Kama Ukawa wanataka waendelee vizuri, wakiwa imara miaka yote na wasitetereke hata baada ya uchaguzi, basi waunde chama kimoja kipya chenye sera mpya, viongozi wa vyama hivyo wakubali kuachia madaraka yao na wagombee upya kupata viongozi wapya wa chama kipya.
Hapa ni kuonesha kuwa Ukawa (Umoja wa Katiba ya Wananchi) ni muungano wa magirini kwa sababu kama kungekuwa na nia ya dhati ya wapinzani kuunganisha nguvu, wangeshafanya huko nyuma lakini kwa sababu za ubinafsi kama siyo uroho wa madaraka, hawakuungana. Wakatukanana!
Imeandikwa na; Luqman Maloto
Aisee eti huyu naye Luqman Maloto ni Investigative journalist! My foot
Kufikia 2015 wagonjwa wa BP Tanzania watakuwa wameongezeka kwa kasi ya ajabu and very sad pia vifo vinavyotokana na BP vitaongezeka kwasababu MSD hawana hata hiyo pesa ya kuagiza madawa ya BP.
Baada ya ushirikiano wa UKAWA wenzako CCM walianza kuimba wimbo wa ITIKADI. Kwamba UKAWA hautadumu kwasababu wana ITIKADI tofauti na Watanzania huwa wanaichagua CCM kwasababu ya ITIKADI yake.
Hao wakereketwa walipoulizwa ITIKADI ya CCM wanayoisimamia ni ipi, wakaingia mitini na hatukuwasikia tena wakiimba wimbo wa ITIKADI.
Sasa na wewe Luqman umekuja na single ya UKAWA kulete MACHAFUKO, very pathetic!
Paragraph ya kwanza unashauri eti UKAWA waungane wafanya chama kimoja! Yaani huo ushauri unajiona eti ni bonge la GT. Hivi unajua process ya kuanzisha Chama kipya hadi kupata usajiri na kushiriki uchaguzi?! Tena Chama ambacho kinategemewa kuwa na NGUVU ya kuindoa CCM madarakani? CCM ikisajiri chapucahpu na kukipatia usajiri wa kudumu? kwa mda huu uliobaki before 2015?! Huu ushauri hauna tofauti na kumshauri binadamu kikimbilia mtoni pindu akifukuzwa na mamba! Huo USHAURI kaeni nao ma-CCM.
Hiyo paragraph ya pili umejitahidi kuzunguka mbuyu lakini lengo lako lilikuwa hilo to discredit UKAWA. Lakini jaribu hata kutumia akili KIDOGO basi katika kujenga hoja zako!
Madhumuni/malengo makuu mawili ya UKAWA ni
- Kutetea katiba ya wananchi
- Kuindoa CCM madarakani
BTW, hii makala yako it will make a good article for UHURU news paper, I advise you to send it there!