Nashukuru kwa kuanzisha uzi huu, kipindi ni kizuri lakini ukweli narudi ukweli kuwa mtangazaji anapwaya sana, wanaoalikwa wanaongoza mazungumzo nayeye anafuata nyuma, ni mara kadhaa hana uhakika na hoja zake na hivyo waalikwa baada ya kuulizwa swali, wanaligeuza wanavyotaka wao na yeye haoneshi kuwa ni mtangazaji akiyeiva kushirikia swali lake na maudhui ya swali lake, ANAPWAYA SANA MTANGAZAJI HUYU, ITV kama ina watangazaji walioelimika basi wapewe kipindi hicho.
Wassira jana kapindisha maswali kibao harafu mtangazaji hajui la kufanya, anapunguza wasikilizaji wa kipindi badala ya kuwaongeza, swali kuhusu kuzomewa, swali kuhusu ccm kuwa makundi makundi na kushindwa 2015 mfano wake ulikuwa hoja za maige, yeye akajibu mfano wa swali sio swali, MTANGAZAJI alikuwa wapi???; Makundi anajibu hata vyama vingine yapo, sasa kweli hilo ndo jibu la hilo swali??? mtangazaji uwezo kiakili am very sorry umapwaya.
Mimechukua mifano michache tu lakini kila nikisikiliza kipindi hicho mtangazaji anapwaya sana, aidha hana uwezo kielimu au kiasilia hawezi vipindi vya aina hiyo; apishe vijana wenye uwezo au abadilike sana, ajue agenda yake kwenye swali ni nini na asimamie maswali yajibiwe, ni afadhali swali likose jibu kuliko blabla tu.
Kipindi ni cha maswali yenye utata/magumu sio maswali ambayo kila mtu analojibu haitakuwa na maana kabisa; aandae maswali vigongo yenye manufaa kwa TZ, aombe yajibiwe, asimamie swali lijibiwe sio mtu atunge lake harafu aanze kujibu.