DJ Fetty wa Power Breakfast ya Clouds FM asimamishwa kazi na maagizo kutoka mamlaka za juu kwenda kwa Bosi wake sababu za Kisiasa

DJ Fetty wa Power Breakfast ya Clouds FM asimamishwa kazi na maagizo kutoka mamlaka za juu kwenda kwa Bosi wake sababu za Kisiasa

Ni sawa

Lakini Fetty hajawahi kuwa biased…. Anapiga kote
Tatizo linaanzia hapa
1000048154.jpg
 
Hio kombinenga ilikuwa mfano wa pilau la mbuzi na kachumbari ya pilipili nya nya na limao.....walikuwa wanajua hasaa kupita hasa wakimuweka waziri kati kumuhoji lazima apate kizunguzungu...maana walikuwa na details pia uwezo wa kutizama mambo kwa jicho la tatu
 
Acheni propaganda wakuu ,issue kubwa ni ITHIBATI ,kuna watu wanapiga SPANA kuliko hata Kipanya lakini wapo ,hivi unamjua vizuri CHARLES WILLIAM Shahidi wa JAMHURI(WASAFI) au SAMSON CHARLES(EATV /EA RADIO)? Hao jamaa "hawacheck na wowote" wanapiga SPANA za hatari lakini bado wanaendelea na shughuli.

Hakuna Serikali ambayo inaweza ikatoa order ufukuzwe kwenye ajira bila kuwa na vitu ambavyo watasimamia kama ground ,kwasababu ukifukuzwa kwa order kutoka juu ,mwajiriwa akienda CMA utamlipa fedha za hatari kwa issue ya UNFAIR TERMINATION ,hivyo mwajiri lazima awe na ground ya kukufukuza.

Hapa wengi wanaleta siasa tu kwasababu hawajui chochote kuhusu sheria ya ajira kazini ya mwaka 2004...Mwajiri hawezi kukufukuza bila kuwa na ground lazima afuate mchakato wa kukufukuza na asipofuata mwajiriwa akienda CMA utamlipa pesa ndefu kwasaabu ya UNFAIR TERMINATION.

Nasisitiza DJ Fetty ,Masoud Kipanya ,CZA ,Zembwela ,Kitenge ,Dina Marious na wengine wanaofanana na hao waende Bodi ya ITHIBATI wakasajiliwe.
Hii ni siasa bhana poli bin tics
Acha maneno mingi
 
Kwn serikali inataka nini? Tuwe mazoba, matahila ,mbumbumbu, au wasengenyaji?
Kwanini wasitumie maneno ya watu km kioo kujikosoa na kujijenga ?
 
Ukweli hausemwi ila kidogo nitakudokezea

Vipindi hivi vya asubuhi vya hizi redio 2(Clouds na Wasafi) vimekuja kuwa mwiba mchungu kwa watawala sababu vimeweza kuamsha ari ya wajibu na haki kwenye jamii. Kwa Kipanya ishu ilianzia kwenye utekaji na namna polisi walivyokuwa wanajichanganya majibu yao, ishu za haki za watu kisheria ilikuja kuonekana jamaa anachokonoa sana mpaka ambako hakutakiwi kufikwa. Zembwela ni mtu wa mtaani kitambo, anayokuwa anayazungumza hayafurahiwi na watawala hata kidogo lakini ndivyo jamii inamotatizika na mengine ni ya wazi kabisa. Kipanya aliwahi kuzisema sana taasisi nyeti za serikali wanazoomba wafanye nao kipindi mwisho wa siku taasisi zile hawatoi mrejesho wa kushiriki.
 
Mtu wa karibu na Fetty amtonye kuacha kung'ang'ana mshahara wa laki 4 clouds ashakua brand kubwa atengeneze ata podcast yake apo full uhuru kuongea unachotaka mtaji wa muhimu ambao ni recognition anayo na C.V yake inajieleza.
 
Mtu wa karibu na Fetty amtonye kuacha kung'ang'ana mshahara wa laki 4 clouds ashakua brand kubwa atengeneze ata podcast yake apo full uhuru kuongea unachotaka mtaji wa muhimu ambao ni recognition anayo na C.V yake inajieleza.
Fetty analipwa Laki 4??? Duh kumbe hamna maana KABISA ya kuwa clouds pale Dah!!!!
 
Back
Top Bottom