Diwani wa CHADEMA mbaroni kwa KUMBAKA YATIMA

tusiwe na double standard, kama alichosema huyu jamaa ni kweli, diwani ana makosa, "undue influence" hyo..., hata kama bibie sio minor
 
Angekuwa CCM humu JF pangekuwa hapatoshi.

Mimi nasema hivi, ikiwa kiongozi wa juu wa CHADEMA hivi sasa mwanamke wake ana kesi ya talaka kwa mumewe, Unategemea nini kutoka kwa Diwani wa CHADEMA? Maadili ni 0 (sifuri) CHADEMA.
 
Miaka 19?
Hivi yatima inaishia miaka mingapi?

Kama taarifa ni sahihi, basi kosa la huyo diwani ni kutumia vibaya ofisi....!
 
Diwani wa kata ya kijitonyama (Dsm) ambaye pia ni mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Ally maua kupitia CHADEMA Juma Athman Uloleulole, amedakwa na polisi na kufikishwa kituoni kwa kosa la kumdhalilisha kijinsia yatima na baadaye kumuomba rushwa ya ngono.

yatima huyo aitwaye Sylvia Kigola (19) alienda kulalamika polisi kwamba alipoenda kwa mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Ally maua kuandikiwa barua ya dhamana kwa ajili ya kwenda kuomba kazi ndipo mwenyekiti huyo alimgeuzia kibao na kumbaka.

Amefunguliwa kesi jalada no.KJN/RB/1117/2012.

Tukio hilo lilishuhudiwa na waandishi mbalimbali wa habari akiwemo wa ITV.

Source:taifa letu Tarehe 17.02.2012 ukurasa wa kwanza.

My take:Ni aibu kwa kiongozi wa umma kufanya kitendo kama hiki.hatua kali za kisheria zichukuliwe baada ya kuthibitika.

Kumbe kosa lake siyo la kubaka?Mbona kama sijakuelewa vizuri mtoa hoja?
 
Back
Top Bottom