Diplomasia mashakani

Diplomasia mashakani

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
359,910
Reaction score
828,534
Wananchi Kenya watishia kuwatimua Watanzania wanaofanya biashara na kazi Kenya
"Mimi kama Mbunge wa Nyatike, jimbo langu linapakana na Tanzania na Uganda. Nyatike ipo kwa kona ya Kenya kabisa, mahali ukivuka unaingia Tanzania na ukienda kidogo unaingia Uganda. Kitu ambacho hawa watu wetu walikuwa hawajaelewa vizuri, hii mambo ya freedom of speech kwa East Afrika nzima, ipo Kenya peke yake. Ukivuka mpaka, hayo mambo unaacha hapa Kenya.

Hawa majirani zetu watu wa Tanzania hawajafika hii kiwango ya Kenya. Hapa Kenya unaweza kusema kitu unataka lakini siyo Tanzania. Sisi tunaosafiri mara kwa mara kwenda Tanzania kwa biashara tunaelewa. Tanzania kuna amani lakini ni ya hofu. Mtanzania hata ndugu yake awe arrested illegally hawezi kuongea, ataenda kupost kwa social media. Na huko social media atafungua fake account ili asijulikane ni yeye. Au atapeana story kwa prominent figures wamsaidie kusema lakini kwa masharti wasimtaje kwa jina. That is the level of cowardice walionayo watu wa huko.

Kwa hiyo hawa activists watu wetu kabla hawajaenda huko walitakiwa wawe wanajua hiyo situation. Siasa ya Kenya na siasa ya Tanzania iko tofauti kabisa. Hii demokrasia tunafurahia hapa Kenya mahali watu wanaweza kuexpress vile wanataka, hakuna kwa kwa jirani. Na siyo Tanzania tu hata ukienda Uganda, DRC, Rwanda, Burundi na South Sudan hakuna. So the whole East Africa community, freedom of speech ipo Kenya peke yake.

So kama tunataka mabadiliko ili majirani wawe na freedom of speech kama tuliyonayo, itachukua muda. Bado hawa watu wako kwa usingizi mzito ambao Kenya iliamka kwa huo usingizi over 20 years ago. Hizi initiatives za kudefend human rights kwa wenzetu zinaitwa ghasia. Kenya mtu akiwa abducted ukimsemelea awachiliwe unaitwa human rights defender, lakini kwa Tanzania unaitwa mchochezi unahatarisha amani. Kwahiyo hizi initiatives za kudai human rights ziishie kwa mipaka ya Kenya, wakienda kwa jirani waheshimu sheria za huko. Ni ngumu kutetea watu ambao hawajakuwa tayari kutetewa. Give them time watajitetea wenyewe" Tom Odege, Mbunge Nyatike.!
IMG-20250523-WA0092.jpg
 
Inakuwaje mtu kwenye akili Timamu unaanza kuwasikiliza na kuwategea sikio watu ambao unaona kabisa wamelewa pombe mpaka ufahamu kuwatoka.
 
Back
Top Bottom