Dizasta Vina Mwana Hip-hop Ndio Best Story Teller Hana Mpinzani

Nikitoa maoni yangu nitashambuliwa wote mliochangia huu uzi hamjui storytelling.
Art ya storytelling sio kuhadithia hadithi za utam kolea. Huyo dizasta ajifunze kwanza kuchana
 
Hatia VI niliirudia mara kadhaa kuelewa kumbe baba anayezungumziwa mule ni Mungu. Aloo kapita naesafi
 
Habari,
Kila Mmoja Anaendelea Vyema Kabisa Na Majukumu Ya Kila Siku.

Dizasta Vina Hadi Sasa Ndio Rapper Mkali Sana Katika Utunzi Na Uaandishi Wa Mashairi Hapa Tanzania. Sijaona Rapper Mkali Zaidi Ya Dizasta Vina Hata Katika Upande Wa Namna Anavyochana.

Ukimsikiliza Dizasta Vina Utaona Kabisa Uandishi Wake Ni Mtu Mwenye Uwezo Mkubwa Sana Na Ubunifu Wa Hali Ya Juu Sana.


Turudi Kwenye Mada Ya Kwanini Nasema Ni Best Story Teller Kupitia Mashairi Anayoimba. Ukisikia Nyimbo Zake Anavyopangilia Matukio Na Uandishi Wa Vina Unabaki Pale Pale Katika Ubora Na Ustadi Wa Juu.

Kuna Watu Wanaweza Kuwa Hawamfahamu Dizasta Vina Nitawawekea Baadhi Ya Ngoma Hapa Chache Mkasilize Baadae Mlete Mrejesho Juu Ya Utunzi Na Uandishi Wa Msanii Huyu.

Kuna Muendelezo Wa Project Yake Inayoitwa HATIA Ambayo Hutoa Kila Maana Ya Mwaka Au Miaka. Hapa Alianza Kwa Kutoa Nyimbo Nyingi Ila Kuna Hatia I, Hatia II, Hatia III, Hatia IV Na Hatia V.

Kuna Hatia III Hii Ngoma Nilimkubali Sana Hapa Anazungumzia Namna Tulivyosahau Tamaduni Zetu Za Asili Na Kukimbilia Za Ughaibuni Na Namna Tunavyoathirika Navyo Katika Nyanja Zote Kijamii, Kiuchumi Na Kisiasa.

Kumi Zangu Bora Za Dizasta Vina Ni Hizi Hapa:

1. Dizasta Vina - Hatia III
2. Dizasta Vina - Hatia V
3. Dizasta Vina - Hatia IV
4. Dizasta Vina - Kanisa
5. Dizasta Vina - Kibabu Na Binti
6. Dizasta Vina - Wimbo Usio Bora
7. Dizasta Vina - Hatia II
8. Dizasta Vina - Shahidi
9. Dizasta Vina - Hatia I
10. Dizasta Vina - Tribulation (Dis Track Kwa Rapcha)

Kama Hujawahi Msikiliza Dizasta Vina Basi Pitia Hizo Ngoma Uje Kuleta Mrejesho Ila Jamaa Hadi Sasa Hana Mpinzani Katika Uandishi.

Nawasilisha Mzee Mkoloni.

Cc: Kichwa Kichafu
Kama kuna anayebisha bila shaka atakuwa mpenzi wa Taarab.
 
Hatia VI
Acha jala
Uwaridi jeusi ndoa is overrated
Money
Kanisa
Shahidi
Dizasta ni kisanga the best storyteller
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom