Dk Hoseah ateuliwa kuingia katika 'Takukuru' ya kimataifa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk Hoseah ateuliwa kuingia katika 'Takukuru' ya kimataifa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Oct 9, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Oct 9, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,420
  Likes Received: 81,471
  Trophy Points: 280
  Date::10/9/2008
  Dk Hoseah ateuliwa kuingia katika 'Takukuru' ya kimataifa
  Na Peter Edson
  Mwananchi

  MKURUGENZI Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk. Edward Hoseah ameteuliwa kuwa mjumbe wa kamati ya utendaji ya Shirikisho la Kimataifa la Mamlaka za Kupambana na Rushwa, uteuzi ulioanza rasmi mwezi huu.

  Uteuzi huo ulifanywa kwenye mkutano mkuu wa tatu wa mwaka wa mamlaka hizo uliofanyika jijini Kiev, Ukraine kuanzi Oktoba 3 hadi 6 mwaka huu.

  Taarifa iliyotolewa jana na Afisa Uhusiano wa Takukuru, Doreen Kapwani ilisema kuwa mkutano huo, ambao ulihudhuriwa na nchi 106 wanachama wa umoja huo na asasi 13 za kimataifa ulijadili na kuweka mikakati ya kuzuia na kupambana na rushwa mahali pa kazi.

  Taarifa hiyo ilieleza kuwa mbali na mikakati hiyo ya kupambana na rushwa, suala la kuimarisha ushirikiano kati ya mamlaka hizo ilikuwa moja ya ajenda ambayo ilijadiliwa kwenye mkutano huo.

  Taarifa hiyo ilieleza kuwa baada ya kutathimini utendaji kazi wa Dk. Hoseah, mamlaka hizo kwa pamoja ziliridhia uteuzi wake wa kuwa mjumbe wa kamati ya utendaji katika shirikisho hilo.

  Shirikisho hilo liliundwa mwaka 2006 kwa lengo la kuunganisha jitihada za kuzuia na kupambana na rushwa kimataifa na makao makuu yake yapo katika mji wa Hongkong nchini China.

  Novemba mwaka jana Dk. Hoseah alichaguliwa kuwa rais wa kwanza wa Shirikisho la Mamlaka za Kupambana na Rushwa kwa Nchi za Mashariki mwa Afrika, ambazo ni Tanzania, Uganda, Kenya, Rwanda na Burundi.
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Oct 9, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,420
  Likes Received: 81,471
  Trophy Points: 280
  Huyu kazi TAKUKURU imemshinda na pia yeye mwenyewe ni fisadi. Hajafanya lolote katika kuwafungulia mafisadi mashtaka. Kamati ya Richmond ilipendekeza afukuzwe kazi, sasa kwa ajili ya usanii wa JK wa kutomfukuza kazi amepewa kazi ya kimataifa ambayo hakustahili kuipata kutokana na utendaji wake dhaifu.
   
 3. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #3
  Oct 9, 2008
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,445
  Likes Received: 7,182
  Trophy Points: 280
  Hongera sana Dr Hosea wenye wivu wajinyonge!
   
 4. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #4
  Oct 9, 2008
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Mwanakijiji,

  Akisome hii anaweza kupata presha!!! maana objective yake inaelekea kutotimia!!!
   
 5. Geeque

  Geeque JF-Expert Member

  #5
  Oct 9, 2008
  Joined: Aug 17, 2007
  Messages: 848
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Inakuwaje huyu Jambazi Fisadi Hoseah anateuliwa kwenye taasisi hii kubwa ya kuzuia rushwa?Nadhani kuna umuhimu wa wengi wetu kuiandikia hiyo taasisi kupinga uteuzi wa huyu Jambazi Fisadi.
   
 6. Kipunguni

  Kipunguni Senior Member

  #6
  Oct 9, 2008
  Joined: Jun 20, 2008
  Messages: 151
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  First Lady, mbona "unakumbatia" ufisadi?!
   
 7. M

  Masatu JF-Expert Member

  #7
  Oct 9, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hongera Dr Hosea kwa kazi nzuri wewe nabii usiekubalika nyumbani.
   
  Last edited: Oct 9, 2008
 8. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #8
  Oct 9, 2008
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,445
  Likes Received: 7,182
  Trophy Points: 280
  Anastahili hongera sana Dr Hosea wewe unadhani hii heshima alopata ni kidogo!ssa huyoooooo ameshachaguliwa wanaopinga hawana lao!la sivyo wameze sumu maana hata wakisema jamaa kachaguliwa!
   
 9. akilimtindi

  akilimtindi JF-Expert Member

  #9
  Oct 10, 2008
  Joined: Jun 30, 2008
  Messages: 423
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  First lady mbona unashabikia "ufisadi" waziwazi? Au na wewe ni fisadi? Kidogo inatia shaka maana huyu ni mwivi na hata watoto wanajua kwamba huyu Dr. Hosea bin Fisadi ni mwivi mkubwa. Tunaomba watanzania tuwe "serious" na nchi yetu sasa, sio wakati wa kushabikia mambo ya namna hii. Ni wakati wa kupambana na hawa jamaa kwa nguvu zetu zote, nawashangaa sana sana wanaompongeza huyu Dr. Uozo, kama hawashindi kula chakula cha mchana kwake basi wake zao na waume zao hawaishi bila Dr. Uozo.

  Si hilo tu, nahisi sana kwamba hizi ni mbinu zingine za CCM kutuchanganya maana yawezekana sana JK akienda huko anawapigia sana chapuo wale mafisadi ili waonekane huko nje kwamba wao ni "clean" na wanachapa kazi. Kwani hatuoni taasisi za Kimataifa zikimsifia JK kwamba amepiga bao wakati hapa tunakufa kwa hali mbaya? Hizo ni mbinu za mafisadi wakubwa (wa nje) na hivi vifisadi vidogo hapa nchini kutupoteza maboya tuone tunajikanyaga.

  Ukweli utabaki pale pale, Hosea ni Uozo na tukimpata nafasi ni kumlenga.
   
 10. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #10
  Oct 10, 2008
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  First lady aka Kuhani unaviroja!
   
 11. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #11
  Oct 10, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  Mkuu Ushi Wa Rombo,

  Heshima mbele mkuu na wewe umeshitukia duh! Jf kwa vichwa bwana!
   
 12. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #12
  Oct 10, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,420
  Likes Received: 81,471
  Trophy Points: 280
  Eti wenye wivu wajinyonge!!! Nani atamuonea wivu huyu fisadi mzembe? Kwa lipi hasa mpaka tumuonee wivu!!!??? :confused::confused::confused:
  Hongera kwa kuendelea kuwapongeza mafisadi na uzembe wakati Tanzania inaangamia na kuelekea pabaya. Hata Mengi alimpakia hivi karibuni kwa kushindwa utendaji wa kazi zake lakini wewe kwa mshangao mkubwa naona una mfagilia tu mtu ambaye hastahili kufagiliwa. Je una maoni gani kuhusu mapendekezo ya Mwakyembe na kamati yake kwamba Edward Hosea afukuzwe kazi? Mwakyembe na timu yake iliteuliwa na JK nao walikuwa wanamuonea wivu?
   
 13. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #13
  Oct 10, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,420
  Likes Received: 81,471
  Trophy Points: 280
  Kama hii ni kweli basi nimebaki mdomo wazi niko hoi bin taabani...Duh!!!!
   
 14. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #14
  Oct 10, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  $&%@#$%@*^....!
   
 15. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #15
  Oct 10, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  well.. wanaweza kumteua kuwa mwakilishi wa Tanzania kwenye jumuiya ya kuzuia Rushwa mbinguni, it won't change a thing. Haibadilishi ukweli kuwa alijaribu kuisafisha Richmond na kuitetea wakati akijua ni kampuni feki.
   
 16. P

  PauliMasao JF-Expert Member

  #16
  Oct 10, 2008
  Joined: Nov 26, 2007
  Messages: 286
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  wivu? my foot! utamwoneaje wivu mtu usiemjua au kua karibu nae? very cheap comment!
   
 17. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #17
  Oct 10, 2008
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Habari ndio Hiyoo!!!!
   
 18. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #18
  Oct 10, 2008
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Hili li Kasheshe kama vile zimepungua kidogo kichwani!
   
 19. P

  PauliMasao JF-Expert Member

  #19
  Oct 10, 2008
  Joined: Nov 26, 2007
  Messages: 286
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Eti wivu, what rubbish! First lady, utamuoneaje wivu mtu usiokuwa nae karibu? huenda akafanya vizuri huko nje ili a-prove kwamba he was the right choice. Lakini hapa kwetu kashindwa kazi and it is a fact.
   
 20. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #20
  Oct 10, 2008
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,445
  Likes Received: 7,182
  Trophy Points: 280
  Mhuuuuuum!achaaaa umbeyaaaaaaa!
   
Loading...