Baada ya Ruge na Sugu kupatana... Mkoloni atangaza vita zaidi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baada ya Ruge na Sugu kupatana... Mkoloni atangaza vita zaidi

Discussion in 'Entertainment' started by MziziMkavu, Feb 26, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Feb 26, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  [​IMG]Na Julieth Kulangwa
  Fredy Mariki a.k.a Mkoloni ambaye ni swahiba na msaidizi wa mbunge wa Mbeya, Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu amesema vita ya kuwashughulikia virusi wa muziki wa Bongo Fleva inaendelea hata baada ya muafaka huo.

  Mkoloni amesema, makubaliano ya Sugu na Ruge Mutahaba ni sehemu tu ya vita waliyokuwa wakipigana, kwani bado kuna virusi wengine wanaoharibu muziki huo.

  Msanii huyo ambaye ni mwenyekiti wa Chama cha Wasanii wa Bongo Fleva nchini, TUMA amesema maandalizi ya kutoa 'mixtape' ya Ant Virus volume 3 yanaendelea na itakuwa hivyo mpaka soko la muziki

  "Tunapenda kupongeza mafanikio yaliyotokana na mixtape ya Anti virus vol 1 na vol 2,kwani ndio yaliyopelekea muafaka uliokuwa umetugawa wasanii na kutufanya tukose haki yetu ya msingi, ikizingatiwa kuwa T.F.U ni kanjanja iliyokuwa imejificha kwa maslahi ya watu wachache na badala yake sasa kinakwenda kuwa chombo cha wasanii wanachama wa TUMA kwa wale waliopo na watakaoendelea kujisajili,

  Tunafurahi sana na kupongeza jitihada za makusudi zilizochukuliwa na serikali kupitia wawakilishi wake yaani Waziri Nchimbi na Tundu Lissu kwa kuweza kutambua hoja za vinega zilikuwa za msingi na hatimaye kufuta T.F.U,

  Lakini pongezi zaidi ni kwa hatua ya kukubali kuirejesha studio iliyotolewa na Rais kwa kuileta kwenye mikono salama kwa maana ya TUMA chini ya BASATA, tunalipongeza hilo na tunapenda kuwaambia wasanii wengine ambao walituona wajinga tusiokuwa na akili kuwa tulijua tunachokisimamia, alisema na kuongeza.

  Sasa ni wakati muafaka wa kuunganisha nguvu zetu ili tuendeleze harakati na mapambano ya kumkomboa msanii wa Tanzania kwa kuwachana mameneja masoko,wasambazaji,madj wenye utamaduni wa zamani na yeyote atakayejitokeza na kuzingua tasnia ya sanaa kwa ujumla wake,

  Tunapenda watu wajue kuwa vita yoyote lazima iwe na malengo....sasa adui kanyanyua bendera nyeupe juu watu walitaka tumuue? na baada ya kumuua vp madai yetu??? tulikuwa na agenda na zote zimesikilizwa na kukubaliwa na si vinginevyo sasa ni kusonga mbele kwa mixtape vol 3 kwa virusi wengine.....ikumbukwe harakati haziwezi kumalizwa kwa kutatua tatizo moja,bado wengine kibao wapo na tuna kazi nao vile vile, alimalizia Mkoloni ambaye ni mwenyekiti wa chama hicho.
  chanzo.
  http://www.mwananchi.co.tz/makala/-/20550-baada-ya-ruge-na-sugu-kupatana-mkoloni-atangaza-vita-zaidi
   
 2. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #2
  Feb 26, 2012
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Point....nimeipenda hii
   
 3. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #3
  Feb 26, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,787
  Likes Received: 36,783
  Trophy Points: 280
  'Adui kainua bendera nyeupe, mlitaka tumuue?'
  Nimeipenda sana kauli hii.
  Hakika harakati za ukweli huwa na tabia za kubezwa mwanzoni ila mwishoni tunafurahi pamoja.
  Hongera vinega kwa kurejesha studio iliyokuwa imetekwa na Mutahaba, hongereni pia kwa kufanikisha kuifuta T.F.U kwani ilikua ni kwa ajili ya wizi kwa wasanii.
  The one who laugh lastly laugh longer.
   
 4. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #4
  Feb 26, 2012
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  ushindi mara zote una baba wengi lakini kushindwa mara zote ni yatima!!!!!
   
 5. L

  LA TOVI Member

  #5
  Feb 26, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Amenikumbusha mapambano ya ndondi kwani ukiwa ulingon ukimchapa mpinzani na akachapika vilivyo taulo hulushwa uwanjan ili kumuokoa na thahama ya makonde.
   
 6. kadoda11

  kadoda11 JF-Expert Member

  #6
  Feb 26, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 16,225
  Likes Received: 8,298
  Trophy Points: 280
  ....hata hivyo bado rugay huwa haaminiki.vinega endeleeni kumchana ktk volumes zenu ili asije akajisahau na kuanza tena dhuluma zake.
   
 7. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #7
  Feb 26, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Sugu asiwasahau tu VINEGA na wale mashabiki wake wote!
   
Loading...