Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 (Tanzania Development Vision 2025)...

Ukishakuja kwenye suala la utawala bora,kwakweli hata hao viongoz hawajui,wao wanasema utawala bora ni uwazi na utawala wa sheria,hawataji principles nyingine za utawala bora,na bahat mbaya miongoni mwa wananchi ndo hatujui kabisaa UTAWALA BORA,wananchi wanautamani 2015 kwa kuneemeka na fulana,pilau na pombe,
 

Umepewa sh ngapi ili kumpigia debe huyo savimbi?
 

Umesahau wezi wa Epa walivyosamehewa na kuamlishwa warudishe fedha walizo iba?
 

Mkulima anaandaa shamba tangu mwanzo,anapalilia,akisha vuna mazao yake ndio wanakuja na ngonjera ya stakabadhi gharani,wizi mtupu!
 
Mtoto wa mfugaji kaimu Waziri wa fedha mh Mwigulu Nchemba sasa anaenda kuitoa nchi kutoka katika hali ya sasa kuelekea katika nchi ya kipato cha kati na hili amelidhihirisha wakati akiongoza mafunzo ya takwimu jana trh 18/sept mjini Morogoro
Ambapo alichukuwa nafasi hiyo kusisitiza ufuatiliaji wa hali ya Umasikini katika kaya kwa Vitendo na na kuacha hadithi kwenye utendaji wa kumkomboa Mtanzania katika lindi la umasikini, na kuongeza kuwa Uhimalishaji wa ofisi za TAKWIMU ni muhimu ili serikali iweze kuwa na mipango ya maendeleo ambayo ni linganifu na Takwimu zilizopo wakati ambao Serikali inafunga mkanda kwa ajili ya kuwa nchi ya kipato cha kati, ni lazima tuwe na takwimu bora na sahihi alisema Mwigulu Nchemba. Pamoja na mambo mengine mh Mwigulu Nchemba ambaye anafananishwa na Sokoine kwa utendaji wake wa kazi alichukua nafasi hiyo kuipongeza ofisi ya TAKWIMU kwa namna inavyoendelea kufanya kazi na kusaidia wadau mbali mbali na kuendelea kuchangia shughuli za maendeleo na kuwaomba wananchi kutoa taarifa sahihi wanapofanyiwa udadisi ili zisaidie kupanga mikakati ya maendeleo. Na kuhitimisha kuwa ili katika Usimamizi wa Kodi na Matumizi yake ni lazima Takwimu ziwiane na kipato na kule fedha zinakoelekea, ili kuondoa gap kati ya walionacho na wasionacho ni muhimu kuwepo na takwimu sahihi.
 
Alikuwepo wapi miaka tisa yote iliyopita ? Wakati ufalme wa CCM umebakiza mwaka mmoja kuangushwa ?
 
"Mwigulu Nchemba sasa anaenda kuitoa nchi kutoka katika hali ya sasa kuelekea katika nchi ya kipato cha kati"!!!!!?????? Really?

Ungeripoti tukio ukatuachia nafasi wasomaji wako watoe tathmini...


Au amekutuma umpigie propaganda?
 
Alikuwepo wapi miaka tisa yote iliyopita ? Wakati ufalme wa CCM umebakiza mwaka mmoja kuangushwa ?

Alikuwa katibu wa uchumi na fedha wa chama baadaye naibu katibu mkuu wa chama bara sasa ndiyo naibu waziri wa fedha tanzania,nadhani umeelewa.
 
Maendeleo haya husemwa kabla ya uchaguzi ukipita tu wanatangaza mpango mpya wa kurudisha pesa walizotumia katika uchaguzi hasa kuhonga....ndoto za mchana nchi yangu kupata maendeleo chini ya CCM..Haiwezekani
 
mwigulu chapa kazi usiangalie pembeni watanzania wanaheshimu kazi yako.
 
Waliitoa wapi 2005 na sasa wamefikisha wapi... kuelekea 2025?
Au walikuwa hawajaanza mwendo?
 
Mikakati baada ya miaka amsini :A S-eek:
 
Wanasiasa ni majanga matupu waliomba wapewe kura,wawaletee maisha bora watanzania ndani ya miaka5,miaka 5 ikapita hakuna cha maisha bora kwa kila mtanzania hata mimba ya maisha bora haikuonekana,wakaomba waongezewe kipindi kingine cha miaka 5 ambacho kiko ukingoni napo hamna kitu.Walichofanikiwa zaidi ni kulitoa Taifa kwenye unafuu wa madeni na kuwa kinara wa madeni.Sasa wamekuja na kali zaidi ya kulifanya taifa kuwa lenye kipato cha kati tena siyo leo mwaka 2015 sijui nani atakuwepo kipindi hicho.
 
Alikuwepo wapi miaka tisa yote iliyopita ? Wakati ufalme wa CCM umebakiza mwaka mmoja kuangushwa ?

Ndo kwanza amepewa nafasi hata miaka 2 bado lakini utendaji wake wa kazi unaridhisha
 
Maendeleo haya husemwa kabla ya uchaguzi ukipita tu wanatangaza mpango mpya wa kurudisha pesa walizotumia katika uchaguzi hasa kuhonga....ndoto za mchana nchi yangu kupata maendeleo chini ya CCM..Haiwezekani

Km mpaka hapa uoni kazi ya chama cha mapinduzi hakika na wewe utakuwa miongoni mwa wale ambao kazi yao kubwa ni kubeza.
 
Tutasikia uongo wa kila aina kuelekea 2015, miaka 53 na utajiri wa kumwaga hamjaweza kufanya lolote la maana katika kuinua viwango vya maisha ya W atanzania walio wengi, sasa mnadai kwa hii miaka 11 hadi kufikia 2025 ndio mtafanya maajabu!!!! Tumechoka na uongo wenu wa miaka nenda miaka rudi huku mkiendelea kuiangamiza Tanzania.

 

Tutoe taarifa sahihi ili vipaombele vya serikali viwe revealed
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…