Disturbing question: Ni sahihi kwa Serikali kutangaza hadharani afisa wake amemaliza kazi ya siri?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,679
149,864
Hivi ni kawaida kwa serikali yoyote duniani kumpa mtumishi wake kazi fulani ya siri na baada ya kuikamilisha kazi hiyo serikali hiyo hiyo inamtangaza hadharani kuwa alipewa kazi fulani ambayo haitajwi na sasa anahamishiwa au anarudishwa kwenye kazi yake ya awali?

Alafu huko anakokwenda au kurudishwa baada ya kazi hiyo maalumu ya siri, wafanyakazi wengine wa umma watampokeaje au watamchukuliaje?

Anaemrithi ambae nae anatangazwa kuwa anaenda kukamilisha kazi iliyobaki atakuwa huru kweli kuifanya kazi yake hiyo ili hali nae ameshatangazwa hadharani kuwa anaenda kukamilisha kazi hiyo maalumu?

Kuna serikali imewahi fanya kitu kama hiki duniani?

Hii jambo mbona kwangu naliona la ajabu sana!!

Muda tu ndio utanijibu/utatujibu.

Tusubiri.
 
Japo wanaficha kuchemka kwao kwa kumteua mtuhumiwa wa Escrow na muonga wabunge ili bajeti ya wizara yake ipite

Lakini Wamedisclose Asset, hii ni hatari katika medani ya usalama.
Sasa hivi kila mtu anajua kuwa jamaa ni mtu wa kitengo na kwa hiyo inahatarisha connections zote za source ya taarifa ambazo jamaa alikuwa ametega, lakini ia wamemhatarishia usalama wake kwa kuwa huenda maadui wakajua kuwa kumbe yeye ndo aliwachoma katka ishu kadha wa kadha
 
Mbona kawaida serikali kufanya hivyo mbona hata Lowassa kapewa kazi za siri anazifanya Chadema.
Hata nyumbu sometimes huwa wanajiuliza kabla ya kuvuka mto, sijui na wewe kama huwa unajiuiza kabla ya ku-post chochote hapa JF!!
 
Tena hiyo ndio safi kwa kuwa watendaji watajua kuwa wanapelelezwa hivyo watafanya kazi kwa maadili na uadilifu mkubwa. Hiyo ndio safi sana. Maana humo maofisini hali ilikuwa mbaya sana.
 
Ukweli ni kuwa. mzee wa pushup alipitiwa hapo na kuamua kufanya masahihisho sasa huwezi mpa mtu kazi maalumu kwenye cheo cha capten halafu aimalize vzr umrudishe kuendelea na kazi kwa cheo cha coplo
 
Kuna watu wanamuota Edo wakati wote!Huyu mzee limbwata yake kali sana!
Kiukweli Magu alichemka!
 
unajiuliza maswali ya ajabu ajabu. Unataka serikali iseme ohh tumechemka?

mtu anayepewa kazi maalumu hawezi kuwa maswi kwasababu ni high profile. Watu wanaofanya unaenda chooni kwa amani ni watu wa kawaida sana huwezi kuwatambua. Hao ndio tunatambua mchango wao.

Serikali haindeshwi kwa kujuana au visasi. Inaendeshwa kwa misingi ya uwazi,taaluma na kuheshimiana.
 
Tena hiyo ndio safi kwa kuwa watendaji watajua kuwa wanapelelezwa hivyo watafanya kazi kwa maadili na uadilifu mkubwa. Hiyo ndio safi sana. Maana humo maofisini hali ilikuwsana.

Unapokuwa ccm akili na ufikiri wako unakuwa upo lege lege kama HAMY B.. tangu lini kachero au usalama akawa anafanya kazi ilhali akiwa anajulikana...

Ifike muda uwe unatumia akili na sio akili ya viroba
 
Unapokuwa ccm akili na ufikiri wako unakuwa upo lege lege kama HAMY B.. tangu lini kachero au usalama akawa anafanya kazi ilhali akiwa anajulikana...

Ifike muda uwe unatumia akili na sio akili ya viroba
Binafsi sikuona hata haja ya kumjibu huyu mtu.
 
Kachemsha hata ukiangalia tamko la balozi amelitamka kwa kutojiamini limetoka ghafla walikuwa hawajajipanga ndiyo maana chanel ten hawakulimalizia nadhani kasoro hiyo mtangazaji alikata hiyo sehemu
 
Kachemsha hata ukiangalia tamko la balozi amelitamka kwa kutojiamini limetoka ghafla walikuwa hawajajipanga ndiyo maana chanel ten hawakulimalizia nadhani kasoro hiyo mtangazaji alikata hiyo sehemu

Ni makususudi maana press release ya ikulu ishatoka
 
Back
Top Bottom