Dk. Magufuli msituadhibu

Dk. Magufuli msituadhibu

happymalya

Senior Member
Joined
Sep 1, 2015
Posts
116
Reaction score
27
*Asema kitanda chenye kunguni hakichomwi moto *Ataka wananchi waichague CCM, aahidi kushughulikia ‘mchwa’

Bakari Kimwanga na Raphael Okello, Bunda
MGOMBEA urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli amewaangukia wananchi na kuwaomba wasikiadhibu chama chake katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi ujao.
Mgombea huyo amewaomba wananchi kuichagua CCM na kuahidi kuwashughulikia watu ambao amewaita kuwa ni mchwa, endapo watampa ridhaa.
Akihutubia mamia ya wananchi wa mji wa Bunda mkoani Mara jana, Dk. Magufuli alisema amejipanga vizuri kuwateketeza mchwa hao mara tu baada ya kuingia madarakani.
“Nawaoamba wananchi msiiadhibu CCM, kwa kuwa nimejipanga kuwashughulikia mchwa serikalini.
“Nawaomba wana Bunda msiipe CCM adhabu…kama ambavyo huwezi kuchoma kitanda kinachoingiliwa na kunguni, badala yake utachoma kunguni, acheni tuwachome kunguni walioko serikalini,” alisema Magufuli.
Kuhusu suala la kuwapatia wananchi wa Bunda maji, Dk. Magufuli alisema.
“Niwaahidi wanabunda, mtapata maji ndani ya miezi mitatu tangu kuunda baraza langu la mawaziri… kama waziri wa maji atashindwa kutekeleza ahadi hii, waziri huyo atageuka kuwa maji,” alisema huku akishangiliwa na mamia ya wananchi.
Alisema kila sehemu ambayo amekuwa akipita, amekuwa na kazi ya kuwaombea msamaha wagombea ubunge na udiwani na kuwasihi wananchi wawachague ili kama akiingia madarakani wasaidie kuleta maendeleo.
AMANI
Katika hatua nyingine Dk. Magufuli amepuuza hoja za baadhi ya watu wanaodai ametoa kauli za vitisho kwa wananchi kwa kuhusisha uchaguzi na vurugu za nchi ya Libya.
Akiwa katika Wilaya za Butiama, Bunda na Serengeti, kwa nyakati tofauti, Dk. Magufuli, alisema kamwe hataacha kuzungumzia amani japo kuna watu wanachukizwa na kauli yake.
Alisema ataendelea kuhubiri amani ya nchi, kwani asipofanya hivyo ni bora asichaguliwe kuwa rais wa awamu ya tano.
“Nimeanzia Butiama kutokana na historia ya amani ya nchi hii. Najua wapo watu eti wanasema nisihubiri amani ya nchi…nasema nitaendelea kuisemea wakati wote.
“Iwe usiku, mchana na hata wakati wote nitazungumzia amani, nisipohubiri amani basi sisitahili kuwa rais.
“…leo Mama Maria Nyerere yupo nchini Namibia anapokea tuzo ya amani kwa sababu ya amani ya nchi yetu kutokana na misingi imara iliyowekwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere,” alisema.
Kauli hiyo imekuja siku moja baada ya Kituo cha Haki za Binadamu na Msaada wa Kisheria (LHRC) pamoja na wasomi mbalimbali, kumtaka mgombea huyo kuacha kutumia mifano ya nchi za Libya na Misri katika kampeni zake.
Itakumbukwa katika nchi hizo, machafuko yalisababisha Kiongozi wa Libya, Kanali Muamar Gaddafi kung’olewa madarakani, huku nguvu ya umma nayo ikimuondoa madarakani Rais wa Misri, Hosni Mubarak.
Dk. Magufuli alisema amedhamiria kuwatumikia Watanzania kwa vitendo na atahakikisha anaunda baraza la mawaziri dogo, lakini lenye uadilifu.

JAJI WARIOBA

Naye Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Warioba, jana aliibuka kwenye kampeni za Dk. Magufuli na kuwashangaza watu wanaobeza maendeleo yaliyopatikana katika miaka 54 ya uhuru.
Jaji Warioba, alitoa kauli hiyo kwenye uwanja wa Mwenge kijijini Butiama alipopewa nafasi ya kusalimia.
Alisema umefika wakati watu wanaomtumia kama dira Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere katika kampeni zao wajitafakari zaidi.
Bila kutaja jina la mtu, Jaji Warioba alisema wakati wa mchakato wa urais ndani ya CCM kila mgombea alikwenda katika kaburi la Mwalimu Nyerere aliyezikwa eneo la Mwitongo na kuanza mikakati yake.
“Wengine katika kampeni zao wanatumia maneno ya Mwalimu kama wamechanganyikiwa. Huwezi kumtumia Mwalimu Nyerere kama dira halafu unasema CCM haijafanya kitu, aliijenga Tanzania kwenye misingi na wote waliomfuata wanapita kwenye misingi yake,” alisema Jaji Warioba.
Alisema hatua ya nchi kupoteza maadili ilitokana na uamuzi wa baadhi ya viongozi kuwa na uhusiano na matajiri.
 
Labda ni kujitoa ufahamu au Dr anaamua kupotosha kwa makusudi kana kwamba Watanzania wooote ni wajinga. Hamna mtu ambae atalaumu kuwa kuhubiri aman ya nchi ni kosa. Lawama anazoambiwa Magufuli ni kufananisha Sanduku la Kura na Mapinduz ya Vurugu kama yaliyotokea Libya et al! Ni mambo mawili tofauti ambayo hayafanani aslan, labda kama hao Wananchi anaowaambia hawana ufahamu. Lakini sote tunajua kilichotokea Libya ni kufanya mabadiliko kwa njia ya vurugu, lakini sote tunajua kilichotokea Nigeria,Ghana, Zambia ni kufanya mabadiliko kwa SANDUKU LA KURA, na hilo ndilo Wanaodai mabadiliko Tanzania wanataka iwe hivyo!
 
Magufuli ana wasiwasi gani? Maisha bora si yameshapatikana chini ya Kikwete?
Yeye asubiri "kuchaguliwa" tu!.
 
Duuu maskini amekata tamaa mapema hii!!! Mbona ndio kwanza tupo half time?

Anyway, adhabu ipo palepale! Asigeuke, asijipepese! Kichinjio kipo palepale! Mmetuboa sana!
 
Anaomba radhi kwa lipi wakati ilani ilyopita wametekeleza kwa asilimia 95 na kuhusu mchwa mbona walisema ni propaganda za upinzani acha tukutane oct 25

Hahahaha! Sipatii picha hasira uliyo nayo!
 
Kwa umaskini wa kutisha ulivyokithiri Tanzania mpaka Tasafu inatoa fedha kwa kaya maskini,hakuna cha kujivunia,miaka 50 ya uhuru bado huduma za maji mbovu,huduma za afya mbovu na elimu katika mazingia duni hili khali watoto wa wenye uwezo wanapata huduma bora na wanasoma academy,Mungu ninaye mwamini anapenda watu watende haki kwa wenigne.Tanzania ni nchi tajiri sana yenye bahari,mito,maziwa,madini,mbuga za wanyama,mlima kilimanjaro,bandari na ardi kubwa kwa kilimo cha umwagiliaji n.k kwa nini tuendelee kuwa maskini baada ya miaka 50 ya uhuru?.Tusishabikie chama gani kizuri tunataka mabadiliko
 
sitawaangusha kwani ss tumebebwa mbeleko??tunajiweza ni usimamizi wa ccm umetufikisha hp
 
Halafu magamba akina Lizaboni na jingalao wanajigamba humu JF, wakati mgombea wenu ameomba pooo just half time. sasa dakika tisini atazimudu?
 
Last edited by a moderator:
Swali kwa magufuli?mh:magufuli umesema hapa tulipo tumefika hapa kwa sababu ya mchwa waliopo serekalini je kwanini ulikuwa hamshauri rais kikwete awachukulie hatua hao mchwa?
Swali no mbili
Kwani wasichukuliwe hatua kipindi hiki cha kampeni ili tuzidishe imani na wewe?
 
Wafute kwanza sheria ya mtandao pili warudishe katiba ya warioba
 
MTAKOMA ukawa MMEPATA MTU KIGEUGEUUU ANAYEANGALI DINI......... MTU KAMA UYUUUU KAMWE IKULU ATAISOMA NAMBA KISHA ABANDUEE
 
Back
Top Bottom