Dk. Kafumu: Igunga wamenifuta machozi; kuna matokeo ya CCM-NEC ya TUNDURU na SIHA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk. Kafumu: Igunga wamenifuta machozi; kuna matokeo ya CCM-NEC ya TUNDURU na SIHA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Oct 4, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Oct 4, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [h=2][/h]ALHAMISI, OCTOBA 04, 2012 04:33 NA WAANDISHI WETU

  *Mhandisi Makani atupwa nje Tunduru

  ALIYEKUWA mbunge wa Igunga, Dk. Dallal Kafumu, amechaguliwa kuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), kupitia Wilaya ya Igunga. Baada ya kutangazwa mshindi kwa kupata 640 dhidi ya mpinzani wake, Aboubakar Shabani aliyepata kura 362, aliwaambia wana CCM wenzake kuwa wamemfuta machozi.

  Itakumbukwa Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, mwezi uliopita ilitengua matokeo ya ubunge wa Igunga, kwa kile ilichodai haukuwa halali, kutokana na kasoro nyingi zilizojitokeza wakati wa kampeni.

  “Nimefarijika mno, wana CCM mmenifuta machozi baada ya kupoteza ubunge mwezi uliopita, nawaomba mtulie tuchape kazi…ile rufaa yangu tayari tumekata,” alisema Dk. Kafumu.

  TUNDURU

  Habari kutoka Tunduru, zinasema Mbunge wa Tunduru Kaskazini, Mhandisi Ramo Makani, ameangushwa kwenye kinyang’anyiro cha ujumbe wa NEC.

  Makani aliangushwa na mpinzani wake, Ajili Kalolo, kwa kupata kura 889, dhidi ya kura 256.

  Pia, wajumbe walimchagua Hamisi Kaesa kuwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Tunduru.

  Nafasi ya Katibu Mwenezi, ilikwenda kwa Aindi Daruweshi, ambaye alipata kura 103 na kuwashinda wapinzani wake, Fatuma Mandingo, aliyepata kura 97 na Saidi Mchonjo aliyepata kura 6.

  Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo jana, uliofanyika katika Ukumbi wa Kiwanda cha kubangulia Korosho mjini hapa, msimamizi wa uchaguzi ambaye pia ni Katibu wa CCM Wilaya ya Songea Vijijini, Lydia Gunda, alisema Kalolo ameibuka mshindi, baada ya kupata kura 889.

  Alisema katika matokeo hayo, Kalolo aliwashinda Said Mkandu, aliyepata kura 300, Makani aliyepata kura 256 na kumfanya akimbie ukumbini kutokana na aibu na Athuman Salehe aliyepata kura 125.

  Akifafanua matokeo ya nafasi ya Mwenyekiti wa CCM Wilaya, iliyoachwa wazi na Mustafa Bora, ambaye jina lake halikurudi, alisema katika nafasi hiyo, Kaesa aliwashinda wapinzani wake, Mohamed Mleani aliyepata kura 450 na Ndawambe Mugwa, aliyepata kura 375.

  Akitangaza wajumbe, Katibu wa CCM Wilaya ya Tunduru, Ramadhan Amer, alisema jumla ya wajumbe 1,830 walihudhuria mkutano huo, kati ya 2,559 waliotakiwa kuhudhuria.

  SIHA

  Hatua ya Halmashauri Kuu ya CCM, kutangaza kurudia upya uchaguzi wa nafasi mbalimbali, ikiwemo Mjumbe wa NEC Wilaya ya Siha, imepokelewa kwa hisia tofauti na wanachama wa chama hicho, huku wengine wakihusisha na kushindwa kupitishwa kwa jina la Mbunge Aggrey Mwanri, aliyekuwa amechukua fomu ya Unec.

  Baadhi ya wanachama ambao walikuwa wamechukua fomu kwa ajili ya kuwania nafasi mbalimbali, ambao kwa sasa wamesema hawatajitokeza kuwania tena nafasi hiyo, walisema bado chama hicho hakijatoa sababu za kurudia kwa uchaguzi huo.

  Mmoja wa wanachama ambaye hakutaka kutajwa jina lake gazetini, alisema hapingani na uamuzi wa chama chake, bali anaona kuna nguvu ya chama kuendelea kuwaogopa watu fulani, ambao wana madaraka badala ya kutoa nafasi kwa wanachama wa kawaida ambao wana uwezo kushika nyadhifa hizo.

  “Wapo wanachama ambao wanahoji kama wagombea ambao majina yao yalikuwa yameshajadiliwa na kupitishwa na Kamati ya Siasa kuanzia wilayani hadi mkoani, kwa nini uchaguzi urudiwe au ni kwa sababu jina la Mbunge Aggrey Mwanry, halikupitishwa anataka kuweka watu wake,” alihoji.

  Katibu wa CCM Wilaya ya Siha, Ally Musa, alipoulizwa kuhusiana na kurudiwa uchaguzi huo, alisema hakuna sababu zozote, bali ni maamuzi ya kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama.

  Mwanzoni mwa Septamba, Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Siha, ilikataa kulipitisha jina la Mbunge wa Jimbo hilo, Aggrey Mwanry, ambaye pia ni Naibu Waziri wa TAMISEMI kugombea ujumbe wa NEC, kwa madai kuwa ana nafasi nyingi za kutumikia.

   
 2. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #2
  Oct 4, 2012
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,817
  Likes Received: 10,107
  Trophy Points: 280
  Aache unafiki wake bhana, nakasirika ssana
   
 3. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #3
  Oct 4, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  LOL... Kapewa Ulaji... Hana haja ya kwenda kufanya kazi Serikalini ??? lakini UBUNGE, No No...
   
 4. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #4
  Oct 4, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,200
  Likes Received: 3,810
  Trophy Points: 280
  Mpumbavu ulizaliwa kuwa mbunge. Wewe ni engineer hilo ndilo la msingi, huku ni uroo na ulafi na tamaa ya mali bungeni, s@#%h*&^%..........e+_^.......n$%^&......z@*%$.....i*&%@! zako
   
Loading...