Mjomba wa taifa
JF-Expert Member
- Apr 20, 2012
- 231
- 161
Wakazi wa Sinza Mori wametelekezwa na viongozi wa Serikali kwa kuonekana si sehemu ya Tanzania. Sitaki kuamini kuwa wakazi hawa wanapata adhabu ya kuwa na huduma mbaya za jamii kwa kuchagua diwani wa CHADEMA. Barabara ya Sinza Mori iendayo Johannesburg Hotel na Wanyama hotel toka Big Bon ina mahandaki, kwa ufupi haipitiki kwa magari, ni bodaboda tu ndio zinazosafirisha abiria kwa sasa. Eneo hilo halina maji toka uchaguzi wa 2010 ulipokwisha na mgombea udiwani kwa tiketi ya CHADEMA kuibuka mshindi.
Hali hii inaonekana kuwa ni hujuma ili Diwani huyu achukiwe na wapiga kura wake.
Diwani tafadhali usivumilie njama hizi.
Hali hii inaonekana kuwa ni hujuma ili Diwani huyu achukiwe na wapiga kura wake.
Diwani tafadhali usivumilie njama hizi.