Diwani CCM atuhumiwa kutafuna mil. 4.8/- | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Diwani CCM atuhumiwa kutafuna mil. 4.8/-

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, May 26, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  May 26, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  [TABLE="width: 879"]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]

  Na Bryceson Mathias, Mvomero

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]
  DIWANI wa Sungaji, Athumani Mkimbu anatuhumiwa kwa kuhodhi fedha za ujenzi wa zahanati kiasi cha sh milioni 4.8.


  Madai hayo yalitolewa hivi karibuni na wananchi, viongozi na mtia saini wa fedha hizo, Kalolina Ferdinand.

  Walidai kuwa, fedha hizo zilitolewa na Benki ya NMB tawi la Madizini kisha kukabidhiwa kwa Mtendaji wa Kijiji Victor Kikoti na diwani huyo bila maandishi, lakini kamati ya ujenzi inapozihitaji inaambiwa hazipo, labda wakopeshwe.


  “Kwa nini fedha zilizochukuliwa benki kwa ajili ya ujenzi wa zahanati ziwe mikononi mwa diwani bila maandishi? Kwa nini basi zinapohitajika kwa ujenzi inadaiwa ziwe ni mkopo unaotolewa na diwani kwa Kamati ya Ujenzi?” alihoji Ryben Sembuche ambaye ni Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).


  Mtendaji wa Kijiji cha Mlaguzi, Kikoti alipoulizwa alisema hawezi kuzungumza na mwandishi na kutoa taarifa hizo kwa kuwa hamjui, lakini akadai kuwa ukweli wa fedha hizo upo kwenye maandishi ofisini kwake.


  Kwa upande wake diwani huyo alikanusha tuhuma zilizoelekezwa kwake, akisema hakupewa fedha hizo wala kwenda benki, lakini alikiri kuombwa msaada wa fedha ili kusaidia ujenzi wa zahanati.


  “Najua hayo ni maji taka wanayonimwagia wanasiasa wenzangu ili kunichafua kama walivyonichafua wakati wa ujenzi wa Sekondari ya Sungaji… ninachojua kamati ya ujenzi haina fedha, iliyopo ni ya kununulia kokoto tu,” alisema Mkimbu.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  May 26, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Bila ya kuwa na Katibu toka Chadema, huyu Diwani wa CCM angepotea na hizo pesa, ina maana Madiwani wa CCM wakati wa Chama kimoja walikuwa wanatokomea na pesa za maendelea kama za kwao.

  Mkubwa anachota, na Mdogo kama Diwani anachota cha kwake hivyo kila mtu ni fisadi ki-kwake hapo nani atambana nani?

  Nchi yetu ilikuwa imeisha, aheri sasa Upinzani unaingia ndani ya vioungo vya CCM hadi kwenye Kata CCM inaogopa sababu wananchi imejua hatari za kuwa na Viongozi walafi.
   
 3. MANGUNGO

  MANGUNGO JF-Expert Member

  #3
  May 26, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 1,538
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  Wizi kwa ccm ni kama mila fulani,yamekalia wizi tu! Fu##c#k them
   
Loading...