Jonathan alukwu kutua msimbazi, je yatatimia?

franckkimm

JF-Expert Member
Aug 25, 2016
440
852
Imefahamika kuwa mabosi wa Simba SC wapo kwenye mazungumzo na winga wa klabu ya Sporting Lagos ya Nigeria, Jonathan Alukwu kufuatia maagizo ya kocha mkuu wa timu hiyo, Abdelhak Benchikha katika usajili wa dirisha dogo.

Taarifa za uhakika zilizotufikia kutoka ndani ya klabu hiyo zinasema kuwa klabu hizo mbili zimeanza mazungumzo hayo na nyota huyo ambaye amepewa kipaumbele kuchukuwa nafasi ya Saido Ntibazonkiza.

Mtoa taarifa hizi ameongeza kuwa, hatua ya kuwania saini ya nyota huyo ni baada ya Saido Ntibazonkiza huenda akaondoka Msimbazi na kwenda klabu ya APR ya Rwanda katika usajili huu wa dirisha dogo.

“Skauti ya Simba na Benchi la Ufundi la kocha Benchikha imeridhika na Alukwu, kwa kuwa mwalimu anafahamu uwezo wake na endapo watafanikiwa kumpata watakuwa wamefanikiwa kuziba nafasi ya Saido ambaye muda wowote ataondoka,” amesema mtoa habari huyo.

Ameongeza kuwa viongozi wanakamilisha masuala ya usajili kulingana na mapendekezo ambayo wameyapokea kutoka kwa benchi hilo la ufundi linaloongozwa na Benchikha.

Meneja wa Habari na Mawasiliano ya Simba, Ahmed Ally amengumzia ishu hiyo ambapo amesema suala zima la usajli wa timu hiyo kwa sasa limebakia kwa kocha mkuu wa timu hiyo ndiyo anaweza kuamua wachezaji anaowataka ndani ya kikosi chake.

Dirisha dogo la usajili limefunguliwa Desemba 15, mwaka huu na utafungwa Januari 15, mwakani.

Nawasilisha!!!
Screenshot_20231223-091751.jpg
 
Nawasilisha!!!View attachment 2850401
Cna iman kabisa na huu uongozi ktk usajili,muda utaongea
 
Back
Top Bottom