Tuko
JF-Expert Member
- Jul 29, 2010
- 11,180
- 7,355
Diwani wa Kata ya LUTORO huko Kagera kwa tiketi ya CHADEMA amefanya Mauaji ya kutisha ya watu wa 4 huku moja ya watu hao akimtaka kabisa Koromeo.
Kyerwa. Diwani wa Kata ya Mabila kwa tiketi ya CCM, Wilaya ya Kyerwa, mkoani Kagera, anatuhumiwa kufanya mauaji ya Mwenyekiti wa Kitongoji cha Nyakatete, Danes Damian na Msaidizi wake, Johnson Damian wakidaiwa kufungiwa kwenye nyumba yake na kuteswa kabla ya kufariki.
Mauaji hayo yalitokea Machi 13, mwaka huu baada ya viongozi hao kutekwa wakiwa shambani na kundi la watu akiwatuhumu kuhusika na kifo cha mtoto wa diwani huyo, kilichotokea mwaka jana.
Kijana aliyeshuhudia utekaji huo, Kamugisha Damian alidai siku hiyo jioni akiwa na Danes wakichimba viazi, ghafla walivamiwa na kundi la vijana lililoongozwa na diwani ambaye alitoa amri wakamatwe naye akaambiwa alale kifudifudi.
Katika kipindi kisichozidi mwaka mmoja, watu sita wameuawa kijiji hicho cha Omukagando, mauaji yanayodaiwa kufanywa na kundi linalojiita ‘Hakuna Kulala'.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Philip Kalangi alithibitisha kuwapo kwa mauaji hayo na kwamba, diwani huyo anasakwa baada ya kutoroka na gari lake akiwa na baadhi ya vijana anaodaiwa kushirikiana nao.
Alitaja tukio hilo kama la kikatili na juhudi za polisi kumnasa diwani huyo na kundi lake, hazijafanikiwa baada ya kutorokea sehemu isiyojulikana. Ofisa Mtendaji Kata ya Mabila, Herman Leonard alisema alipigiwa simu na diwani akimtaka afike ofisini kupokea watuhumiwa aliodai anawatafuta muda mrefu.
Source Mwananchi...