Dk. Bashiru Ally: Nape, Bashe wanahitaji kupikwa

Dk. Bashiru Ally: Nape, Bashe wanahitaji kupikwa

Mene mene tekeli na felesi. Magufuli anatumia Kagame style, kila mtu anamuhisi ni adui, alianza CHADEMA kawamaliza, sasa kawarudia ma-CCM wenzie, hii movie ni tamu kuliko asali.

TUKAE MKAO WA KULA.
Hayo maneno yanatoa picha ya nini kinachoongelewa na uongozi wa nchi hii. Hawataki mawazo mbadala by all costs.
 
Tatizo la ccm imeingiliwa na mamluki.na hicho ndicho kiama chake.
Stay tuned
 
Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally amesema licha ya mchango mkubwa alioutoa kwa chama hicho, mbunge wa Mtama, Nape Nnauye anahitaji kupikwa, kusikilizwa, kuaminiwa na kusimamiwa.

Mbali na Nape, pia amemtaja mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe akisema ni miongoni mwa vijana waliopitia katika Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) wakati mfumo wa kuandaa viongozi ukiwa umekufa.

Dk Bashiru alikuwa akizungumza jana katika mahojiano maalumu na Tido Mhando kupitia kituo cha televisheni cha ZBC2 kuhusu Muungano uliotimiza miaka 55.
Mhadhiri huyo wa zamani wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) alizungumzia pia umuhimu wa vijana kuandaliwa kupitia mifumo ya chama.

Julai 28, 2018, akizungumza na wanachama wa CCM mjini Nzega, Dk Bashiru alisema kuwa Nape na Bashe ni watukutu wanampa wakati mgumu kutokana na udadisi wao wa mambo mbalimbali wawapo bungeni, jambo linalowafanya mawaziri wafikiri kwa kina kabla ya kutoa majibu na maamuzi.

“Nawafahamu wabunge hawa kuwa ni watukutu kwelikweli, wadadisi kwelikweli, lakini wanapishana, kwa kuwa Nape ni mdadisi na mtukutu ambaye joto lake ni kali, hivyo kazi yake ni kupoza,” alisema.
 
Dk Bashiru awataja tena Nape, Bashe
By Elias Msuya, Mwananchi emsuya@mwananchi.co.tz
pic+bashiru+1.jpg

Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally amesema licha ya mchango mkubwa alioutoa kwa chama hicho, mbunge wa Mtama, Nape Nnauye anahitaji kupikwa, kusikilizwa, kuaminiwa na kusimamiwa.
Mbali na Nape, pia amemtaja mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe akisema ni miongoni mwa vijana waliopitia katika Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) wakati mfumo wa kuandaa viongozi ukiwa umekufa.
Dk Bashiru alikuwa akizungumza jana katika mahojiano maalumu na Tido Mhando kupitia kituo cha televisheni cha ZBC2 kuhusu Muungano uliotimiza miaka 55.
Mhadhiri huyo wa zamani wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) alizungumzia pia umuhimu wa vijana kuandaliwa kupitia mifumo ya chama.
Julai 28, 2018, akizungumza na wanachama wa CCM mjini Nzega, Dk Bashiru alisema kuwa Nape na Bashe ni watukutu wanampa wakati mgumu kutokana na udadisi wao wa mambo mbalimbali wawapo bungeni, jambo linalowafanya mawaziri wafikiri kwa kina kabla ya kutoa majibu na maamuzi.
“Nawafahamu wabunge hawa kuwa ni watukutu kwelikweli, wadadisi kwelikweli, lakini wanapishana, kwa kuwa Nape ni mdadisi na mtukutu ambaye joto lake ni kali, hivyo kazi yake ni kupoza,” alisema.
Jana, Dk Bashiru alisema kati ya mambo ambayo CCM haiyafanyi kwa muda mrefu kwa sasa ni pamoja na kuwaandaa viongozi wao na alirejea historia akisema awali chama hicho kilikuwa na vyuo vya kuandaa makada na viongozi kabla ya kurejeshwa serikalini.
“Sasa Umoja wa Vijana ambao ulikuwa ndiyo tanuru la vijana, likakosa hiyo faida ya vijana kuandaliwa. Sasa kina Bashe na Nape wametokea Umoja wa Vijana kipindi ambacho maandalizi yao yalikuwa yanasuasua, kipindi ambacho umoja wa vijana ukageuzwa chombo cha wagombea kujipima umaarufu wao, hasa wagombea urais,” alisema Dk Bashiru.
Alisema, “bahati mbaya chama kikawa mbali na vijana wale na bahati mbaya vijana ni watukutu, wakati wote akili inachemka. Ndivyo Bashe na Nape walivyopatikana, walitokea Umoja wa Vijana, wakaaminiwa, wakapewa nafasi za uongozi wakaenda wakawa wabunge kwa hiyo ule udadisi wao ukaonekana una usumbufu fulani.”
Huku akimtolea mfano Nape, Dk Bashiru alisema vijana hao wanahitaji kusikilizwa, kuwaandaa, kuwaamini na kuwasimamia kama wanakwenda kinyume na taratibu, huku akisema wana mchango mkubwa katika chama hicho.
“Mtu kama Nape Nnauye amekuwa mwenezi wetu jasiri kabisa wa kutetea chama, lakini kwa kweli anahitaji kupikwa. Kwa hiyo nilipokuwa nasema siyo kwamba nilikuwa nakubaliana nao kila kitu. Kwa hali ilivyo kwa kweli ni kati ya watu kwa maoni yangu wana mchango mkubwa,” alisema Dk Bashiru.
Alisema ili kuwaandaa viongozi chama hicho kina mpango wa kujenga vyuo vya itikadi na uongozi ambavyo ni pamoja na chuo kitakachoshirikisha nchi sita na vyama vya ukombozi wa Afrika.
Kuhusu Muungano, Dk Bashiru licha ya kuunga mkono muundo wa Serikali mbili, alisema bado Taifa linatakiwa kuwa na mjadala wa Katiba kwa ajili ya kujenga mfumo wa kisiasa unaofaa.
Alisema kwa muda mrefu suala hilo limekuwa likijitokeza na aliitaja Tume ya Jaji Francis Nyalali, Kamati ya Jaji Robert Kisanga na Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyoongozwa na Jaji Joseph Warioba akisema mjadala wa Muungano bado haujahitimishwa.
“Kwa hiyo jambo hilo halijahitimishwa, lakini kwa maoni yangu mimi bado muundo wa sasa umethitisha umadhubuti wake na uhimilivu wake kwa kiwango ambacho wasiwasi uliopo unadhibitika na Watanzania wanazidi kuwa wana umoja zaidi kuliko idadi ya Serikali,” alisema Dk Bashiru.
“Kwa hiyo si tu mjadala wa Katiba ili tubadilishe aina ya Muungano, lakini mjadala wa kuhusu aina ya mfumo wa kisiasa unaotufaa na umuhimu wa uchumi unaotufaa.”
Maalim Seif na ACT Wazalendo
Kuhusu mpasuko ndani ya Chama cha Wananchi (CUF), Dk Bashiru alisema walishtushwa na kambi ya aliyekuwa katibu mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad kuhamia ACT Wazalendo.
“Ndiyo, tulishtuka zaidi kwa sababu hatukujua mabadiliko yale, baada ya CUF chama kilichokuwa na mshikamano na kilikuwa na mgogoro, na tulishtuka kwa sababu hatukuwa na utabiri,” alisema.
Hata hivyo, alisema kuimarika kwa ACT Wazalendo na vyama vingi hakuitishi CCM huku akitoa mfano wa wabunge wa vyama hivyo kuhamia chama tawala.
Akijibu swali kuhusu malalamiko ya wapinzani ya kuzuiwa kufanya mikutano ya hadhara ilhali CCM wanafanya, alisema mikutano hiyo haijakatazwa bali kilichokatazwa ni mikutano ya operesheni.
“Kwa hiyo sijafanya mikutano ya hadhara ambayo imezuiwa. Siyo yote imezuiwa, madiwani si wote kwa sababu hatuwalazimishi, wabunge wote wakiwemo wa viti maalumu wanaruhusiwa.
“Mikutano iliyozuiwa ni ile ya operesheni, kama vile ni ya kitaifa na kuanza kuzunguka nchi nzima.”
Kuhusu kurejea CCM kwa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, Dk Bashiru alisema kulikuwa na mazungumzo ya muda mrefu na alitakiwa aombe upya uanachama.
“Kulikuwa na mazungumzo kwa upande wa chama baada ya kupokea maombi yake. Na yeye hakuwa mtu wa kwanza, wapo wanachama tuliwafukuza ndani ya chama wakandika barua wenyewe wakikiri makosa yao. Vikao vilikaa wakafikiriwa, wakasamehewa na Lowassa alikuwa mmoja wao,” alisema Dk Bashiru.
 
Unafiki wa kupindukia na kujitoa ufahamu. Huyu kabla ya kuingia CCM alikuwa akiongea mambo ya maana sana, baada ya kuingia huko kayakana anadai ni mawazo yake binafsi sasa anaunga mkono yale ya chama cha wahuni! Anajua fika kwamba mawazo yake ndiyo mawazo ya Watanzania wengi lakini katanguliza tumbo lake mbele badala ya maslahi ya Taifa.

Hv ccm kuna nini lkn?kwann hata ukiwa Prof ukiingia tu ccm akili zako zinakua kama za std 7
 
Unafiki wa kupindukia na kujitoa ufahamu. Huyu kabla ya kuingia CCM alikuwa akiongea mambo ya maana sana, baada ya kuingia huko kayakana anadai ni mawazo yake binafsi sasa anaunga mkono yale ya chama cha wahuni! Anajua fika kwamba mawazo yake ndiyo mawazo ya Watanzania wengi lakini katanguliza tumbo lake mbele badala ya maslahi ya Taifa.
COM = Chama Cha Mahuni?
 
Na majizi pia Mkuu. Wana mtandao wao wa majizi ukiongozwa na kubwa la majizi kuanzia Ikulu umetambaa serikalini, ccm hadi bungeni. Sasa wamejenga chuki kubwa dhidi ya CAG Assad kwa kuuanika hadharani mtandao wao.

COM = Chama Cha Mahuni?
 
Kwa maoni yangu Mwenyekiti wao wa Chama ndio hajapikwa kabisaa. Rejea lugha za kudhalilisha anazowatolea wateule wake na viongozi wenzake majukwaani. Sijawahi ona kwenye awamu yoyote tangia ya kwanza Waziri anaambiwa hadharani nakupa siku saba usipofanya jambo fulani nakufukuza! Au Waziri Mkuu anaambiwa kwenye mkutano wa hadhara nitawachapa shangazi zako!!!

Bashiri mwenyewe hajapikwa, kwahiyo hana uwezo wa kujua mtu asiyepikwa kisiasa yukoje na aliyepikwa anatakiwa awe vipi. Heshima aliyojijengea akiwa Mhadhiri pale UD anaiporomosha kwa kasi.

Ifike wakati watu wakatae teuzi za kisiasa kulinda hadhi na heshima zao kitaaluma ikiwezekana wabaki kutoa ushauri tu hata kama ni kwa kukodiwa(consultancy) maana ukikubali teuzi ukubali pia kukabidhi remote control ya ubongo wako kwa wale waliokuajiri
 
Unafiki wa kupindukia na kujitoa ufahamu. Huyu kabla ya kuingia CCM alikuwa akiongea mambo ya maana sana, baada ya kuingia huko kayakana anadai ni mawazo yake binafsi sasa anaunga mkono yale ya chama cha wahuni! Anajua fika kwamba mawazo yake ndiyo mawazo ya Watanzania wengi lakini katanguliza tumbo lake mbele badala ya maslahi ya Taifa.
Yeye na polepole walikuwa wanaharakati sema wameeingizwa huko akili zimewekwa makwapani kama jogoo
 
Inaonekana naye ni kamongo ila tatizo la kamongo sio rahisi kujua yupi ni dume na yupi ni jike maana wote wana ndevu
 
Why only Nape & Bashe ? You know what I mean.
 
Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bshiru Ally amesema licha ya kuwa Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye ni kiongozi mzuri na alikuwa mwenezi wa CCM lakini bado anahitaji kupikwa.

Ameyasema hayo leo Aprili 26, 2019 alipokuwa anahojiwa na Tido Mhando katika kipindi cha Gumzo la Uchaguzi kilichorushwa na Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC 2)

Akijibu swali aliloulizwa na mtangazaji Tido Mhando juu ya kuwepo kwa wabunge walio na kauli kali kama wanatia wasiwasi katika chama huku akiwatolea mfano mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe na Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye.

Akijibu swali hilo Dk Bashiru alisema
“Nape ni Mwenezi wetu, jasiri kabisa lakini anahitaji kupikwa. Nilichokuwa nasema siyo nakubali kila kitu bali mtambue kuwa chama kinawajibu wa kuwasikiliza, kuwaandaa, kuwaamini na kuwasimamia kama wanakwenda inavyotakiwa.”

“Lakini kwa jinsi hali ilivyo ni kati ya watu ambao wana mchango mkubwa na ndiyo maana nimeomba chama tujenge chuo cha kuandaa viongozi kutoka nchi sita tofauti ili tuweze kuandaa viongozi waliochipukia kwa sababu suala hili linahitaji maarifa na bila shaka tutakuwa na kina Nape na Bashe wengi,” amesema Dk Bashiru.
Ni kweli, yaani Mh. Nape na Bashe hawaishi misingi ya Uongozi ndani ya CCM.
 
Back
Top Bottom