwaaa...

SASA AMEKIRI MWENYEWE... CCM haifaiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii....


UKAWA ndio jibu sahihi.... MAGUFULI kashakubali matokeo.....

ADABU ni kuwapiga CHINI CCM... aache kuhadaa watu hapa...


Lowassa, ukawa ndio MPANGO MZIMA..
 
Anaomba radhi kwa lipi wakati ilani ilyopita wametekeleza kwa asilimia 95 na kuhusu mchwa mbona walisema ni propaganda za upinzani acha tukutane oct 25

Anashangaa kusikia kwamba twiga waliibiwa wakapandishwa kwenye ndege.Hapohapo anaomba msamaha na kuahidi kuunda mahakama ya mafisadi swali twiga watarudi.
 
Mkuu hawa jamaa wanakera sana tatizo wamejaza Ndugu, watoto mjomba, shangaz huko serikalini alaf risimoja ndio anaamua nan awe rais huyu dogo ndo aliyeharibu

Ni kweli kabisa mkuu, lakini John kasema anaenda kufuta huo mtindo, kasema mkwewe ataendelea kuwa mwalimu na watoto wake wataendelea na maisha yao, nadhani tumjaribu huyu jamaa.
 
kweli kwa maneno yakuomba wasiadhibiwe hiyo ni dalili tosha ya kuomba poooo daa!!mimi nasema kama kitanda na godoro vina kunguni hakuna namna nyingine ni kutoa nje mwagia mafuta ya taa choma moto,tafuta vingine vinginevyo utahangaika na mayai ya kunguni miaka yote.
 
mkuu unajua nafasi ya waziri mkuu kwa mujibu wa katiba? pia kwa nini hataki kusema hiyo mamlaka ya juu ni nani? makamu wa Rais au Rais? kwa nini asimtaje hadharani kama kweli ana nia ya kweli?

Unapoichagua serikali kwenye ballot box unampigia Waziri Mkuu au Rais? Na nani anaemchagua mwenzake kati ya rais na waziri mkuu? Unamjua katibu mkuu wa baraza la mawaziri? Je Waziri Mkuu anaweza kubadilisha maamuzi ya baraza la mawaziri? Ni halali pia kusema kuwa wizi wa ESCROW ulifanywa na Pinda kwa sababu alikuwa Waziri Mkuu? Mbona Pinda hamumsakami au kwa sababu yuko CCM? Mtawadanganya wajinga tu
 
Ni kweli kabisa mkuu, lakini John kasema anaenda kufuta huo mtindo, kasema mkwewe ataendelea kuwa mwalimu na watoto wake wataendelea na maisha yao, nadhani tumjaribu huyu jamaa.
tumia akili wewe,unategemea Joni kidevu aseme hatafuta,atapataje kura sasa.hoja hapa ni kwamba wameshaaìdi mara ngapi?
 
Jeki hatuna muda wa kujaribu ccm ni ile ile tu watoke warioba nako nguru 2 kero za ccm
 
Tunawakusanya sisi wenyewe hawa kunguni kwani ccm mmeshindwa kuwakusanya , 25oct tutawachoma wote kunguni hakika
 
Hahaha huyu maguful anafurahisha...sasa kwa mawazo yake mimi na akil zangu niipigie kura ccm!!!!! Mi lofa!!!!! Watapigiwa na kina diamond
 
Back
Top Bottom