Diwani wa CHADEMA, Ally Bananga amwambia Godbless Lema aache ndoto na kumpangia marafiki!

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,975
Diwani wa Kata ya Sombetini Katika Jiji la Arusha kwa tiketi ya CHADEMA, Ally Bananga amejitokeza kwenye chombo cha habari na kudai Godbless Lema na kundi lake waache mambo ya kijinga ya kumpangia marafiki na kumtabiria kuwa anataka kuhamia CCM.

‘’Lema na kundi lake wanataka nisiwe na marafiki kutoka CCM wakati wao wana marafiki kutoka CCM’’ Bananga alisema.

Aliendelea kusema, ‘’Madiwani wote waliohamia CCM kutoka CHADEMA wataendelea kuwa rafiki zangu wa karibu, nitakula nao, nitakunywa nao kwa sababu hawaathiri utendaji kazi wangu kama Diwani. Sidhani kama kuna muda wa kupangiana namna ya kuishi. Kila mmoja alikuja CHADEMA kwa muda wake, kwa matakwa yake na kama atataka kujiondoa, atajiondoa kwa muda wake na matakwa yake’’.

Kuhusu tuhuma za kuhamia CCM, Diwani Bananga alisema, ‘’wananitabiria ndoto za manabii wajinga ambazo ni sawa na kuipigia kura kanzu ya Yesu wakati kaivaa. Bado niko CHADEMA nina wajibu na watu wa Sombetini mpaka nitakapokabidhi Kata mwezi Juni mwaka huu’’ Bananga alisema.

Bananga amesema mambo yanayofanywa ya kupangiana maisha, kuingilia familia za watu na kutuhumiana ni utoto na ujinga hasa ikichukuliwa kuwa tuna miezi michache sana kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu.

Mimi na Diwani Isaya Doita tunapingwa ndani ya CHADEMA kwa sababu huwa hatulei ujinga’’ Bananga alisema.

Ikumbukwe kuwa, CHADEMA juzi ilitoa barua inayoonyesha Diwani wa Ngarenaro, Isaya Doita amefukuzwa Uanachama wa CHADEMA baada ya kumtuhumu Godbless Lema kuwa hajitambui na hajui majukumu yake.

Kusoma tuhuma za Lema gonga LINK> CHADEMA Arusha ‘’kwafuka moshi’’; Godbless Lema aambiwa hajitambui na hajui majukumu yake

Kusoma thread ya Diwani Isaya Doita kufukuzwa uanachama wa CHADEMA gonga LINK> Diwani Isaya Doita aliyemtuhumu Godbless Lema afukuzwa Uanachama

Diwani Bananga amebainisha kuwa hana urafiki wa karibu na Godbless Lema bali wana mahusiano ya kikazi kwa sababu Lema ni Mbunge wake na Mwenyekiti wa Kanda wa CHADEMA.

Kuhusu suala la kugombea Ubunge katika Jimbo la Arusha, Bananga amesema hakuna mtu aleyeandikiwa na daktari kuwa atakuwa Mbunge milele na atavuka mto akifika kwa sababu umri wake unamruhusu hata kugombea Urais wa Tanzania.

Kusikia kwa kirefu alichokisema Diwani Ally Bananga angalia hii Video.
 
CHADEMA katika Jiji la Arusha kunafukuta moto wa kisiasa!

Tunauona moshi wa kisiasa na kilichobaki ni moto wa kisiasa kulipuka!

Je,moto ukiwaka utakiteketeza chama au utazimwa kabla haujaleta athari kubwa!

Muda utatoa jibu sahihi!
 
CHADEMA katika Jiji la Arusha kunafukuta moto wa kisiasa!

Tunauona moshi wa kisiasa na kilichobaki ni moto wa kisiasa kulipuka!
Kwanza nikupongeze kwa umahili wa uchochezi na uchonganishi.
Pili nakushangaa wewe na genge lako kushindwa kutubandikia taarifa ya kikao cha hawa waunga juhudi cha pale nane nane.
Mwambie Bananga ni kweli ana dhamana ya watu wa Sombetini lakini ajue itakoma nje ya CHADEMA.
Halafu mkakati wote wa CCM kutumia vyombo vya dola kwa maagizo ya DC na RC kutumia fedha za halmashauri kwenye mchakato huu; una kosa moja tu, halijatugusa na halitafaulu kwa sababu Watanzania siyo wajinga. Na sisi wapiga kura wa Arusha tuna taarifa ya kinachoendelea kiganjani. HATUDANGANYIKI
 
Alichofanya diwani ndio uanaume, facts tu hakuna kuzunguka, ila kuna mtifuano unakuja Arusha hasa ubunge ikizingatiwa bwanayule mwenye mkoa wake inasemekana naye anajiwinda
Kwa yanayoendelea Arusha tutashuhudia mapambano makali sana ya kisiasa wakati wa mchakato wa uchaguzi mkuu!
 
CHADEMA katika Jiji la Arusha kunafukuta moto wa kisiasa!

Tunauona moshi wa kisiasa na kilichobaki ni moto wa kisiasa kulipuka!
Jamaa unahangaika sana na CDM Arusha, waambie hao CCM wenzako mwezi October waitishe uchaguzi free na fair halafu uone kitakachowapata Arusha, unadhani CDM Arusha inabebwa na majina ya watu kwa akili zako fupi! hukumbuki kilichowapata kwenye ule uchaguzi mdogo wakati ule.

Halafu napata shaka, kwanini hizi video unakuwa wa kwanza kila mara kuzileta huku kama na wewe sio sehemu ya huo mchezo wa kijinga mnaoufanya huko Arusha, kachezeeni akili za wapuuzi wengine, sio CDM Arusha.

Chezeeni hao hao kina Bananga na mwenzake, wengine wanajitambua, nakusubiri ulete tena video ya mwingine, jinga kweli!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
CHADEMA katika Jiji la Arusha kunafukuta moto wa kisiasa!

Tunauona moshi wa kisiasa na kilichobaki ni moto wa kisiasa kulipuka!
Toka umehamia Arusha sasa Chadema Arusha watakukoma. Siku hizi nyuzi zako ni za Chadema Arusha tuu.
Au yule mlezi wa CCM Arusha (sina uhakika ni mzee au kijana) ndio kakupa jukumu hilo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii movie mmeshaiharibu hata kabla haijatoka, but ndio kawaida yenu mara zote lazima mfeli tu, ukadhani utapata supporters wa ujinga bwege kweli, na huyo Bananga km anatafuta sababu asijali, atatupwa kule kama mwenzake.

CDM sio CCM inayawaogopa kina Membe na wenzake. Mngekuwa na akili hata kidogo mngebadilisha hata blogu, but mmekomaa na muungwana blogu hiyo hiyo, wapuuzi kweli na hiyo blogu yenu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza nikupongeze kwa umahili wa uchochezi na uchonganishi.
Pili nakushangaa wewe na genge lako kushindwa kutubandikia taarifa ya kikao cha hawa waunga juhudi cha pale nane nane.
Mwambie Bananga ni kweli ana dhamana ya watu wa Sombetini lakini ajue itakoma nje ya CHADEMA.
Halafu mkakati wote wa CCM kutumia vyombo vya dola kwa maagizo ya DC na RC kutumia fedha za halmashauri kwenye mchakato huu; una kosa moja tu, halijatugusa na halitafaulu kwa sababu Watanzania siyo wajinga. Na sisi wapiga kura wa Arusha tuna taarifa ya kinachoendelea kiganjani. HATUDANGANYIKI
hilo jamaa bogus kabisa!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom