Dira ya wana Jamiiforums mwaka 2014

Donpela

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2011
Posts
2,040
Reaction score
592
Habari wana JF,

Poleni sana na majukumu yanayowakabiri katika harakati zenu na kila siku na hongereni sana kwa hatua za kimaisha kila siku.
back to the topic, nilikua najiuliza kitu kwa mda kidogo, nikasema ngoja tu share wote ili tuweze pata dira kamili ya wanajamvi wengi kuokana na mwaka huu 2014.

Dira ya wana jamii mwaka huu itatabiriwa kutokana na mtazamo wako wewe mwana jamiiforums juu ya pendekezo la ku comment jukwaa gani limekua likitumika ipasavyo ( poleni kwa mods maana mnakesheshwa kwenye majukwaa haya)

Jinsi ya kupiga kura

Please kila mwana jf ata comment namba kuashiria kura yake

1 - Kama unadhani jukwaa la mmu ndo limekua likipambazwa kila mda, tupate dira ya watanzania ni wako ki rafiki na mapenzi zaidi mwaka huu

2 -Kama unadhani jukwaa la siasa ndo limekua likibamba sana, tupate dira ya watanzania wako busy na siasa mwaka huu kutokana na patashike ya uchaguzi mkuu mwakani

3 -Kama unadhani jukwaa la mambo ya kikubwa limebamba sana, tupate dira mwaka huu watanzania wameamu kujikita katika mambo yetu yaleee ya kikubwa zaidi ( e.g wazee wa 0712.. mimeno nje)

4 -Kama unadhani jukwaa la nafasi za kazi/jukwaa la elimu kama limeguswa sana, tupate dira watanzania wameamua kujiajiri/kuajiri na kupata mafunzo ya ujasiriamali

5 -Kama unathani jukwaa la chit chat limebamba, kupata taswira watanzania mwaka huu ni uzaramo mwanzo mwishoo, story tu na kusogeza mda..(please dont be offended.)

6 -Kama unadhani majukwaa mengine ndo yanabamba (kama una mtazamo wa majukwaa mengine ambayo hujaona katika 1-5)

Angalizo
- please no offense given, none taken
- majukwaa yaliyotajwa yamezingatia utaratibu maalum.
- ukumbi wako ruksa hata kuharibu kura,

karibuni wana jamii
 
Namba 1 itapata kura nyingi maana bandiko lako liko humo...ni sawa na kumtafutia kura mgombea wa cdm makao makuu ccm..
 
Mbona hujataja ya katiba mupya, manaake napo tupo kwenye mchakato
 
Namba 1 itapata kura nyingi maana bandiko lako liko humo...ni sawa na kumtafutia kura mgombea wa cdm makao makuu ccm..

hahaha mkuu umekomenti ki jukwaa la siasa siasa..ulivomalizia apo
pole alafu naskia uchakachuzi umeanza kwenye bunge la katiba
 
Nimeshindwa kuelewa lengo la mada!
 
si mdau wa huko sana...i just try to be fair...

safi sana mkuu,,mungu akujalie busara zaidi..maana jukwaa lile ase lastahili muongozo wa kiroho
 
Nimeshindwa kuelewa lengo la mada!

mkuu tulitaka kujua mtazamo wa mwaka huu kwa kuangalia mwanzo wa mwaka majukwaa gani yanatumika sana na wadau ..through this tunaweza pata picha kamili ya mwenendo wa mwaka mzima..
#ceterisparibus assumption
 
mkuu tulitaka kujua mtazamo wa mwaka huu kwa kuangalia mwanzo wa mwaka majukwaa gani yanatumika sana na wadau ..through this tunaweza pata picha kamili ya mwenendo wa mwaka mzima..
#ceterisparibus assumption

Tunatumia njia gani kujua hayo?
 
Tunatumia njia gani kujua hayo?
njia rahisi ya mtazamo wako tangu mwaka umeanza na mwenendo wa watu humu jf...unaona jukwaa gani kati ya hayo tajwa hapo juu matano ndo yamekua yakipendelewa sana / kuwa very active / kuwavutia wadau wengi humu jf🙂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…