Diwani Kigamboni ampuuza Dk. Ndungulile | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Diwani Kigamboni ampuuza Dk. Ndungulile

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jul 14, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jul 14, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  [TABLE="width: 879"]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]  na Shehe Semtawa

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]
  DIWANI wa Chama cha Wananchi (CUF) Kata ya Kibada, amesema kauli ya Mbunge wa Kigamboni, Dk. Faustine Ndungulile, kuwa ni miongoni mwa madiwani wanne waliohongwa na Waziri wa Ardhi ili kuunga mkono ujenzi wa mji mpya wa Kigamboni haina athari kwake.


  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana diwani huyo, Juma Nkumbi alisema kauli ya mbunge huyo inaonyesha ni jinsi gani alivyofilisika kisiasa mbele ya jamii.

  Alisema kutokana na mbunge huyo kushindwa kwake kutoa ushahidi dhidi ya kauli yake hiyo, moja kwa moja imekidhihirishia chama chake kuwa hakuhusika na kitendo hicho.


  Nkumbi alisema mbunge huyo amekuwa akitapatapa, kutafuta umaarufu baada ya kupoteza imani kwa wananchi wa jimbo hilo kutokana na kushindwa kwake kwa makusudi kusimamia kero zao.


  Aliongeza kuwa kauli ya Dk. Ndungulile ni ya kutaka kuwachonganisha wananchi wa Kigamboni ambao hawapingi mradi huo isipokuwa wanataka tathmini ya mali zao ifanyike kwa kuzingatia haki na walipwe vizuri.


  Nkumbi alisema kwa kudhihirisha kuwa mradi huo unakubalika, ni hivi karibuni wenyeviti wa mitaa wa jimbo hilo, walimtembelea bungeni, na kumweleza mbunge wa Temeke, Abas Mtemvu, ambaye ni mwenyekiti wa wabunge wa Dar es Salaam kuwa kauli za Dk. Ndungulile ni mawazo yake binafsi.


  Akichangia hotuba ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi juzi, Dk. Ndungulile alidai kuwa madiwani hao wanne Juma Nkumbi (Kibada), Suleiman Mathew (Vijibweni), Albert Luambano (Tungi) na Doto Msawa, walihongwa na waziri ili wakubali mradi wa mji mpya wa Kigamboni
  .


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Jul 14, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  Hili Jimbo lina kazi hakuna Mbunge aliyelishika Mara Mbili
   
 3. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #3
  Jul 14, 2012
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  unataka kusema safari ya huyu jamaa imewadia?

   
 4. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #4
  Jul 14, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  Kabisa, Watu Wakubwa Wameisha Jipanga kulichukua na wana pesa haswa... Hilo jimbo ni hatari toka litengwe

  Hakuna anayelifanya lake 4 a second term
   
Loading...