Dizasta Vina a.k.a Maradona

Mwanajua imetoka 27 Dec 2020 na JPM kafariki 2021

Kwani alivoimba almasi umeelewa ?

Kamzungumzia Diamond Platnumz miaka mingi mbeleni!

Navoamini mimi Dizasta ni kama time traveller anaandika vitu vya kufikirika sana ni kama utabiri..sometimes concept zake ni kama nabii tunasubiri zitimie

Huu ni mtazamo wangu!

Naheshimu mtazamo wako pia

Ila mwanajua bado inanisumbua natamani nikutane na dizasta nimuulize,alikuwa anamaanisha nini?

Nmepitia comments nyingi YouTube wengi pia wanafikiria “clouds fm” or “JPM

So nawew unaeza share code zako

Ni maoni sio sheria,so be free
 
Ndio maana nikakwambia weka mstari ambao huuelewi nikujuze.
 
Jamaa namkubali sana
 
Walikuja madogo wajanja na mapesa
Wakauliza mama ukivaaje unapendeza
Wakamuahidi ndizi, mawaridi na hariri
Lakini jasiri rangi yake ya asili ilitesa
Jamaa kagoma kutuletea tafsiri
 
Jamaa kagoma kutuletea tafsiri

Kapotea tena..[emoji1]
Wakati aliomba line atafsiri

Ngoja nimpe code[emoji725]

Hapo imezungumzwa bongo fleva ya akina janjaro

Amezungumzwa jasiri mwongoza njia

So..ukifatilia vizuri utaona hii ilikuwa “clouds fm” against “music industry”

Dizasta is the master of big words[emoji28]
 
Na ukitaka kuielewa “THE VERTELLER “sikiza kwa mpangilio kuanzia track 1-20 bila kuruka

Mpangilio wa jumla wa albamu ni kwamba
[emoji736]msimuliaji anazaliwa,
[emoji736]msimuliaji anajifunza na
[emoji736]kisha anafanya makosa,
[emoji736]anaingia kwenye mapenzi,
[emoji736]anajuta,
[emoji736]msimuliaji anapata faraja na
[emoji736]mwisho wa siku msimuliaji anakufa.!

 
Kwa muktadha huo track ya “mwanajua” ipo kene category [emoji736]kufanya makosa
 
Sasa mkuu mbona nawewe unachanganya tena madesa, mwanzo unasema ulihisi inaongelewa clouds, badae ukajiridhisha kuwa anaongelewa JPM...!

Hence umerudi tena kwa clouds, itoshe kusema kuwa jamaa katuumiva vichwa na ataendelea kutuumiza vichwa hadi pale atakapoamua mwenyewe kutoa tafsiri rasmi
 

Ofcoz bado naumiza kichwa kipi hasa kati ya hivo
Maana kwangu vyote vina “click” hizo concept 2

Ndo maana nakaribisha mawazo mbadala na hoja

Ili tupate tafsiri kamili..I’m very flexible

Ili mradi tu mtu aje na hoja! Ili tufungue code
Kama ilivofanyika kene shahidi

Ni mtazamo binafsi na Niko tayari kurekebishwa.

that’s all
 
Naheshimu mawazo yako mkuu
 
Concept behind?
"Alizaliwa mashariki alifahamika mahali pote"
Hapo zingatia upande ambao jua hutokea alfajiri.

"Alitamalaki nuru ilitua mahali kote"
Hii inajieleza yenyewe.

"Hakuna aliyemgusa kwani alikuwa wa moto sana"

Hii line inaelezea character ya jua.

"Tuliwaonea wivu rafiki zake Mekuli na Veneranda"

Mekuli ni mercury, veneranda ni vernus. Hizi ni sayari zilizo karibu na jua, hivyo kwenye kazi yake ya uandishi kaziweka ni marafiki zake.

"Wazungu walikuja na pozi kibao
Walimkaribia mwisho walibabuka Ngozi zao"

Hii line inaonyesha wana anga wanashindwa kumsogelea kwa sababu ya joto.

"kuna walo'diri kumwita Mungu
Walitukuza walisadiki na kuabudu"

Hii ni kwa wanaoabudu jua.

"Tuliishia kumwona mbali na mwisho kuumia macho"

"Maana alingáa sana kiasi alizificha nyota kama wingu"


"Tulikosea kwani... zile sifa hazivai tena
Imefika jioni na yeye hang'ai tena"

Hapa anaonyesha ilivyofika jioni zile sifa zote za jua zikapotea.

"Najiuliza, alifichwa na ndugu kwenye kaya? Au alinenepa kutoka aliona haya"

Hii ni jioni wanamtafuta jua haonekani tena.

"Nuru yake pahala pote ilitawanyika
Toka mzizima pwani kote alipagawisha
Aliondoka na mwisho alionekana ziwa Tanganyika"

Kigoma kule ndio jua linapozamia "joke" ila utakuwa unajua jua huwa linaishia ziwa tanganyika kigoma huko kwa ukanda wetu.

"Dhahania zimeandikwa alichoka pengine
Aliondoka ili wang'ae nyota wengine"

Hapa ameonyesha kuwa jua ni nyota na anajiuliza usiku ulipofika aliondoka ila wang'ae nyota wengine? Akimaanisha hizi nyota za usiku.


Kwa hizo lines toka nilivyosikia siku ya kwanza niling'amua kuwa muhusika ni jua kama tafsida ambayo unaweza kuiweka kwenye jambo lolote linaloendana na mada.
 
Alizaliwa mashariki...... na mwisho alionekana ziwa Tanganyika (magharibi)
.
.
.
Tuliwaonea wivu rafiki zake mekuri na veneranda ( Mercury na Venus )

Haya Tafakari tena.

Halafu nitakwambia HATIA V kagusa nini
Hatia V mkuu, lete madini
 
Safi mkuu hadi hapo tuko pamoja na uko Sawa na tafsiri ya walio wengi ila kuna sehemu bado panahitaji msaada

Walikuja madogo wajanja na mapesa/

Wakauliza mama ukivaaje unapenda?/

Wakamuahidi ndizi,mawaridi na hariri/

Lakini jasiri rangi yake ya asili ilitesa/

Warembo wa dunia na vivazi vyao/

Walipanga kumfikia na ilibaki njozi kwao/
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…