Diwani wa CHADEMA mbaroni kwa rushwa

diana chumbikino

JF-Expert Member
May 29, 2018
428
368
1569059077900.png


TAASISI ya Kuzuia na Kupambana Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Morogoro, imemtia mbaroni Diwani wa Kata ya Katindiuka Halmashauri ya Mji Ifakara Mkoa wa Morogoro, Furaha Muhidini Nganya (Chadema) kwa tuhuma za kupokea rushwa ya Sh 200,000.

Diwani huyo anadaiwa kupokea rushwa hiyo kutoka kwa mfugaji (jina limehifadhiwa) ili amruhusu kulisha mifugo yake ndani ya eneo la Hifadhi ya Jamii la Iluma kinyume na utaratibu. Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Morogoro, Janeth Machulya alisema hayo jana katika taarifa yake kwa waandishi wa habari mjini hapa.

Machulya alisema uchunguzi wa Takukuru ulibaini kwamba Septemba 18, mwaka huu, mtuhumiwa huyo alipokea hongo ya Sh 200,000 kutoka kwa mlalamikaji, ambaye ni mfugaji katika Kata ya Katindiuka. Alidai kuwa diwani huyo aliomba rushwa hiyo kama kishawishi ili akubali kumruhusu mlalamikaji huyo, kulisha mifugo yake katika eneo la Hifadhi ya Jamii la Iluma lililopo Kata ya Katindiuka kinyume na utaratibu.

Kwamba mtuhumiwa huyo anatarajiwa kufikishwa wakati wowote katika Mahakama ya Wilaya ya Kilombero mjini Ifakara ili kujibu tuhuma zinazomkabili. Aliwakumbusha watendaji wa Serikali za Mitaa wa Mkoa wa Morogoro, hasa wale wanaowahudumia wananchi wa chini, kuacha kujihusisha na vitendo vya rushwa, ambavyo vinakoleza migogoro baina ya wakulima na wafugaji kwa lengo la kupata manufaa binafsi.
 
Back
Top Bottom