Hawa madogo wa xxl nawakubali ila sometimes wanakuwa "very four"
Huwa sielewi uwepo wa Basata ila hata Ng'ombe na udunya wake lakini tukumbuke ana uwezo wa kupiga teke, sasa kama utamuacha mwanao akampapase kwa sababu tu hapo nyumbani mmezoea kumpapasa na hana madhara kuna siku utarudi mtoto taya inaning'inia.
Pili huyo Shilole anayetetewa ni wachache tu wasiojua kuwa amefyatuka, sasa kuanza kumtetea kama vile hilo limemkuta Nyota Waziri ni ajabu.
Hata leo tukipiga kura ya wanaounga mkono adhabu ya Basata mtaambulia kura za baadhi ya Wanaclouds na Nuhu.
Alafu ndugu zangu wa Clouds muache kudhani kwamba ndio mnaopaswa kufahamu kila jambo, nyie wenyewe mpaka wa leo kuna wasanii mmewaweka kifungoni kwa muda usiojulikana....na sijui kama hao BASATA wamewahi kuwahoji...na kama wamewahi kufanya hivyo sijui ni jibu gani mliwapa kuhalalisha kwani mpaka wa leo hatuwasikii kina 20% na wengineo.
Kama nyie mkikerwa mnaumia na kuadhibu basi ndivyo na hao BASATA wanavyolazimika pale wanapokerwa, au kuadhibu muachiwe nyie wengine wabaki kushabikia ?
Na swala la mbona na fulani alifanya hivyo halina mantiki na halipaswi kuhojiwa na mtu yeyote mwenye uwezo wa kupima mambo.
Adhabu ya Shilole ni sahihi na tumieni muda huu kuhimiza Wasanii kujali staha wawapo jukwaani.
Anayekwenda kuangalia Kangamoko huenda kwa ridhaa yake na hutarajia kuona anayoyaona, ila kuandaa jukwaa la muziki na kuwakuta Kangamoko nao wapo ni dhuluma kwa wasiopenda hayo.