Mhaya
JF-Expert Member
- Aug 20, 2023
- 2,563
- 7,321
Wengi wetu ambao ni wapenzi wa vipindi vya radio tutakuwa tunamfahamu DJ Fetty ambaye alianza kazi ya utangazaji muda mrefu katika stesheni ya Radio Ya Mawingu (Clouds FM). Alikuwa nguli wa kipindi cha XXL kilichokuwa mahususi kwa vijana na wapenda burudani hasa mziki, miaka hiyo bado unafuta kamasi kwa mkono miaka ya 2000s mwishoni kuja 2010s akiwa binti mdogo tu, na badae miaka kadhaa hakuonekana tena kwenye radio kwa muda mrefu. Ila miaka badae katika utawala wa Magufuli (sikumbuki Mwaka gani) aliweza kurejea tena kama Mwandishi wa habari akitangaza vipindi kama Jahazi cha jioni na badae Power Breakfast cha asubuhi.
Akiendelea na kazi yake ya utangazaji wa kipindi cha Power Breakfast hivi karibuni amekuwa hasikiki tena Redioni kama ilivyokuwa kawaida yake akitema cheche mbalimbali kuhusu masuala ya kijamii, kisiasa, uchumi na mambo mengine ya maendeleo yanayohusu jamii katika kipindi icho pendwa cha asubuhi. Kutokusikika kwake kumeleta maswali mengu huku bloggers na watu wengine maarufu wakihusisha kuwa DJ Fetty kasimamishwa kazi kwa sababu ya watawala wa Nchi kutoka ngazi za juu wametoa maelekezo kwa Boss wa Radio ya Mawingu (Clouds FM) kuwa asimamishwe kazi.
Mwanasiasa kama Godbless Lema ameandika kwenye Instagram
Na Martin Maranja Masese ambaye ni content creator na blogger ameandika;
Ikumbukwe DJ Fetty amekuwa na Misimamo ambayo inatetea wananchi na muda mwingine kutoa maoni mazuri katika kipindi cha radio na muda mwingine kwenye ukurasa wake wa Instagram wa TheBestFetty kwa ajili ya kujenga Nchi yake. Ila jambo hilo inasemekana ndilo limepekea yeye kusimamishwa kazi kwa sababu mamlaka hazitaki kukosolewa. Na ukizingatia mwaka huu 2025 ni mwaka wa uchaguzi wa urais, ubunge na udiwani.
Sio hivyo tu, kuna waandishi wa habari nguli na maarufu wa radio na TV maarufu Jijini Dar es Salaam wamefungiwa na Bodi ya ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) kutangaza au kufanya kazi ya uandishi wa Habari kwa kile kinachoitwa “kushindwa kujisajili katika bodi ya ithibati”
Mpaka zinaandikwa habari hizi Wahusika na mwaajiri wao wamefanya siri kwa mujibu wa maelekezo waliyopewa na serikali kuwa “wasifanye kazi ya uandishi wa habari na wasiseme lolote kuhusu kuzuiwa kwao”
Kwa mujibu wa kifungu cha 19 cha sheria ya huduma za habari sura ya 229 kina weka masharti kuwa
“waandishi watakaoshindwa kujisajili hawataruhusiwa kufanya kazi za kihabari”
Waandishi hawa wamewekewa kikwazo hiki baada ya kuwa mwiba katika vipindi vyao na mahojiano yao kwa wakati huu nchi inapoelekea katika uchaguzi Mkuu.
Uchunguzi unaonyesha Masoud Kipanya ameingia katika kifungo hiko pia baada ya kuchora mchoro wa katuni uliowakasirisha watawala ,uliolenga kutaka media zisitumike kama Toilet Paper
Mwenyekiti wa Jukwa la Wahariri Tanzania Balile aliongea na kuonyesha hadharani kukasirishwa na mchoro huo huku akiahidi Masoud Kipanya achunguzwe na mamlaka za nchi. Kipindi hiki kimekuwa kikihoji mfano ciza aliwai kupiga simu kama mwananchi wa kawaida hospitali ya Mwananyamala huku akiwa kwenye kipindi cha Power Breakfast akiuliza kuhusu uwepo wa ambulance ya wagonjwa na haifanyi kazi, pia wamewai kuhoji kuhusu foleni mbalimbali kama za Dar na mambo chungu nzima yanayohusu maendeleo ya nchi.
Masoud Kipanya na Ciza wote pia wa kipindi cha Power Breakfast wameshindwa kujisajili kwa sababu ya kukosa sifa ya kusomea taaluma ya uandishi wa Habari kinyume na sheria kama inavyoelekezwa katika kifungu cha 24 cha sheria ya huduma za habari sura ya 229.
Rungu la namna hii pia linaonekana kumkumba mwanahabari na Mkurugenzi wa Jambo TV, John Marwa ambaye amekuwa mwiba katika mahojiano mbalimbali na kuendesha vipindi vilivyo wakwaza watawala.
Duniani kote watu wenye uzoefu na kazi ya uandishi wa habari kwa zaidi ya miaka 10 kama Masoud Kipanya, SIZA, na John Marwa walipaswa automatically kuwa na sifa za kusajiliwa na bodi ya ithibati ya Waandishi wa Habari kwa kigezo cha uzoefu na muda waliofayia kazi tasnia ya habari.
Hawa ni baadhi ya Waandishi wa Habari wakubwa Duniani ambao hawakusomea taaluma ya uandishi wa Habari Anderson Cooper (CNN na ABC News) Stephen A. Smith (ESPN) na Trevor McDonald (ITN na ITV)
My Take: Mimi binafsi ni msikilizaji wa radio hasi hawa wakongwe wa Tasnia ya utangazaji kama Masoud Kipanya, DJ Fetty na kijana chipukizi wa habari Ciza katika vipindi hivi maridhawa kama Power Breakfast. Maoni ambayo uwa anayatoa DJ Fetty, Masoud Kipanya na Ciza uwa ni ya kujenga zaidi na hawajawai kuwavunjia heshima moja kwa moja viongozi au serikali kwa sababu wanaheshimu miiko ya kazi, kwa wengi tunaowasikiliza tunaelewa hili. Na ndio maana hata kama wamesimamishwa kazi basi waliowasimamisha kazi wamemtumia bosi wao na sio Wizara ya habari kama tunavyowaona waandishi wa habari wengine wakipigwa marufuku na wizara husika hadharani, hii inamaana kuwa hawakutaka kuleta attention kwenye jamii kwa sababu kosa walilosimamishwa kazi nalo limekaa kisiasa na watu wangehoji hivyo kumtumia bosi wao kuwasimamisha kazi watu wataona ni kama kusimamishwa kwa mambo ya kiofisi tu.
FID Q aliwai kuimba kwenye kibao chake kimoja kinachoitwa Bongo Hip-hop, alisema "Sio tu Bongo, Mpaka Ng'ambo Hakuna Uhuru wa Habari, Kuna Uhuru wa Mwenye Chombo... Mitambo na Mwenye Mali" akaongeza kwa kusema "Kujifanya hawasikii... Haiwasaidii... wala haiwajengi... unachosema ni... Kamwe IPP haitompinga Mengi"

"DJ Fete, Kupitia maumivu ya kusimamishwa kazi kwa sababu ya msimamo wako, najua si rahisi lakini naamini ndani yako kuna kitu kikubwa, msimamo wa kweli, ujasiri wa moyo, na heshima kwa dhamira yako. Walio kusimamisha wana mamlaka ya leo, lakini Mungu ndiye anayeshika kesho.Usiogope. Mara nyingi mlango unapofungwa kwa nguvu, ni ishara kuwa Mungu anafungua mlango mkubwa zaidi , mlango wa heshima, wa uhuru, na wa mafanikio yasiyotegemea mnyororo wa hofu.
Endelea kuwa mwaminifu kwa kweli, msimamo, na utu wako maana kesho ni bora kwako kuliko jana.Mbele yako kuna mlango usiofungwa na mkono wa mwanadamu.
Much ❤️"
Na Martin Maranja Masese ambaye ni content creator na blogger ameandika;
"Pole sana Bi. Fatma Hassan Ahmed (@thebestfetty), DJ FETTY. Tunaelewa kwamba wenye mamlaka wameelekeza uondolewe katika kipindi cha radio, asubuhi. Ndiyo maana wasikilizaji hawaisikii sauti yako tena. Tunaelewa, mwajiri wako amepewa maelekezo na amepokea na kuyafanyia kazi. Kwamba, kwa kuwa (wewe) ni mkosoaji, ukae pembeni. Jamii nzima inatambua kwamba, wewe ni mwanahabari nguli uliyekidhi vigezo vyote vya kitaaluma, usivunjike moyo. Tumia kuta za mitandao yako ya kijamii kuendelea kuhabarisha umma. Faida itakuja kesho. Katika ulimwengu wa sasa, mainstream media siyo mlango pekee wa kufanikiwa katika tasnia ya habari na mawasiliano. Social Media ni jukwaa kwa kila mtu. Unaweza kuwekeza nguvu katika 'podcast' yako sasa. Jikite hapa. Tutakusoma na kukusikiliza. Usijute na kuumizwa na jambo hilo. Bosi ameshindwa kukulimda mbele ya meza ya watawala katili. Amechagua kuwa mbinafsi. Naelewa, kwa heshima uliyonayo kwake, na labda hofu ya kuikwaza mamlaka, hutoweza kusema - utabaki na mamumivu tu. Lakini sisi TUTASEMA kwa niaba yako. USIOGOPE. Wenye hatia wanayo hofu. The guilty are afraid."