Diwani Kata ya Masoko, Lindi anashikiliwa na Polisi kwa kukutwa na mbao zisizo na kibali

ALWATAN KIZIGO

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
539
642
Kinara wa biashara za magendo Wilayani Kilwa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashahuri ya Wilaya ya Kilwa Ndugu. Abuu Musa Mjaka (CUF) amekamatwa na Mbao za Magendo vipande 400 Nyumbani kwake.


Taarifa ambazo zimethibitishwa na mkuu wa wilàya ya Kilwa,Christopher Ngubiagai zimeeleza kwamba diwani huyo wa kata ya Masoko(CUF) anatuhumiwa kukutwa na vipande vya mbao takribani 400 ambazo vimevunwa bila ya kufuata utaratibu wa kisheria.

"Huyo mheshimiwa nikweli amekamatwa usiku huu.Yupo kituo cha polisi cha Kilwa Masoko.At amekutwa na mbao takribani 400 ambazo zilikuwa nyumbani kwake.Lakini hakuonesha nyaraka zinazoonesha kuwa ni halali," alisema Mwenyekiti huyo wa Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Kilwa.

Wilaya ya Kilwa ni miongoni mwa Wilaya zinazoongoza kwa biashara haramu ya magendo ya maliasili kna ndio maana Ofisi ya Mkuu wa Wilaya imeamua kupambana na Biashara za Magendo kwa udi na uvumba.
 
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kilwa Mkoa wa Lindi, Abou Mussa Mjaka amekamatwa na jeshi la Polisi.

Taarifa kutoka wilayani humo zinaeleza mheshimiwa Mjaka alikamatwa jana majira ya saa nne usiku nyumbani kwake mji mdogo wa Kilwa Masoko.

Taarifa hizo ambazo zimethibitishwa na Mkuu wa wilàya ya Kilwa, Christopher Ngubiagai zimeeleza kwamba Diwani huyo wa kata ya Masoko kupitia Chama Cha Wananchi (CUF) anatuhumiwa kukutwa na vipande vya mbao takribani 400 ambazo vimevunwa kinyume cha sheria.

Akithibitisha kukamatwa kwake Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama wilayani humo alisema”Huyo mheshimiwa nikweli amekatwa usiku huu.Yupo kituo cha polisi cha Kilwa Masoko.Inasemekana amekutwa na mbao takribani 400 ambazo zilikuwa nyumbani kwake. Lakini hakuonesha nyaraka zinazoonesha kuwa ni halali,”

Alipoulizwa Mwenyekiti wa CUF wa wilaya ya Kilwa, Seleman Bungara(Bwege) alisema hata yeye amesikia na hajui kwa undani kuhusu jambo hilo kwasababu yeye anaishi Kilwa Kivinje,wakati Mjaka anaishi Kilwa Masoko.

Halmashauri ya wilaya ya Kilwa ipo chini ya chama cha CUF kutokana na wingi wa madiwani wansotokana na chama hicho.Huku majimbo yote mawili(Kilwa kusini na kasikazini) wabunge wake wanatokana na chama hicho pia

1.jpg
 
Figisu za chama chetu kile.

Huyu diwani atakuwa Akikata kuunga mkono jihudi za mbatizaji.
 
Back
Top Bottom