Diwani Japhet Nanyaro mkombozi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Diwani Japhet Nanyaro mkombozi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Giddy Mangi, Jun 30, 2011.

 1. G

  Giddy Mangi JF-Expert Member

  #1
  Jun 30, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 833
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Ndugu wanajamvi jana nimepata kuona wananchi wakiwa na jazba na hamasa kubwa kumwona Mh Japhet Nanyaro diwani wa kata ya Levolosi (CHADEMA) akitembea kwa mguu maeneo ya stand ya viford huku kundi kubwa la wananchi vijana,wazee na kinamama akimwimbia "mkombozi mkombozi mkombozi" nikabaki nashangaa ndio nikagundua yote yalitokana na Msimamo wake kwenye Makubaliano waliyofikia madiwani wa Chadema na ccm yeye alikataa kushiriki na yeye hadi sasa anasema wazi Hamtambui Meya wala Naibu Meya.Hii nimeipenda sana viongozi kuwa na msimamo,NAOMBA KUWASILISHA.
   
 2. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #2
  Jun 30, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Ni muhimu wananchi hao kuendelea kumuunga mkono diwani wao kwakuwa hawakumchagua ili akagawane vyeo bali kupigania maendeleo yao kwa njia inayokubalika kisheria na kikanuni.

  Nawapongeza wananchi wa levolosi kwa kuchagua diwani makini.
   
 3. Donyongijape

  Donyongijape JF-Expert Member

  #3
  Jun 30, 2011
  Joined: May 28, 2010
  Messages: 1,451
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Mbona kama Hili Jina la Nanyaro ndiyo nimeona ni la diwani aliyeshiriki?? Hebu nikachimbe upya..sielewi elewi!
   
 4. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #4
  Jun 30, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Naomba kusahihisha kwamba anaitwa Efatha Nanyaro. Ni diwani wa Levolosi na member wa JF. Natumain ataiona hii thread na kuchangia hoja. Alikuwa mmoja kati ya waliochaguliwa kuunda kamati ya muafaka katika hatua za awali na nilipoongea nae juzi alinieleza kutokukubaliana na huu muafaka kwa kuwa haukuzingatia makubaliano, majadiliano wala mapendekezo waliyokuwa wameyafanya katika hatua za awali. Nadhani wananchi wake wanamshangilia kwasababu wanakubaliana na msimamo wake!
   
Loading...