Diwani CHADEMA akosa dhamana, aswekwa mahabusu

NDIKILO

Member
Joined
Feb 17, 2014
Posts
18
Reaction score
5
Diwani wa CHADEMA Kata ya Nyamanoro Ilemela Mwanza ,Bwana Abubakari Mwombeki Kapera leo amefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi Mwanza ili kujibu shitaka linalo mkabili la tuhuma ya kumfungia ndani ya ofisi Mkurugenzi wa manispaa ya Ilemela.Bahada ya kusomewa shitaka hilo Diwani alikana shitaka ndipo hakimu akamweleza wakili wa Diwani kuwa mdhamana ukowazi, mshitakiwa anatakiwa awe na wadhamini watatu wenye vitambulisho,barua iliyo pitishwa na mwenyekiti wa mtaana kuidhinishwa na Afisa mtendaji wa Kata,na kila mdhamini asahini bondi ya shillingi millioni tatu .Kwa baati mbaya wadhamini walio kuwepo mahakamani walikuwa ni wawili na barua zao zilikuwa zimepita kwa Afisa mtendaji wa kata,Hakimu ali mueleza wakili wa Diwani kwamba mdhamana upo wazi wadhamini waende wakarekebishe kasoro zilizopo kwenye barua zao za mdhamana na ndipowarudi mahakamani kumdhamini Mh;Diwani. Chakusikitisha ni kwamba ilipotimia saa saba mchana wa leo wadhamini watatu walikuwa wamekamilika na dosari za barua za mdhamana zilikuwa zimekamilika lakini kupitia kwa karani wa Hakimu huyo wadhamini wakaanza kuambiwa kuwa ,mara HAKIMU katoka nje ya CHAMBER ya mahakama,mara hakimu kaenda kuhuguza mtoto wake nyumbani, na kwasababu ya kizungumkuti hicho MH; Kapera amepelekwa magereza ya Butimba. Kutokana na mazingila haya ukurasa huu ulipo chunguza juu ya sintofahamu ya dhamana ya MH;DIWANI ukurasa humebaini kuwapo kwa mchezo mchafu kwenye mahakama hiyo ambapo pamoja na mambo mengine hasimu wa CHADEMA MEYA MATATA, ameonekana mazingira ya mahakama hii majira ya saa mbili asubuhi akiwa na hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo ambaye pia ni adui waChadema Mwanza,lakini pia wakati hakimu mwenyekesi hiyo akiendelea nakusoma masharti ya dhamana mtu wa karibu kimausiano na hakimu mfawidhi alimpatia kimemo akimu anaye sikiliza kesi hiyo ndipo uso wa hakimu huyo ukabadilika kutoka muonekano wa awali.

Haki uwa aipotei yaweza cheleweshwa ,lakini haki iliyo cheleweshwa nisawa na haki iliyo potea.

Matata afahamu Mungu ni mkubwa kuliko CCM,hipo siku hipo siku.
 
huyu diwani afungwe jela maisha..hana adabu ni taahira kama makamanda wa chadema.
 
Wanasema "Usichopenda kutendewa Usimtendee mwenzako"Na Mungu wa siku hizi bwana ni wa kidigitally zaidi,maana malipo yake atajibiwa tu.
 
SAFI SANA WEKA NDANI MACHOCHEZI HAYO ADABU IRUDI NCHI IMEPOTEZA WATALII SABABU YA FUJO ZAO HIYO NDO DAWA YAO AFADHALI SIKU HIZI HATA MAOFISINI TUNAPUMUA MAANA ILIKUWA JOTO TUPU CHADEMA IMEKUFA NA AMANI NCHINI Imerudi...
 
Huu uonevu una mwisho wake.
 
Suala la Mwanza wacha Matata aendelee 'kusaidia' kifo cha CCM. Lakini watu wa Mwanza watakaposema sasa basi, asitafutwe mchawi kabisa. It had been too much.
 
Shika adabu yako wewe,usioongee usichokijua...

kitendo alichofanya huyu diwani kimelaaniwa na watanzania wote.. anajipendekeza tu kwa wachaga,, ruzuku yenyewe inaishia kanda ya kaskazini tu kanda nyingine mtajiju
 
Its ze matter of time.....matata kawekwa kwenye utelezi tuuu atatumika baada atatupwa kweny jalala.....atapotea Mara ka srkl dhaifu ya ccm
 
Diwani wa CHADEMA Kata ya Nyamanoro Ilemela Mwanza ,Bwana Abubakari Mwombeki Kapera leo amefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi Mwanza ili kujibu shitaka linalo mkabili la tuhuma ya kumfungia ndani ya ofisi Mkurugenzi wa manispaa ya Ilemela.Bahada ya kusomewa shitaka hilo Diwani alikana shitaka ndipo hakimu akamweleza wakili wa Diwani kuwa mdhamana ukowazi, mshitakiwa anatakiwa awe na wadhamini watatu wenye vitambulisho,barua iliyo pitishwa na mwenyekiti wa mtaana kuidhinishwa na Afisa mtendaji wa Kata,na kila mdhamini asahini bondi ya shillingi millioni tatu .Kwa baati mbaya wadhamini walio kuwepo mahakamani walikuwa ni wawili na barua zao zilikuwa zimepita kwa Afisa mtendaji wa kata,Hakimu ali mueleza wakili wa Diwani kwamba mdhamana upo wazi wadhamini waende wakarekebishe kasoro zilizopo kwenye barua zao za mdhamana na ndipowarudi mahakamani kumdhamini Mh;Diwani. Chakusikitisha ni kwamba ilipotimia saa saba mchana wa leo wadhamini watatu walikuwa wamekamilika na dosari za barua za mdhamana zilikuwa zimekamilika lakini kupitia kwa karani wa Hakimu huyo wadhamini wakaanza kuambiwa kuwa ,mara HAKIMU katoka nje ya CHAMBER ya mahakama,mara hakimu kaenda kuhuguza mtoto wake nyumbani, na kwasababu ya kizungumkuti hicho MH; Kapera amepelekwa magereza ya Butimba. Kutokana na mazingila haya ukurasa huu ulipo chunguza juu ya sintofahamu ya dhamana ya MH;DIWANI ukurasa humebaini kuwapo kwa mchezo mchafu kwenye mahakama hiyo ambapo pamoja na mambo mengine hasimu wa CHADEMA MEYA MATATA, ameonekana mazingira ya mahakama hii majira ya saa mbili asubuhi akiwa na hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo ambaye pia ni adui waChadema Mwanza,lakini pia wakati hakimu mwenyekesi hiyo akiendelea nakusoma masharti ya dhamana mtu wa karibu kimausiano na hakimu mfawidhi alimpatia kimemo akimu anaye sikiliza kesi hiyo ndipo uso wa hakimu huyo ukabadilika kutoka muonekano wa awali.

Haki uwa aipotei yaweza cheleweshwa ,lakini haki iliyo cheleweshwa nisawa na haki iliyo potea.

Matata afahamu Mungu ni mkubwa kuliko CCM,hipo siku hipo siku.
Kapelekwa Magereza ya Wapi mkuu?hukumu imetolewa lini?ndo mana mnaishia pabaya shauri ya kuongea msicho kielewa, kijua wala kufaham
kajipange
 
Tatizo la watu kutokufahamu kati ya magereza na mahabusu hili. Kwani Huyo diwani amehukumiwa tayari.
 
Unapomtakia mabaya mwenzako wewe utaishi milele?wewe utatawala milele? Je siku yakikufika utakumbuka ulivyowatendea wenzako????Mungu hali ugali kwa mtu hata awe na upendeleo.
 
Back
Top Bottom