DJ kwa simu yako ya Android.

DJ kwa simu yako ya Android.

castongo

Member
Joined
Mar 16, 2008
Posts
57
Reaction score
74
Pengine umewaalika rafiki zako nyumbani. Una party ndogo. Unachezesha miziki kwa laptop yako. Laptop yenyewe umeiweka kwenye meza ya pembeni karibu na chanzo cha umeme, au pengine karibu na Amplifier yako au music system yako. Ni wazi huwezi kuiweka laptop kwenye meza ulipoketi na rafiki zako, watakushangaa.

Tena kuna glass, chupa za vinywaji na vitu vingine ambavyo usingependa viwe karibu na laptop yako. Au utafute mtu mwingine atakayeshughulikia mambo ya muziki. Lakini haitajiki maana parti yenyewe si sherehe kuuubwa kihivyo uanze kutafuta Dj.

Usihangaike unaweza kubaki mezani na rafiki zako, mnakunywa mnaongea, bila kuifuata laptop pembeni kule, ukawa unabadili miziki, unapunguza sauti unaongeza sauti una-pause, una-stop, una-play nk. kwa kutumia simu yako ya android!

Najua umeanza kuwaza zile apps zinazoenda kwa "BLUETOOTH". Hizo sio mbaya pia, halafu naomba kama unazipatapata uzimwage kwenye mwendelezo wa uzi huu. Pia kuna uwezekano wa kuchezesha miziki iliyo kwenye simu yako kwa kupitia bluetooth kwenda moja kwa moja kwenye music system, sizungumzii hiyo pia, maana katikati hapo muziki unapoteza ubora. Miziki ipo kwenye laptop. Katika mbinu hii unatumia WIFI.

Kama una wifi network, ni nzuri, maana utaunga simu yako na computer yako kwenye network hiyo. Manake ziwe kwenye network moja. Lakini kama huna usiogope, maana simu yako ina kitu kinachoitwa WIFI HOTSPOT" au pengine majina mengine kama tethering, hotspot nk, utatumia hiyo hiyo (tutafundishana hapa).

Kwenye computer download program inayoitwa "Music Bee" ni ya bure na ni nzuri sana click hapa uende site.

Uzuri wa hii program ni kwamba unaweza kuwa na playlist nyingi sana na ukapanga miziki kwenye computer yako kwa namna nzuri ajabu. Android hawakuchelewa kutengeneza remote yake, inayotenda kwa simu za android kwa kupitia WIFI download hapa. (sijui kama kuna ya Ios) Ukisha install kwenye cm na kwenye computer na baada ya kuziunga kwa wifi; process inayobaki ni ndogo sana.

Kwenye ile music-bee ya cm gusa juu kushoto kwenye vistari vitatu, kisha settings, kwenye settings juu kabisa utaona Manage connections gusa pale. Kwenye hii ya kwenye computer uta-klick juu kushoto, penye jina MusicBee nenda tools, nenda MusicBee remote utaona private address, ndo ya kuweka kwenye ile ya kwenye simu. Mambo safi.

Enjoy. Binafsi natumia hiyo.

Ukifaulu, wasaidie na wengine wenye maswali kwenye uzi hapa.
 
Back
Top Bottom