Dk. Bashiru Ally: Nape, Bashe wanahitaji kupikwa

Dk. Bashiru Ally: Nape, Bashe wanahitaji kupikwa

Hivi punde

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2017
Posts
2,554
Reaction score
8,606
Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bshiru Ally amesema licha ya kuwa Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye ni kiongozi mzuri na alikuwa mwenezi wa CCM lakini bado anahitaji kupikwa.

Ameyasema hayo leo Aprili 26, 2019 alipokuwa anahojiwa na Tido Mhando katika kipindi cha Gumzo la Uchaguzi kilichorushwa na Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC 2)

Akijibu swali aliloulizwa na mtangazaji Tido Mhando juu ya kuwepo kwa wabunge walio na kauli kali kama wanatia wasiwasi katika chama huku akiwatolea mfano mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe na Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye.

Akijibu swali hilo Dk Bashiru alisema
“Nape ni Mwenezi wetu, jasiri kabisa lakini anahitaji kupikwa. Nilichokuwa nasema siyo nakubali kila kitu bali mtambue kuwa chama kinawajibu wa kuwasikiliza, kuwaandaa, kuwaamini na kuwasimamia kama wanakwenda inavyotakiwa.”

“Lakini kwa jinsi hali ilivyo ni kati ya watu ambao wana mchango mkubwa na ndiyo maana nimeomba chama tujenge chuo cha kuandaa viongozi kutoka nchi sita tofauti ili tuweze kuandaa viongozi waliochipukia kwa sababu suala hili linahitaji maarifa na bila shaka tutakuwa na kina Nape na Bashe wengi,” amesema Dk Bashiru.
 
Dkt Bashiru anajichanganya sana kikauli siju hizi.. sijui kapatwa na nini?
 
No. minadhani Nape anahitaji kansela yaani ushauri hili aweze kurudi nomo, nahili ndilo tatizo lake kubwa linalomsumbua, na kikubwa hana washauri wazuri wanaoweza kumwambia nape kuwa dunia inazunguka na kujizungusha na ndiyo maana tunapata majira ya kuongoza.
 
Enzi hizo za bao la mkono Nape alijidanganya na kujiaminisha kuwa wao ndio wanaijua CCM, sasa mambo yamebadilika.
 
Sasa Nape na Bashiru nani anaehitaji kupikwa. Bashiru anafata upepo anang'ata ana puliza ili asimkorofishe amlipae.Nape ,Bashe si wanafiki wanazungumza hali halisi bila kujali tumbo.Bashiru panapomfaa ni chuoni,huku anapwaya sana.
 
[QUOTE="Hivi punde, post: 31239994, member: 426068"“
Lakini kwa jinsi hali ilivyo ni kati ya watu ambao wana mchango mkubwa na ndiyo maana nimeomba chama tujenge chuo cha kuandaa viongozi kutoka nchi sita tofauti ili tuweze kuandaa viongozi waliochipukia kwa sababu suala hili linahitaji maarifa na bila shaka tutakuwa na kina Nape na Bashe wengi,” amesema Dk Bashiru.
Kumbe Nape alikuwa bado kabisa hajapikwa kisiasa!!??
 
Dkt Bashiru anajichanganya sana kikauli siju hizi.. sijui kapatwa na nini?

Kinachomfanya ajichanganye ni kutaka kuchanganya uadilifu huku ni katibu mkuu wa chama ambacho Magufuli ni mwenyekiti na rais. Ukitaka kufanya kazi chini ya Magufuli, lazima uchague moja uadilifu uwe nje, au mnafiki muende naye.
 
Back
Top Bottom