Asante sana mkuu, mimi ni mtu ambae siamini katika adhabu physical kama kupiga, kufinya au kugomba. Ninaamini maongezi yanaweza kusuluhisha kosa, mfano mtoto amepigana na mwenzake shuleni, unamuita na kumuuliza ni kwanini amefanya vile. Unaweza kukuta kosa si la mtoto ila yeye ni victim wa kuchokozwa na wewe kama mzazi ukishalifahamu kosa utajua jinsi ya kulirekebisha.Ni sahihi. Mtoto akipotoka na kukosa adabu anapaswa kupewa adhabu inayoendana na kosa. Hapa ninaongea kuhusu makosa wafanyayo watoto, yale ya kawaida.
Chukulia mtoto ameleta kiburi kutumwa jambo, kutoa lugha za kuudhi, kupiga au kupigana, utoro shuleni /mafunzo fulani, kuaibisha au kufanya vitendo vya aibu nk. Hapa anapaswa kupewa adhabu kama kufinywa, kutandikwa viboko nk. Na hiyo adhabu yapaswa kuwa kwa kiasi.
Mzazi au mlezi anapaswa kuepuka sana kuchubua ngozi, kung'oa nywele au sehemu ya mwili, kuunguza, kuponda /kugonga na kitu kizito au kuparuza mwili wa mtoto kwa "makucha" au meno.
Hapo basi, mtoa adhabu anapaswa kuelewa na kujikita katika kuonya, kukataza na kufundisha tabia iliyo njema.
Kwa hiyo, kama nia ya kutoa adhabu ni njema kuna mambo ya kuyaepuka. Kwa mfano, mtoto amevunja chombo au kifaa adhabu yaweza kuwa ni kumueleza kwa umakini tu. Mtoto aelezwe kuwa mara ingine awe makini kwa kila jambo alifanyalo. Hakikisha ameelewa.
Kumueleza bila kipigo humjengea mtoto akilini kuwa yeye ni muhimu na wa thamani kuliko vitu. Hii husaidia, itumike.
NB:Nia kuu ya adhabu ni kuonya, kufundisha, kurekebisha, kukumbusha, kurudisha kwenye mstari na kuijenga nidhamu ya kwelikweli. Si kukomoa, kuumiza au kuharibu tabia ya muadhibiwa.
Hatutakiwi kwenda kinyumbe na maneno ya Bible lakini pia nchi nyingi duniani haziruhusu kupiga mtoto kwa fimbo, na kama m-Kristo wa kweli unatakiwa kuheshimu sheria za nchi unayoishi pia.Mithali 23: 13-14 "Usimnyime mtoto wako mapigo; Maana ukimpiga kwa fimbo hatakufa.Utampiga kwa fimbo Na kumwokoa nafsi yake na kuzimu."
Sahihi mkuu. Ndiyo maana nikaandka iwe kwa kiasi na ilingane na kosa. Mimi bado ni muumini wa kutoa zawadi ya viboko viwili vitatu kwa nguvu ndogo kuadhibu mtoto mtukutu.Asante sana mkuu, mimi ni mtu ambae siamini katika adhabu physical kama kupiga, kufinya au kugomba. Ninaamini maongezi yanaweza kusuluhisha kosa, mfano mtoto amepigana na mwenzake shuleni, unamuita na kumuuliza ni kwanini amefanya vile. Unaweza kukuta kosa si la mtoto ile yeye ni victim wa kuchokozwa na wewe kama mzazi ukishalifahamu kosa utajua jinsi ya kulirekebisha.
Ninakuelewa mkuu, pia kama mzazi unawafahamu vizuri watoto wako. Ni kweli mtoto anapofanya kosa kama una hasira jaribu kunywa kwanza glass ya maji na ujitafakari. Kumpiga mtoto kwa hasira unaweza kumdhuru na wewe mwenyewe kuishia kwenye vyombo vya sheri. Kuongea na mtoto pia huongei nae kama best friend, unatakiwa umwangalie mtoto machoni na umuulize ni kwanini amefanya alichofanya na akueleze. Kama ni mkubwa kidogo unaweza kumwambia akuandikie kwenye karatasi akijieleza.Sahihi mkuu. Ndiyo maana nikaandka iwe kwa kiasi na ilingane na kosa. Mimi bado ni muumini wa kutoa zawadi ya viboko viwili vitatu kwa nguvu ndogo kuadhibu mtoto mtukutu.
Watoto wetu hawa tunaowalea huku uswahilini nyakati zingine bila viboko hawaendi. Ni njia mojawapo ya kumtia uchungu wa muda na awe na hofu yenye adabu.
Pamoja na yoooooteee, sidhani kama kuna mzazi anayeona fahari "kumdunda" tu mtoto wake. Angalizo langu :Mtoa adhabu jiepushe kutoa adhabu ukiwa na jazba, msongo wa mawazo, jizuie kutoa adhabu za kushtukiza kama makofi, mateke au hata matusi. Utsishia kuharibu zaidi.
Aiseee maneno tuu hayasaidii ....mtoto ni fimbo ( maandiko yamesema ). Na kumpa ushauri (maandiko yamesema ).Kama wazazi tuna wajibu wa ku-discipline watoto wetu, katika makuzi tuliyokulia wengi ilikuwa ni mwendo wa vitasa na fimbo kama njia ya adhabu. Njia hii ni njia sahihi ya kutoa mafunzo kwa watoto wetu, ni kweli wanaelewa ni kwanini wanaadhibiwa. Njia mbadala kama kuongea na mtoto na kumfanya aelewe kosa lake inawezekana katika hii jamii yetu?
Ninakaribisha maoni.
Ninakuelewa mkuu lakini inategemea mtoto umemlea katika msingi gani tangia anazaliwa, ninaamini maneno lakini na body language ya mzazi inabadilika wakati wa maongezi haya. Mtoto anafahamu kabisa kuwa hapa si picninic.Aiseee maneno tuu hayasaidii ....mtoto ni fimbo ( maandiko yamesema ). Na kumpa ushauri (maandiko yamesema ).
Sometimes fimbo zinazalisha manunda na waoga(watoto wasiojiamini).Aiseee maneno tuu hayasaidii ....mtoto ni fimbo ( maandiko yamesema ). Na kumpa ushauri (maandiko yamesema ).
Chit chat is for the not-so-serious matters.Bado ni mshamba wa ku-classify mada mkuu.
Mkuu ,nmeedit tena upya ......Ninakuelewa mkuu lakini inategemea mtoto umemlea katika msingi gani tangia anazaliwa, ninaamini maneno lakini na body language ya mzazi inabadilika wakati wa maongezi haya. Mtoto anafahamu kabisa kuwa hapa si picninic.
Sio kila kitu kitakachopitishwa na wenye mamlaka ni cha sahihi, na sio kila mamlaka imewekwa na Bwana kuna mamlaka nyingine ni za Giza.Hatutakiwi kwenda kinyumbe na maneno ya Bible lakini pia nchi nyingi duniani haziruhusu kupiga mtoto kwa fimbo, na kama m-Kristo wa kweli unatakiwa kuheshimu sharia za nchi unayoishi pia.
Ndiyo maana nimekueleza kuwa maongezi na mtoto, ambayo yanajumlisha firm tone with eye contact, unamuuliza mtoto ni kwanini umefanya ulichofanya? Unajua kuwa hili ni kosa? Umefiria jinsi ulivyomuumiza flani? Mtoto mwenyewe ataomba msamaha na kusema hatarudia tena.Mkuu ,nmeedit tena upya ......
Narudi kusimamia ,,, kiboko na busara za maneno humshep mtoto sana ..
Ngoja nikupe somo..
Mtoto anapozaliwa anakua na tabia mbili
Tabia ya asili na tabia ya biological .
Hii yaasili niile inayomfanya mtoto from no where anajua existence of God nahii ya biological anairith toka Kwa wazazi wake ,,,
SASA hizi tabia nimzazi pekee awezaye either kuziendeleza km ninjema au kuziendeleza ijapokua nimbaya ..
Nakatika hayo yote ,,, kama nimbaya ,,Nifimbo pekeee na kisha maneno ndiko kutambadilisha na kumweka mtoto ktk njia sawa.
Kuna mama mmoja alikua anawambia bintize , mkikua tumieni kondomu ,, aiseee wale watoto ni wagawaji balaaaa ...
Nkweli ndo maana nikasema fimbo na maneno ..ujue fimbo zinakua zinamkumbusha juu yakosa alolifanya kwaiyo yeye anakua anajiepusha .Sometimes fimbo zinazalisha manunda na waoga(watoto wasiojiamini).
Ninakuelewa mkuu lakini mamlaka za giza unazishinda kwa hekima si kwa kutumia nguvu ya ushindani.Sio kila kitu kitakachopitishwa na wenye mamlaka ni cha sahihi, na sio kila mamlaka imewekwa na Bwana kuna mamlaka nyingine ni za Giza.
Sky ndo maana nashauri fimbo kwajili ya kumbukumbu na maneno kwaajili ya kumponda moyo..Na zinafanya mtoto anakuwa Nunda anajua si nitapigwa tu.