Diwani machachari wa CCM kata ya Kamachumu, Muleba avua gamba na kuvaa gwanda

Direction is more important than speed. We are so busy looking at our speedometers that we forget the milestone.

TAARTIIIBU ILA KWA UHAKIKA!

Makada hakuna anayeshawishi watu kwenda CDM ni hasira tu na watu ni kama wanalipa kisasi. Makada waacheni wanaotaka kuwa ccm au UKAWA, 4U si chama lakin kina wanachama wa vyama mbalimbali. Mjue pia tunatofautiana kwa maauzi na uwezo wa kutulia kabla ya kufanya jambo. Kuna watuni first oriented kila jambo anataka awe wa kwanza tena wamuone. Ni njema kwake huyo lakini wapo ambao hupiga hesabu saa na kupima upepo ndo waamue, hao pia msiwaone wanachelewa. Kuna wanaoamua lakini kusema wanachelea, hao nao tunso. Nawaomba watu wangu itikaditunazo toka awali lakini mwelekeo wetu hadi sasa ni PUSH EDO INTO MAGOGONI kama anasimama lazima wawepo wa kumsukuma. Hakuna aliyemchafua EDO kama CCM lakini mbona bado yumo humo? Msimamo wa SLAA kwa EDO ulikuwa wa kisiasa na si wa dhati, SLAA hakuwa na kosa siasa zilimtuma na CCM hawana makosa siasa zawatuma, sisi tutende kwa dhati popote tulipo tuonyeshe kuwa OUR HERO IS THE NATIONAL HERO watatujua tu with time watatukubali. You are born a Tanzanian before you are a partisan somewhere do Tanzanian responsibilities responsibly utaona wanaulizana kwani huyu jamaa chama gani? Hapo sasa ndo utasema UKAWA AU CCM! LOVE YOU ALL MA FIGHTERS!

Copy copy copy copy
 
Mbona nashindwa kuelewa na ninachoka sana, hivi gamba likivaa gwanda linageuka kuwa kamanda?
 
Katika harakati zote hizi za mtifuano baina ya team Lowasa na chama chake nimegundua mambo kadhaa nyuma ya hii filamu:
1.Kuna ishu ya ukanda,hiihaijalishi mhisika anatoka chama gani lakini imradi anatokea ukanda huo na ana nguvu ya kuwafikisha katika ndoto zao kwa haina shida, mtu huyo hata kama ni mchafu kiasi gani akionekana anaweza kubeba maslahi mapana ya ukanda huo huyo ni mtaji mkubwa sana.

2.Kuna ishu ya imani (dini) najua hapa wengi wanaweza wakabisha sana kuonyesha kuwa wanalichukia jambo hili lakini kwa upeo wangu wa kuchunguza mambo haya nimegundua pia kwamba pia lina msukukmo mkubwa sana.hili la dini kwa kiasi kikubwa linahusu juu ya imani moja lakini tofauti ipo katika madhehebu, wapo wanaodhani kwamba kwa muda mrfu sana baadhi yamadhehebu yamekuwa yakitoa Marais wa inchi wakakati madhebu mengine yakiwa wasindikizaji tu.

3.Fedha katika kundi hili kuna mambo ya ajabu kidoogo, yani kuna jamii inaona ina kila kitu kwa maana ya uwezo wa kifedha, lakini wanataka angalau na wao watoe Rais wa inchi kuonyesha nguvu ya fedha walionayo ndio maana pamoja na ukweli kwamba aliyeteuliwa kuwania nafasi ya Rais kwa upande wa CCM yeye anauzika kwa jamii bado kwao sio jambo la msingi wanachotaka kupata heshima ya kuwa nao wametoa Rais wa inchi.

Jambo la kushangaza kidogo na ambalo linaweza kukupapicha ya haya ninayoyasema, pamekuwa na dhana kwamba CCM hamna kiongozi mzuri, tena wengine wakafikia hata kusema kumpata kiongozi msafi ndani ya CCM ni sawa na kumpata bikira katika kundi la machangudoa,wengine wakasema hata akishuka malaika juu mbinguni kuiongoza CCM bado haiwezi kuwa safi, lakini leo viongozi hao hao wachafu ambao hata malaika hawawezi kuwasafisha wakifika CDM wanakuwa wasafi kabisa,tena hata mabikira wanaweza patikana huko . hapo ndipo unapoweza kuona ilipojificha agenda kuu.ambazo ndizo hizo nilizoziainisha hapo juu.
Hii haihalalishi hoja yako ya ukanda na udini bali inahalalisha zaidi kuwa mfumo uliopo (CCM) ni mbovu na ndio maana mtu akiwa humo huonekana hafai kabisa na akitoka nje huonekana anafaa. Mfano mzuri ni kuwa ukiangalia wabunge wanaoukubalika na ccm ni wale ambao jamii inawaona ni bogus wakati wachache wanaoonekana wanakubalika ndio wanakataliwa na ccm (Lugola, Bulaya, Lembeli). Hata magufuli anayeonekana ni mtendaji mzuri lakini bado mpaka kufika hapo amelazimaka kufanya madudu kwanza, mfano kukubali mabango yaendelee kubaki barabarani bila mpangilio kwasababu tu Pinda kamwambia ayaache. Magufuli na wanaccm wengine kukubali kuunga mkono uvurugaji wa maoni ya wananchi kwa katiba mpya lakini watu hao wangekuwa nje ya ccm ungewasikia wanapigania maoni ya wananchi. Dawa ni kuing'oa ccm ili kubadili tabia ya nchi kuongozwa kienyeji.
Kuhusu Udini na ukanda: Ingekuwa kweli basi tusingetarajia Msuya amuunge mkono Membe, Nchimbi amuunge mkono Lowassa, Mgeja, Msindai, Msukuma, Matayo, Gachuma wamuunge mkono Lowasa, Kingunge amuunge mkono Lowasa, Msekwa, Malecela wampinge kwa nguvu kubwa Lowassa. Ukiangalia hiyo mifano michache utaona hakuna udini wala ukanda ila kuna maslahi mengine. Ishu ya udini na ukanda ni propaganda ya ccm tena ya muda mrefu kiasi kwamba baadhi ya watu wameanza kuathirika kwa kuangalia mambo kwa misingi ya ukanda bila kujali efficiency na hii ni propaganda pekee ambayo ccm wamekuwa wakiitumia na natarajia ktk kipindi hiki wataitumia kwa nguvu zote, bahati mbaya kwao ni kuwa hawaendi na wakati na hawana strategists wa uhakika, ccm imetekwa nyara na mbumbumbu, wanafiki, majambazi, wakwepa kodi, mafisadi na wachumia tumbo kiasi kwamba haiwezi sasa hivi kujua inachotakiwa kufanya.
 
Kuna watu humu hata hawajui kusoma alama za nyakati, wewe jumba linavuja karibu lianguke umeng'ang'ana kubaki ndani, aya, litakuangukia halafu utamlaumu nani, toka nje usalimike. Hahahahahahahahahahhahaha. Ni shiiiiiiiiiiida.. Mungu asingemchukua mapema marehemu Komba sasa hivi angekuwa anaimba mapambio ya kuisifia CDM. Wako wabunge wengi sana wale waliopanga foleni kwenda kumuona wakati ule wanangoja tu atamke wafungashe virago vyao. CCM kwa msukosuko huu itawachukua mda mwingi sana kukaa sawa. Believe that.
 
Ni kama ka upepo ka utani utani vile, ila kanaiathiri CCM kidogokidogo.

Hata mchwa hawashushi nyumba ghafla, ni kidogo kidogo bila hata wewe kujua. Wewe utaona mti wa kenchi mmoja umeliwa unapopanda kufanya marekebisho ghafla unashuka na nyumba yote!!
 
Hii ni kutokana na kutoridhishwa na utendaji ndani ya chama hicho, msuguano wa muda mrefu kati yake na Wabunge wa Muleba, Prof.Tibaijuka na Charles Mwijage n.k Aidha diwani huyu ni hatari sana kwa ushindi wa CCM wilayani humo anakubalika sana kuliko hata hao wabunge.
Kwani Huko Baraza La Madiwani Bado Halijavunjwa? Kama Lmeshavunjwa Yeye Bado Ni Mwenyekiti Wa WADC?
 
Back
Top Bottom