Dj Khaled aongeza nguvu kwenye albamu yake mpya

WilsonKaisary

JF-Expert Member
Apr 4, 2017
392
926
Dj Khaled amezidi kuipa nguvu albamu yake mpya ‘Grateful’.

rihanna-dj-khaled-club.jpg


Rapper huyo ameamua kuwaongeza mastaa wengine wawili, katika albamu hiyo, wakiwemo muimbaji Rihanna na Rapper Nas. Khaled amesema hayo mjini Los Angeles, katika Power 106 ambapo kwa msanii Rihanna, itakuwa mara yake ya kwanza kushirikishwa na DJ Khaled katika nyimbo, huku Nas akiwa tayari alishasikika katika albamu yake iliyopita ya ‘Major Keys’.

Mastaa hao wataungana na wasanii wengine katika albam hiyo ya ‘Grateful’ wakiwemo Chance The Rapper, Travis Scott, Mariah Carey, Bryson Tiller, Future, Alicia Keys, Lil Wayne, Justin Bieber na wengine.

Wakati huo huo Jay Z na Beyoncé ni sauti nyingine zitakazo sikika kwenye albamu hiyo ambapo tayari walishirikishwa kwenye wimbo wa ‘Shinning’ uliotoka mwezi Februari mwaka huu, ambao nao utakuwemo kwenye albamu hiyo.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Top Bottom