Dirisha la usajili wanasiasa limefunguliwa TZ, je nani bei yake kama Neyma??

tikatika

JF-Expert Member
May 6, 2011
2,332
2,000
Kwa wale wazee wa kuweka mizigo, wazee wa soka , kabumbu a k a football, wanajua vizuri usajili wa wachezaji wa mpira. nakumbuka katika mikutano mara kadhaa nimemsikia kocha msaidiz mmoja akisema tumesajili wachezaji bora kabisa. Kocha huyo wanamwita taratibu taratibu.

Duniani kwa sasa mchezaji ghari zaidi ni neyma. Wa pili pogba kama sijakosea watatu ni Ronaldo.

Siasa zetu kwa kipinndi kirefu tulikua tunacheza siasa za ridhaa! Yaan walikua wanajitolea wakisubili mshara na posho tu. Ila kwa sasa wanasiasa wetu ni wa kulipwa na kuuzwa pia kama sio kujiuza.

Daraja la kwanza lilikua ni usajili wa madiwani.
Katika daraja la ligi kuu naona limepamba moto ni la wabunge. Kuna mashabiki pia wananunuliwa kwa kupiga sana ngoma za kushangilia timu yake kwa kupewa wadhifa na mzigo juu. Ila mshangiliaji mmoja hawajamtendea haki mpaka leo anasotea naye ni prinses murooooo!!

Soko sio wazi sana ila biashara imepamba moto. Hongera kwa mbunifu wa biashara hii . Huenda tutapata akili kuchagua wanasiasa bora na bei yao ikawa nzuri. Maana kwa sasa inasemekana wanaofika bei ni wale wachezaji wa kawaida . Bei zao zinafika 1 billion mpaka 2 billion. Kwa sasa natafuta atakaye tikisa kibubu cha timu ya manunuzi.

Sasa sijui ambaye bei yake ni
Kubwa kama ya mess. Et wana JF nani bei yake itakua kama Neyma au kuwa ghari kama Mess!??

Nani wa kukataa offa toka timu tajiri ya kijani??
Wewe ungeamin Kafulia angeingia timu ile huku ametoka kushindana nao mahakaman kwa kumnyima uchezaji wa timu pinzani. Leo et kajiunga kwao!! Hahahahaha nacheka kama mazuri. Hongera kocha Sizonje kwa ubunifu huu!

Kesho sijui kesho kutwa atasajiliwa mmoja toka sijui simanjiro!! Huu utakua usajili wa mchezaji wa kawaida. Namtafuta wa bei kubwa hadi mashabiki wasikitike kwa kupoteza hela!!

Dirisha limefunguliwa sijui siku ya kufungwa .
Mashabiki wenzangu msiwaamin hawa wachezaji wetu wakipewa offa nzito wanatimua. Usifanye mchezo kuna timu ya madalali imejaa watu makini wa kushawishi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom