Diplomasia inafungua milango ya fursa

Diplomasia inafungua milango ya fursa

Maryam Malya

Senior Member
Joined
Nov 29, 2021
Posts
116
Reaction score
260
Na Mwl Udadis

Taarifa ya Benki kuu ya Tanzania inaonyesha bidhaa za zetu zinazouzwa nje zimeongezeka hadi kufikia thamani ya Dola za kimarekani Bilioni 1.2 kutoka Milioni 908.6 mwaka 2020. Ongezeko hili ni kielelezo muhimu kinachoonyesha matokeo ya utekelezaji wa diplomasia ya uchumi.

Diplomasia ndio inayowezesha mipaka ya nchi jirani na masoko kufunguliwa kwa wafanyabiashara wetu na pia ni kigezo muhimu kuvutia wawekezaji (FDI's). Mpaka mwishoni mwa 2021 Mamlaka kama EPZA tayari ilikuwa imesajili miradi yenye thamani ya takribani Dola za kimarekani milioni 86.86 ndani ya mwaka mmoja pekee.

Juhudi za Rais Samia kuimarisha diplomasia ya nchi yetu ni moja ya mambo muhimu yanayopaswa kuungwa mkono kwa vitendo na watanzania wote bila kujali itikadi za vyama vya siasa. Leo hii tumeona Mh. Rais tayari yuko barani Ulaya kuhakikisha diplomasia inaendelea kuimarika.

Mwaka 2021 tuliona Taasisi za kifedha zikifanya vizuri ambapo Benki kama NMB iliweza kutengeneza faida ya takribani bilioni 289, CRDB ikitengeneza zaidi ya Bilioni 267 na kufanikisha kupata takribani Bilioni 459.9 kutoka Umoja wa Mataifa (GCF) kwaajili ya kusaidia katika miradi endelevu(Green financing).

MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU MMBARIKI RAIS WETU.
 
Akili yako haina akili.
Kuuza Ngorongoro kwa warabu wenzie..?!
 
Hizi ziara anaenda as act alone kwa nini hawachukui wakuu wa polisi,wakuu wa jeshi wakuu wa manispaa ,unamkuta mtu ni mkuu wa manispaa ajawai kuona ata trafic light,nasema uongo ndugu zangu ?

Mfano nimeona clip ya Mwinyi Huseni akionyeshwa namna polisi wa uarabuni ni jinsi gani wanaangalia nchi nzima usiku na mchana wakiwa ofisini ,bahati nzuri yule asikari akizungumza nae inaonyesha alisoma kwenye lugha za kigeni na akiongea kiswaili fasaha,mpaka mwinyi amefarijika na kumpa maelezo mengi tu kuhusiana na uangalizi wa raia na mali zao.

sasa kama pale angekuwepo Mkuu wa polisi au wa polisi si lazima siro wapo wasomi wengi ndani ya jeshi la polisi angalau na wao wakafungue macho na kujua huko nje ya dunia yetu kuna nini kinachoendelea.
 
Akili yako haina akili.
Kuuza Ngorongoro kwa warabu wenzie..?!
Alieuza ni msukuma au mnyamwezi sio mwarabu ni kama vile akina Ali Hasani Mwinyi Isac sepetu wanatokea pande za nyanda za juu,itakuwa kigoma au tabora..
 
Na Mwl Udadis

Taarifa ya Benki kuu ya Tanzania inaonyesha bidhaa za zetu zinazouzwa nje zimeongezeka hadi kufikia thamani ya Dola za kimarekani Bilioni 1.2 kutoka Milioni 908.6 mwaka 2020. Ongezeko hili ni kielelezo muhimu kinachoonyesha matokeo ya utekelezaji wa diplomasia ya uchumi.
Naomba kueleweshwa tunauza bidhaa (finished product zenye value addition) au tunauza malighafi ?

Kama tunauza malighafi huoni kwamba ni vema tukawekeza zaidi kwenye kutengeneza valuable product na kuhakikisha tuna soko la ndani na sio kutegemea wanunuzi kutoka nje pekee
Diplomasia ndio inayowezesha mipaka ya nchi jirani na masoko kufunguliwa kwa wafanyabiashara wetu na pia ni kigezo muhimu kuvutia wawekezaji (FDI's). Mpaka mwishoni mwa 2021 Mamlaka kama EPZA tayari ilikuwa imesajili miradi yenye thamani ya takribani Dola za kimarekani milioni 86.86 ndani ya mwaka mmoja pekee.
Kama tunauza malighafi sidhani kama tuna shortage of buyers au kama tutaendelea (Africa) kuwa a dumping ground zidhani kama tutakosa bidhaa; Hata kama tunafanya long term projects tusisahau hata short term..., sasa kama wakulima wanakosa masoko na mbolea kwa bei nafuu huenda vipaumbele vyetu ni vice versa
Juhudi za Rais Samia kuimarisha diplomasia ya nchi yetu ni moja ya mambo muhimu yanayopaswa kuungwa mkono kwa vitendo na watanzania wote bila kujali itikadi za vyama vya siasa. Leo hii tumeona Mh. Rais tayari yuko barani Ulaya kuhakikisha diplomasia inaendelea kuimarika.
Kufanya hiki sio kwamba kile kisifanyike..., afanye yote na huenda afanye delegation katika Diplomasi awashirikishe Mabalozi zaidi huenda ikawa more efficient....
Mwaka 2021 tuliona Taasisi za kifedha zikifanya vizuri ambapo Benki kama NMB iliweza kutengeneza faida ya takribani bilioni 289, CRDB ikitengeneza zaidi ya Bilioni 267 na kufanikisha kupata takribani Bilioni 459.9 kutoka Umoja wa Mataifa (GCF) kwaajili ya kusaidia katika miradi endelevu(Green financing).

MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU MMBARIKI RAIS WETU.
How does that impact huku chini wakati loans bado ni double digits na hazilipiki ? Wala siwezi kulaumu Benki hapa with rate of defaulters....

Unajua shortcut ya yote haya ? Ni kuhakikisha disposable income ya wananchi inaongezeka na hio can only be done kwa kuwa na sera za kuongeza ajira zenye ujira (no shortcut) na kwa nchi yenye vyanzo lukuki kama hii this is doable....
 
Hizi ziara anaenda as act alone kwa nini hawachukui wakuu wa polisi,wakuu wa jeshi wakuu wa manispaa ,unamkuta mtu ni mkuu wa manispaa ajawai kuona ata trafic light,nasema uongo ndugu zangu ?
Mfano nimeona clip ya Mwinyi Huseni akionyeshwa namna polisi wa uarabuni ni jinsi gani wanaangalia nchi nzima usiku na mchana wakiwa ofisini ,bahati nzuri yule asikari akizungumza nae inaonyesha alisoma kwenye lugha za kigeni na akiongea kiswaili fasaha,mpaka mwinyi amefarijika na kumpa maelezo mengi tu kuhusiana na uangalizi wa raia na mali zao.
sasa kama pale angekuwepo Mkuu wa polisi au wa polisi si lazima siro wapo wasomi wengi ndani ya jeshi la polisi angalau na wao wakafungue macho na kujua huko nje ya dunia yetu kuna nini kinachoendelea.
Akiongozana na hao unaowataja kuna watu watalalamika kuwa raisi anaponda mali za umma kwa kuongozana na viongozi wengi ktk ziara zake.
 
Hizi ziara anaenda as act alone kwa nini hawachukui wakuu wa polisi,wakuu wa jeshi wakuu wa manispaa ,unamkuta mtu ni mkuu wa manispaa ajawai kuona ata trafic light,nasema uongo ndugu zangu ?
Mfano nimeona clip ya Mwinyi Huseni akionyeshwa namna polisi wa uarabuni ni jinsi gani wanaangalia nchi nzima usiku na mchana wakiwa ofisini ,bahati nzuri yule asikari akizungumza nae inaonyesha alisoma kwenye lugha za kigeni na akiongea kiswaili fasaha,mpaka mwinyi amefarijika na kumpa maelezo mengi tu kuhusiana na uangalizi wa raia na mali zao.
sasa kama pale angekuwepo Mkuu wa polisi au wa polisi si lazima siro wapo wasomi wengi ndani ya jeshi la polisi angalau na wao wakafungue macho na kujua huko nje ya dunia yetu kuna nini kinachoendelea.
viongozi wengi wa UAE hasa Dubai na Oman wana asili ya Zanzibar. Hivyo, unapowakuta mara nyingi wanazungumza kiswahili. Hata Mabalozi wadogo wanaoletwa Zanzibar wanazungumza Kiswahili. Pia hilo limechochea uwekezaji kwani wanahisi kuwekeza Tanzania ni kama nyumbani.
 
Back
Top Bottom